SERIKALI imeendelea kusisitiza utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2023 inayotaka taasisi zote za umma kutenga asilimia 30 ya bajeti ya ununuzi kwa ajili ya makundi maalum, yakiwemo vijana, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu, ikiwa ni mkakati wa kukuza uchumi jumuishi nchini. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa PPRA, Bw. Dennis Simba, wakati akiwasilisha mada kuhusu fursa za zabuni za umma kupitia Mfumo wa NeST, katika kongamano la kuadhimisha miaka 104 ya kuzaliwa kwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Kongamano hilo lilifanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma na kufunguliwa Rasmi na Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi. Katika wasilisho lake, Bw. Simba alibainisha kuwa mfumo wa NeST umeboreshwa ili kurahisisha ushiriki wa makundi maalum katika zabuni za umma, huku akihimiza vijana kuchangamkia fursa hizo ili kujijengea uwezo wa kiuchumi. “Sheria hii siyo tu mwongozo wa manunuzi, bali ni chombo muhimu cha kuwawezesha wananchi kiuchumi, hasa makundi maalumu ...
Marato tv - Sauti ya Jamii