Skip to main content

Posts

Showing posts from February 10, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Mwigulu Azindua Uwanja wa Ndege Mtemere

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 11, 2026 amezindua uwanja wa ndege Mtemere uliopo katika kijiji cha Mloka, mkoani Pwani kwenye hifadhi ya Taifa ya Nyerere. Uzinduzi wa uwanja huo umeenda sambamba na uzinduzi wa miradi mingine 20 (kufanya miradi 21) ikiwemo Malango ya kuingilia Hifadhini, vituo vya taarifa kwa wageni, kambi za wageni, Eneo la Kupumzikia wageni, Nyumba za wageni, Hosteli za Wanafunzi, kituo cha kufuatilia ikolojia, na vituo vya askari. mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa  wa miaka mitano unaolenga kukuza uchumi wa nchi yetu kupitia shughuli za utalii.

Waziri Dkt. Gwajima Apongeza Mchango wa Sekta Binafsi Katika Maendeleo na Ustawi wa Jamii

‎*Na WMJJWM – Arusha* ‎Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mheshimiwa Dkt. Dorothy Gwajima, amepongeza mchango wa sekta binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kuimarisha ustawi wa jamii, hususan watoto, vijana na familia, wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya SOS Children’s Villages Tanzania iliyofanyika Ngaramtoni, wilayani Arumeru mkoani Arusha. ‎Dkt. Gwajima amesema ameridhishwa na utekelezaji wa programu zinazolenga malezi chanya, ulinzi wa mtoto, maendeleo ya awali ya mtoto (ECD) na uwezeshaji wa kiuchumi kwa vijana na familia, akisisitiza kuwa jitihada hizo zinaendana na sera na miongozo ya Taifa. Amesema malezi bora na mazingira salama kwa watoto ni msingi wa kujenga Taifa imara. ‎Aidha, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali, mashirika ya kiraia na jamii katika kuhakikisha utekelezaji wa programu za maendeleo una matokeo endelevu, huku akiwataka wadau kuendelea kuzingatia mipango ya Taifa, hususan katika kukomesha ukat...

Tanzania Yaandika Historia Mpya Katika Sekta ya Kinga ya Jamii-Waziri Kikwete

 Tanzania imeandika rekodi mpya ya kihistoria katika sekta ya Kinga ya Jamii! Hatua hii imekuja baada ya nchi yetu kutajwa rasmi kuwa miongoni mwa nchi 17 duniani zenye mifumo bora zaidi ya hifadhi ya jamii.  Mafanikio haya si ya bahati mbaya, bali ni matokeo ya utekelezaji thabiti wa maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yanayolenga kuinua ustawi wa kila Mtanzania. Kauli hiyo imetolewa na Nchi Ofisi ya Rais,Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete , wakati akihitimisha mkutano wa siku mbili wa wadau wa sekta ya Kinga ya Jamii jijini Arusha, Februari 10, 2026. Waziri Kikwete ametaka kuwepo kwa utekelezaji wa kina wa maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kuhusu kinga ya jamii kwani tayari maono yake Rais Samia yamesababisha mafanikio makubwa . Amewataka watekelezaji wa sera hiyo kujipanga vyema na kuweka nguvu katika kutekeleza dira na maono yaliyotolewa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.  Aidha ametoa wito kwa...

Dkt. Mwigulu Kukabidhi Miundombinu ya Utalii

 Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 11, 2026 ameelekea katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere ambapo anatarajiwa kuzindua na kukabidhi Miundombinu ya Utalii.

Dkt. Mwigulu Amwakilisha Rais Dkt. Samia Katika Mkutano wa 43 wa Auda-Nepad

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Afrika (AUDA-NEPAD) uliofanyika kwa njia ya Mtandao, Ofisini kwa Waziri Mkuu Magogoni Jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika mkutano huo, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema kuwa Tanzania inaendelea kujidhatiti katika kutekeleza Ajenda 2063 kupitia uwekezaji wa kimkakati katika miundombinu, kilimo na maendeleo ya rasilimali watu.  “Miongoni mwa miradi muhimu ni Mradi wa Umeme wa Maji wa Julius Nyerere, ambao utazalisha megawati 2,115 za umeme pamoja na mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) unaounganisha Tanzania na Burundi pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili kuimarisha muunganisho wa kikanda” Dkt. Mwigulu amesema kuwa Tanzania inaamini kuwa Afrika inaweza kuwa mahali bora zaidi pa kuishi kwa vizazi vya sasa na vijavyo, endapo kila mmoja atajitoa kikamilifu kulinda na kuhifadhi mazingira kwa njia endelevu. “Ili kuf...

Dkt.Mwigulu aongoza Kikao cha Kamati ya Kitaifa ya AFCON 2027

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amekutana na Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) kwa ajili ya kupitia hatua mbalimbali zilizofikiwa katika maandalizi ya michuano hiyo mikubwa itakayofanyika mwaka 2027 katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amefanya kikao hicho leo Jumanne (Februari 10, 2026) Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo hayo, Waziri Mkuu amepongeza kazi kubwa inayofanywa na kamati hiyo, akieleza kuridhishwa na kasi na mwelekeo wa maandalizi yanayoendelea.  “Maendeleo yaliyofikiwa hadi sasa yanaonesha dhamira ya dhati ya Serikali katika kuhakikisha Tanzania inakuwa mwenyeji bora wa michuano hiyo”.   Waziri Mkuu amesisitiza kuwa ni muhimu kuwepo kwa ushirikishwaji wa sekta zote, “mawaziri, makatibu wakuu pamoja na watendaji wengine hakikisheni mnazishirikisha sekta zetu kila mmoja katika eneo lake, tunataka kuona matokeo chanya katika michuano hii”. Aidha, Mheshimiw...