Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma. Ukuaji wa teknolojia unazidi kuimarisha huduma mbalimbali ambapo kwa kiasi kikubwa mifumo imekuwa sehemu ya kuwezesha maboresho ya huduma rahisi kwa wananchi. Kwa umuhimu huo Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imehakikisha inaendelea kushiriki kikamilifu kuendana na mabadiliko ya teknolojia mkupunguza malalamiko kwa wananchi hasa katika huduma ya maji kwa kuja na njia mbadala ya matumizi ya teknolojia kwa kuleta mita za malipo kabla. Hivi sasa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Musoma(MUWASA) kupitia Mkurugenzi Mtendaji Esther Gilyoma kwa kuhakikisha malalamiko yanapungua tayari mita za malipo kabla zimeanza kufungwa. Gilyoma amesema ataendeleza ushirikiano na wananchi na yupo tayari kutoa na kupokea taarifa za huduma ya maji pamoja na uondoshaji wa maji taka. Aidha katika mpango wa mwaka wa fedha wa 2026 mamlaka imejipanga kuwahudumia wananchi kwa kutumia teknolojia mpya na inaendelea kutii agizo la ser...
Marato tv - Sauti ya Jamii