Skip to main content

Posts

Showing posts from August 10, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

RAIS DKT. SAMIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA TEC

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 10 Agosti, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania kupitia Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (Tanzania Episcopal Conference - TEC), Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma. Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na TEC na kujadili masuala mbalimbali ya kitaifa yanayoigusa jamii, yakiwemo ya kisiasa, imani na maendeleo, pamoja na kuimarisha amani, mshikamano na kujenga mustakabali mwema wa Taifa. Aidha, mazungumzo hayo yaligusia umuhimu wa nafasi ya madhehebu na Viongozi wa Dini katika kulea jamii yenye maadili mema, uwajibikaji na mshikamano, ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika ustawi na maendeleo endelevu ya Taifa. Mheshimiwa Rais aliwashukuru Maaskofu hao kwa kuona umuhimu wa kukutana na kujadiliana naye masuala yenye tija kwa Taifa na kuwahakikishia dhamira yake ya kuendeleza utamaduni wa kushauriana na kushirikisha Viong...

HOSPITALI YA SINO MIKOCHENI YAUNGA MKONO DIRA YA RAIS SAMIA UTALII TIBA

  Mwandishi Wetu, Dar es Salaam. WATANZANIA wameanza kunufaika na huduma za matibabu ya kibingwa zinazopatikana nchini, hali inayopunguza gharama na ulazima wa kusafiri nje ya nchi kutafuta matibabu. Mkurugenzi Mtendaji wa Universal Medical Tourism, Dk. Sharif Mollel, amesema huduma hizo zinapatikana katika Hospitali ya SINO iliyopo Mikocheni, Dar es Salaam, inayomilikiwa na wawekezaji kutoka China katika sekta ya afya. Amesema kampuni yake inashirikiana na hospitali hiyo katika kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibingwa, teknolojia za kisasa za matibabu pamoja na baadhi ya huduma zinazotokana na tiba za jadi za China, zinazojulikana kama Traditional Chinese Medicine. Dk. Mollel amesema uwepo wa huduma hizo nchini unawapa Watanzania nafasi ya kupata matibabu bila kulazimika kuingia gharama kubwa za tiketi za ndege, malazi, visa na matumizi mengine yanayotokana na safari za matibabu nje ya nchi. “Lengo letu ni kuona Watanzania wanapata huduma nyingi zaidi hapa nchini. Kama huduma...

TADB YATOA MIKOPO YA SH15 BILIONI ZANZIBAR, HEMED AWASIHI WANANCHI KUCHANGAMKIA FURSA

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka wananchi hususan wakulima , wafugaji na wavuvi kuchangamkia fursa zinazotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kukuza mitaji ya biashara zao. Ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Benki ya maendeleo ya kilimo Kanda ya Zanzibar Afisini kwake Vuga. Amesema Benki ya maendeleo ya Kilimo ina mchango mkubwa katika kuwawezesha kifedha na kuwapatia ujuzi wa kisasa wakulima, wafugaji na wavuvi ili waweze kukuza mitaji yao hivyo TADB wanapaswa kufikisha elimu kwa wananchi ili waweze kutambua fursa za kilimo na ufugaji zinazopatikana kupitia benki ya maendeleo ya Kilimo. Aidha, Mhe. Hemed amesema wananchi wengi bado hawajaziona fursa za uwekezaji wa Kilimo zinazopatikana Zanzibar hasa vijijini ambako kuna maeneo mengi ya kufanya uwekazi endelevu na stahmilivu wa Kilimo. Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka viongozi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Kanda ya zanzibar kuhakiki...

SUGUTI VIEW HOTEL MAZINGIRA RAFIKI KWA WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI YACHOCHEA MAENDELEO NCHINI.

