Skip to main content

Posts

Showing posts from February 10, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Gavana BoT Aongoza Uzinduzi wa Ripoti ya Ufuatiliaji wa Fedha Zinazoingia Kutoka Diaspora

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, ameongoza uzinduzi wa Ripoti ya Ufuatiliaji wa Fedha zinazoingia katika nchi kutoka kwa Watanzania wanaoishi  ughaibuni (Cross-border Remittance Diagnostic), katika ofisi za BoT jijini Dar es Salaam.  Akizungumza kwenye uzinduzi wa Ripoti hiyo, Gavana Tutuba amelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) kwa msaada wake wa kiufundi katika kufanya utafiti huo ambao una mchango mkubwa katika kustawisha sekta ya fedha nchini. “Nianze kwa kutoa shukrani zangu za dhati kwa UNCDF kwa msaada wa kiufundi walioutoa  ambao ulisaidia katika katika utafiti huu, ambao ripoti yake inazinduliwa leo. Pia, ninashukuru sana kwa wadau wote wa sekta ya fedha walioshiriki katika utafiti huu zikiwemo wizara na mashirika ya umma, mabenki, watoa huduma za mitandao ya simu, watoa huduma za malipo kwa niia kielektroniki, na taasisi zinazotoa huduma ndogo za fedha,” amesema Gavana Tutuba. Aidha, amesisitiza kuwa fe...

Serikali yaainisha Mikakati ya Kuwawezesha Vijana Kushindana Kwenye Soko la Ajira

Na Mwandishi Wetu. BUNGE limeelezwa mikakati mitano inayofanywa na serikali katika kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana nchini na namna kumudu ushindani kwenye soko la ajira. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema hayo leo Februari 10, 2025 bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Mpendae (CCM), Mhe. Toufiq Turky aliyehoji kuna mpango gani wa kuwandaa vyema vijana waweze kushindana katika soko la ajira ndani na nje ya Tanzania ili kukabiliana na upungufu wa ajira nchini. Akijibu swali hilo, Waziri Kikwete ametaja mipango ya serikali katika kuwaandaa vijana ili kumudu ushindani katika soko la ajira ndani na nje ya nchi. Mhe. Kikwete amesema, mipango hiyo ni pamoja na kubuni na kutekeleza programu maalum zinazowawezesha vijana kujifunza kwa vitendo kupitia sekta zinazozalisha ajira kwa wingi kama vile sekta ya kilimo kupitia programu ya Jenga Kesho iliyobora (BBT), ujasiriamali, na madini kupitia Programu ya Mining...

Mkandarasi Anayejenga Barabara Za Tactic Morogoro Atakiwa Kukamilisha Kazi Ndani Ya Miezi Mitatu

Morogoro Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila amemtaka Mkandarasi M/s Jiangxi GEO Engineering Group anayejenga barabara ya Kihonda - VETA yenye urefu wa Km 12.85 kwa kiwango cha lami Manispaa ya Morogoro mkoani Morogoro kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa ubora unaotakiwa ndani ya miezi mitatu hadi kufikia mwezi Mei 2025. Mhandisi Mativila ametoa agizo hilo kwa mkandarasi pamoja na Mhandisi Mshauri wa mradi huo katika ziara ya ukaguzi wa mradi huo unaotekelezwa kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Miji Tanzania (TACTIC) chini ya mkopo nafuu toka Benki ya Dunia.  “Nimekuja kutembelea moja ya miradi mikubwa ambayo serikali ya awamu ya sita inatekeleza kwa ajili ya kuleta maendeleo na ushindani katika miji 45 ya Tanzania iliyochanguliwa iwe na ushindani wa kuwa na miundombinu bora ikiwemo ya barabara kwa kiwango cha lami inayowezesha kukua kwa uchumi’’, al...

Makamu Mwenyekiti Ccm Bara Amjulia Hali Mnec Gachuma- Bugando Medical Center

 Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Mzee Stephen Masato Wasira amefika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando leo tarehe 10 Februari 2025 kwa ajili ya kumjulia hali Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayewakilisha Mkoa wa Mara Mzee Christopher Mwita Gachuma (MNEC).  Mzee Wasira amefika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kumjulia hali MNEC Gachuma aliyepata ajali jana tarehe 09 Februari 2025 baada ya gari yake kupinduka na kuacha njia jana katika Eneo la Rung'abure Wilayani Serengeti akiwa njiani kuelekea kwenye mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Stephen Wasira akitokea Wilayani Tarime kuelekea Serengeti.  Mzee Wasira amemuombea afya njema na uponyaji wa haraka MNEC GAachuma ili aweze kurejea kwenye majukumu yake ya kila siku ya ujenzi wa Taifa.

Wasira :Ccm Tutashika Dola Kwa Kura ,Si Bunduki

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Tanzania Bara Stephen Wasira amesema katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu Chama kitaendelea kushika dola kwa wingi wa kura na si mtutu wa bunduki. Pia, amesema CCM imebeba maono na fikra za ukombozi na kwamba itaendelea kuwa wakili wa kuwatetea Watanzania. Wasira aliyasema hayo leo Februari 10, 2025 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Jimbo la Busega mkoani Simiyu alipokuwa akielekea jijini Mwanza. “Katika uchaguzi mkuu mwaka huu CCM tutashinda maana hakuna wa kupambana na CCM. Mtaji wetu ni kushika dola na dola hatuishiki kwa bunduki bali tunaishika kwa kura na kura zinapigwa na wana CCM na wasio wana CCM,” alisema Wasira Akieleza zaidi kuhusu uimara wa CCM amesema unatokana na muungano wa vyama vilivyoleta ukombozi wa nchi ambavyo ni TANU na Afro-Shiraz Party (ASP). “Kwa hiyo wanachama na viongozi wa Chama tunabeba maono ya vyama vilivyopita na sisi ndio tunaendeleza kazi ya uhuru, kuleta mabadiliko katika maisha ya watu," alisema. Kuh...

Balozi Nchimbi Achangisha Sh. 1.7b Ujenzi Ofisi Ya Ccm Mkoa Wa Singida

Matukio mbalimbali katika picha wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoenda sambamba na harambee ya uchangishaji wa fedha na vitu vingine, kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi. Jumla ya kiasi cha fedha takriban shilingi bilioni 1.7 zilipatikana.  Hafla hiyo iliyowahusisha viongozi, wanachama, wafuasi wa CCM na wananchi wa kada mbalimbali, ilifanyika Ukumbi wa Jenerali Venance Mabeyo, jijini Dodoma, tarehe 9 Februari 2025.