Skip to main content

Posts

Showing posts from December 20, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt.Mwigulu aweka Jiwe la Msingi mradi wa maji Ruangwa - Nachingwea

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 21, 2025 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji  Lindi-Ruangwa- Nachingwea, katika kijiji cha Chimbila A wilayani Ruangwa Mkoani Lindi. Mradi huo wa maji kutoka Mto Nyangao uliopo Wilaya ya Lindi, unatekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa mazingira vijijini (RUWASA), na utanufaisha vijiji 56 katika Wilaya za Ruangwa (vijiji 34), Wilaya ya Nachingwea (vijiji 21) na Wilaya ya Lindi (Kijiji 1). Mradi huo utagharimi kiasi cha shilingi Bilioni 119 na mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 67% ya utekelezaji. Mradi huo umeanza utekelezaji February 2023 na unatarajiwa kukamilika June 2026 kwa hatua ya kwanza. Hata hivyo ifikapo February 2026 baadhi ya vijiji vitaanza kupata huduma ya Maji. Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ameridhishwa na hatua ya utekelezaji wa mradi ambayo imefikiwa. “Hivi ndivyo Rais Dkt. Samia anataka kuona namna kazi inavyofanyika. Hapa tumeona asilimia ya utekelezaji ni kubwa kuliko ...

Dkt Mwigulu akagua hali ya Bandari ya Barazani mkoani Lindi

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 21, 2025 amekagua hali ya bandari ya Barazani mkoani Lindi na kuiagiza Mamlaka ya Bandari Tanzania kukamlisha kwa haraka michakato ya awali ya kitaalam ya ujenzi wa mradi wa Bandari ya Ngongo wilayani Lindi mkoani Lindi. Amesema kukamilika kwa bandari ya Ngongo kutasaidia kuwaondolea adha watumiaji wa bandari inayotumika sasa ya Barazani ambayo hali yake haiendani na mahitaji ya sasa. Dkt. Mwigulu ameongeza kuwa kukamilika kwa ujenzi wa bandari ya Ngongo kutaleta chachu ya maendeleo mkoani humo kwani bandari ya Lindi imeanza kuchangamkiwa na wafanyabiashara, wakiwemo wa nchi jirani.

Dkt. Mwigulu Aweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Kampasi ya Lindi ya Udsm

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kampasi ya Lindi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika eneo la Ngongo mkoani Lindi na kusema kwamba huo ni uthibitisho wa dhamira ya Serikali ya kupanua fursa za elimu ya juu nchini. “Uwekezaji huu ni utekelezaji wa vitendo wa nguzo ya pili ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika kujenga uwezo wa watu kifikra, kiubunifu, kufanya uchambuzi, kutatua changamoto, pamoja na kuwa na utaalamu na umahiri katika nyanja mbalimbali za maisha,” amesema. Akizungumza na viongozi na mamia ya wananchi wa mkoa wa Lindi waliofika kushuhudia uzinduzi huo leo (Jumamosi, Desemba 20, 2025), Waziri Mkuu amewapongeza viongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuamua kutekeleza maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kupanua huduma za elimu ya juu katika maeneo ya kimkakati kama vile Mkoa wa Lindi. “Maono haya ni ya kwake mwenyewe Mheshimiwa Rais. Zilipotolewa fedha za mradi huu kwa vyuo vikuu kama vya Dar es Salaam na Mzumbe, alisema ...

Waziri Simbachawene Apokelewa na Askofu Dkt. Bagonza

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene amewasili wilayani Karagwe mkoani Kagera kumuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Mwigulu Nchemba katika Ibada ya Ubarikio wa Wachungaji na Wadiakonia,tukio ambalo litafanyika kesho tarehe 21 Disemba,2025 katika Kanisa Kuu la  Lukajange Dayosisi ya Karagwe. Waziri Simbachawene amepokelewa na Askofu Dkt.Benson Kalikawe Bagonza ambae ni Askofu wa Kanisa  la Kiinjili la Kilutheri Tanzania wilayani Karagwe ambapo jumla ya Mashemasi watano watapata uchungaji.

Diwani Katikiro Awapa Elimu ya Maendeleo Wananchi wa Bweri

 DIWANI wa kata ya Bweri katika halmashauri ya Manisipaa ya Musoma mkoani Mara Mh Paul Katikiro amewataka wananchi wa kata hiyo kujenga utamaduni wa kuchangia shughuli za maendeleo badala ya kutegemea serikali pekee. Mh Katikiro ameyasema hayo Desemba 19 mwaka huu 2025 katika kikao cha kwanza cha maendeleo ya kata kilichoboreshwa na kufanyika katika ukumbi wa chuo cha ufundi (Bweri FDC). Amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mh Dkt Samia Suluhu Hassan imefanya mambo makubwa ya maendeleo hasa katika sekta ya Elimu,Afya,Barabara pamoja na huduma nyingine za kijamii na kwamba juhudi hizo zinapaswa kuungwa mkono na nguvu za wananchi. "Maendeleo hayawezi kuja kwa kutegemea serikali kwa kila Kitu,lazima uanze kisha uiambie Serikali tumeanza tumefika hapa,....kuna baadhi ya shule zinachangamoto za ukosefu wa uzio,wapo walikubali kwa kuniita diwani niende tukafanye harambee ili tuiambie Serikali tunefika hapa,hata hiyo Marekani mnayoiona hakuibuka kama uyoga ilianza kama mchicha...

Diwani Katikiro awapa elimu ya maendeleo wananchi wa Bweri