Na Mwandishi wetu Jovina Massano,Musoma. MABORESHO na mazingira rafiki kwa wawekezaji na wafanyabiashara hapa nchini yanayofanywa na Serikali ya awamu ya sita yazidi kuchochea Maendeleo  nchini. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Suguti View Hotel Masegenya John Chiganga mara baada ya kuzinduliwa na kuwekwa kwa jiwe la msingi katika hotel hiyo na Kiongozi wa mbio za mwenge ndugu Wazo Michael Mwang'onda akiwa na wakimbiza Mwenge wa uhuru kitaifa. Amesema uwepo wa miundombinu muhimu maeneo ya vijijini kunazidi kuwavutia wawekezaji na wafanyabiashara na kuzidi kuchochea Maendeleo yanayokwenda kuongeza vipato vya wananchi wengi na kukuza uchumi kwa jamii na Serikali. Amefafanua kuwa Uwekezaji huo umegharimu kiasi cha Shillingi za kitanzania zaidi ya  million 100.17 zikiwa zimetokana na biashara ya uvuvi katika ziwa Victoria. Mradi huo umewezesha baadhi ya jamii katika kijiji Cha Suguti kupata soko la uuzaji wa bidhaa za mazao ya nafaka na uvuvi katika eneo hilo. Sanjari na hayo pia ...

PAMBA TANZANIA: SAFARI YA TANI MILIONI MOJA NA CHANGAMOTO YA TIJA

 Tanzania imezalisha tani 222,057 za pamba katika msimu uliopita, kiwango ambacho bado kiko mbali na lengo la Serikali la kuongeza uzalishaji wa zao hilo hadi kufikia tani milioni moja ifikapo mwaka 2030. Pengo hilo linaonyesha ukubwa wa kazi iliyopo mbele ya Serikali, wakulima na wadau wa tasnia ya pamba katika kuongeza uzalishaji wa zao hilo muhimu kwa uchumi wa nchi. Kutoka tani 222,057 hadi tani milioni moja kunahitaji uzalishaji kuongezeka kwa zaidi ya mara nne.  Hili haliwezi kufikiwa kwa kuongeza maeneo ya kilimo pekee, bali linahitaji kuongeza tija kwa kila ekari, kuboresha ubora wa pamba na kuimarisha mnyororo mzima wa uzalishaji na masoko. Pamba ni miongoni mwa mazao muhimu ya biashara nchini Tanzania, likiwa chanzo cha kipato kwa maelfu ya wakulima na likichangia shughuli mbalimbali za kiuchumi katika maeneo yanayozalisha zao hilo. Hata hivyo, pamoja na umuhimu wake, uzalishaji bado haujafikia kiwango kinacholingana na uwezo wa Tanzania. Changamoto kubwa ni tija ndo...

UREKEBISHAJI WA MAGEREZA WABADILI MAISHA YA MUSSA MALALE, SASA NI FUNDI KIYOYOZI KATIKA MRADI WA UWANJA WA NDEGE WA MSALATO

 Na Ssgt Mawazo Mtondo - DODOMA Jeshi la Magereza linaendelea kutoa Programu mbalimbali za Urekebishaji kwa Wafungwa ili kuwapa ujuzi utakaowasaidia kujitegemea kwa kujiajiri au kuajiriwa pindi wamalizapo vifungo magerezani. Magereza Tanzania Habari, tumefanya mahojiano na aliyekuwa mfungwa, Ndugu Mussa Malale, ambaye ni miongoni mwa wanufaika wa programu za urekebishaji zinazotekelezwa na Jeshi la Magereza. Akizungumza katika mahojiano hayo, Ndg. Malale amesema kipindi chote alichokuwa gerezani alipewa mafunzo mbalimbali ya ufundi stadi, ikiwemo ufundi wa viyoyozi (Air Conditioning – AC), yaliyotolewa na wakufunzi wenye uzoefu na kumjengea ujuzi uliokuwa msingi wa mafanikio yake baada ya kumaliza kifungo. Amesema baada ya kuachiliwa huru alianza kufanya kazi ya kuendesha gari la kubeba mchanga, lakini shughuli hiyo ilisimama baada ya gari kuharibika. Baadaye, rafiki yake alimshauri kutafuta kibarua katika mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege Mpya wa Msalato jijini Dodoma. Malale, am...

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amemtembelea na kumjulia hali, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, katika makazi yake, Kawe Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 10 Agosti 2026.