Skip to main content

Posts

Showing posts from July 16, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Fahamu Kuhusu Chuo Kikuu Cha Kilimo na Teknolojia Cha Mwalimu Julius K. Nyerere Butiama Kilichopo Mkoani Mara

Na Emmanuel Chibasa Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Mwalimu Julius K. Nyerere Butiama[MJNUAT] ni taasisi mpya ya umma iliyoanzishwa rasmi mwaka 2012. Makao yake makuu yako wilayani Butiama, mkoani Mara. Kampasi kuu ya Chuo Kikuu ipo kilomita 38 kutoka Musoma mjini karibu na barabara kuu ya Musoma-Arusha, na kilomita 15 kutoka Kiabakari kutoka barabara kuu ya Musoma – Mwanza na kilomita 5 kutoka makao makuu ya Wilaya ya Butiama. Serikali ya awamu ya nne iliamua kuanzisha chuo hiki cha umma kwa heshima ya Mwalimu, Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye aliamini kwamba kilimo kwa mapana yake kinabaki kuwa njia ya kutegemewa ya maisha ya Watanzania wengi walioko vijijini Chuo kikuu kinalenga kuwa katika hatua kuu ya mabadiliko ya kilimo nchini Tanzania. Pia inajitahidi kuwa mdau wa kikanda na kimataifa katika Elimu na Mafunzo ya Kilimo yenye ubunifu na mwitikio wa jamii (AET). Chuo hiki kinalenga kufanikisha hili kwa kukumbatia dhana za Chuo Kikuu cha Kizazi cha T...

Fahamu Jinsi ya Kutambua Habari na Taarifa za Uongo na Uzushi Kwenye Mitandao ya Kijamii

Na Emmanuel Chibasa Habari za uongo na uzushi ni miongoni mambo yanayoisumbua dunia kwa sasa. Wanao kutiana na  changamoto hii ni watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwa ni kupata habari au shughuli za kibiashara. Kuna aina mbalimbali za habari za uzushi na uongo ambazo hatumika zaidi kwenye mitandao ya kijamii kama vile facebook na YouTube  ambapo kichwa cha habari hutofautiana kabisa na maudhui ya habari yenyewe au kichwa cha habari pekee bila ya kuwa na maudhui ya habari katika kueleza zaidi juu ya habari husika. Mara nyingi madhumuni ya upotoshaji huo ni  watu kutaka kujipatia pesa kwa njia ya matangazo au kujiongezea watazamaji na wasomaji. Lakini habari au taarifa huzo hutumika kuharibu heshima na sifa ya watu kwenye jamii. Kwa mujibu wa takwimu za mawasiliano ya robo ya mwaka inayoishia machi 2024 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (Tcra), Idadi ya laini za internet imeongezeka kutoka milioni 35.9 kwa robo mwaka iliyoishia desemba 20...

Mhe.Dkt Tulia Ackson Afungua Kikao Cha Kujadili Amani, Haki na Taasisi Madhubuti

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akifungua Kikao cha Kibunge wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Juu la Siasa la Umoja wa Mataifa juu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu, Jijini New York, Marekani leo tarehe 16 Julai, 2024. Kikao hiki kinaangazia lengo nambari 16 lenye kusisitiza Amani, Haki na Taasisi madhubuti. Aidha, namna ambavyo Mabunge yatasaidia kuzishauri na kuzisimamia Serikali zao katika kutimiza lengo hilo.  Mabunge yameshauriwa kujikita kwenye uwazi, usawa na uwajibikaji kama njia mojawapo ya kutimiza lengo linaloangaziwa.

Waziri Nape Aagiza Tanesco na Tarura Kupeleka Huduma Maeneo Yanayojengwa Minara ya Mawasiliano

 Na Angela Sebastian  WAZIRI wa habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Mnauye ameagiza Shirika la umeme nchini Tanesco na Wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) kupeleka huduma za umeme na barabara maeneo yote yanapojengwa minara ya mawasiliano. Amesema hii itasaidia wadau hao kukabiliana na changamoto kadha wa kadha ikiwemo kuingia gharama za manunuzi ya petrol na diseli kuendesha mitambo minara hiyo. Nape amesema.hayo baada ya kuwasili mkoani Kagera kwa ziara ya siku moja  kupokea taarifa ya mkoa na chama cha Mapinduzi (CCM) ambayo inaonesha kuimalika kwa mawasiliano mkoani humo. Amesema kuwa agizo la kupeleka huduma hilo ni la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwamba Tarura,Rea na Tanesco wahakikishe wanafikisha huduma hizo maeneo inapojengwa miundombinu ya minara kama ilivyo katika taasisi nyingine kama vile shule na hospitali na maji. Amesema makadilio ya kuendesha mnara kwa kutumia dizeli kwa ni makubwa na kutumia fursa hiy...

Rais Dkt Samia Atoa Wito Kwa Watanzania Kulinda Miundombinu ya Barabara Kwa Matumizi Endelevu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wasafirishaji wote nchini pamoja na Wananchi kuhakikisha wanalinda miundombinu ya barabara inayojengwa na Serikali kwa kutofanya shughuli za kijamii kama kulima, kuchimba pembezoni mwa barabara  pamoja na kazi nyingine zinazoathiri barabara. Dkt. Samia ametoa wito huo Wilayani Kalambo mkoani Rukwa, leo Julai 16, 2024 mara baada ya kufungua barabara ya Sumbawanga - Matai - Kasanga Port (km 107) iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami. “Ujenzi wa barabara ni gharama sana, ukijenga kilometa moja ya barabara ni sawa na kujenga vituo vitatu vya afya pamoja na kuweka vifaa tiba ndani yake kwahiyo niwaombe sana tutunze barabara zetu”, amesema Dkt. Samia. Dkt. Samia ameeleza kuwa kukamilika kwa barabara ya Sumbawanga - Matai - Kasanga Port (km 107) kwa kiwango cha lami utasaidia kutatua changamoto ya usafiri na usafirishaji wa bidhaa kwa wananchi wa Mkoa wa Rukwa. “Kabla ya barabara hii kujengwa...