Skip to main content

Posts

Showing posts from October 10, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Bilionea Aidan Kuifufua Sunshine, Kiwanda Kikubwa Cha Kuchenjua Dhahabu Chunya

*Kitakuwa na uwezo wa kuchenjua tani 500 kwa Saa 24* *Kuzalisha Ajira 350 kwa Watanzania* *Ukarabati kuchukua  Miezi Miwili*  *Chunya* Septemba 2024, jina la Bilionea Aidan Andrea Msigwa lilitikisa Sekta ya Madini kama radi katikati ya jua kali kwa kuuza kilo 111.82 za dhahabu. Alivuna zaidi ya shilingi bilioni 20.11 kwa mkupuo mmoja hatua iliyotikisa si tu wadau wa madini, bali iliwaamsha Watanzania wengi hadi kuvuka mipaka ya nchi. Aidan hakutajwa tu kama gwiji wa madini, bali aliwekwa rasmi kwenye meza ya mabadiliko ya kiuchumi ndani na nje ya Tanzania. Baada ya kuvuna mabilioni kutokana na kuuza dhahabu hiyo Aidan hakukimbilia anasa bali alichagua kuwekeza kwa watu baada ya kutumia kiasi kikubwa cha fedha kuinunua Kampuni ya SUNSHINE Group iliyoko Matundasi Chunya iliyokuwa ikimilikiwa na wawekezaji kutoka China. Kwa sasa yupo mbioni kwa kushirikiana na wawekezaji wengine wa China kukifufua kiwanda hicho kikubwa cha kuchenjua dhahabu kilichokuwa kimesimamisha shughuli zake...

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Awajibu Wanaomzushia Kifo

RAIS Mstaafu Dk.Jakaya Kikwete ameamua kuwatolea uvivu wale ambao wamekuwa wakimzushia kifo ambapo amesema yeye ni mzima wa afya hana mafua wala kichomi na kusisitiza wanaomuombea mabaya watatangulia wao na atahudhuria mazishi yao. Mzee Kikwete ambaye ni Rais Mstaafu was Serikali ya Awamu ya Nne ameyasema hayo leo Oktoba 10,2025 alipokuwa akiwasalimia  wakazi wa Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, katika Mkutano wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) ulioongozwa na Mgombea Mwenza wa Urais kupitia CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi. “Wale  wanaonizushia  kifo kupitia mitandao ya kijamii niwaambie niko salama, afya yangu  ni nzuri,sina  mafua wala kichomi,wanaomwombea mabaya watatangulia wao na mimi nitahudhuria mazishi yao.” Kikwete ametoa kauli hiyo baada ya kueleza sababu zinazowafanya wananchi kukiamini  Chama Cha Mapinduzi kutokana na mikakati na uwezo wa chama hicho katika kupangilia mambo.  Amesema uwezo huo ndio unasababisha CCM kuendelea kuongoza Serika...

Serikali Imetoa Trilioni 3.5 Kuwawezesha Vijana-Majaliwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imefanikiwa kutoa kiasi cha shilingi trilioni 3.5 kufikia mwaka 2024 kwa ajili ya uwezeshaji wa vijana kiuchumi kutoka shilingi bilioni 904 mwaka 2021. Amesema kuwa fedha hizo zimewasaidia vijana kupata mitaji *ambayo ambayo* imewawezesha kushiriki katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali na hatimaye kuinua vipato vyao pamoja na uchumi wa Taifa. Amesema hayo leo Ijumaa (Oktoba 10, 2025) Wakati *wa* maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa iliyofanyika mkoani Mbeya. Kaulimbiu ya Maadhimisho hayo ni Nguvu Kazi ya Vijana kwa Maendeleo Endelevu.” Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali imefanya hivyo kwa kutambua kuwa Vijana ni nguvu kazi  na ndiyo msingi wa safari ya maendeleo ya Taifa letu. “Vijana wakipewa nafasi na kuandaliwa ipasavyo, wanaweza kuwa nguzo kuu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, na kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs)”. Mheshimiwa Majaliwa ameongeza kuwa vijana wameku...

Dkt Nchimbi Amuombea Kura za Ushindi wa Kishindo Dkt.Samia Kibaha Vijijini

Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwahutubia Wananchi waliofika kumsikiliza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa mpira wa Mama Salmini, Mlandizi ndani ya jimbo la Kibaha Vijijini leo Ijumaa Oktoba 10, 2025 mkoani Pwani. Katika mkutano huo, Dkt.Nchimbi pamoja na kunadi Sera na Ilani ya CCM ya 2025-2030,pia alimuombea kura za ushindi wa kishindo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani. Pamoja na mambo mengine,Dkt Nchimbi pia alitumia nafasi hiyo  kuwanadi wagombea Ubunge wa mkoa huo akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Kibaha Mjini Ndugu Silyvestry Francis KOKA, mgombea Ubunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Ndugu Hamoud Abuu JUMAA pamoja na Madiwani.

Oktoba 29 ni Samia Day, tujitokeze kwa wingi kurundika kura kwa CCM

Na: Dkt. Reubeni Lumbagala, Tanga Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Uchaguzi Mkuu hufanyika kila baada ya miaka mitano. Kwa kuwa Uchaguzi Mkuu wa mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2020, basi mwaka huu wa 2025, tunafanya Uchaguzi Mkuu. Uchaguzi Mkuu ni fursa adhimu ambapo wananchi wanapata nafasi ya kuchagua viongozi watakaowaongoza katika kipindi cha miaka mitano ijayo yaani 2025-2030. Kutokana na upekee wa tukio hili, kwa sasa siku ya Uchaguzi Mkuu ni siku ya mapumziko ya kitaifa ambapo wananchi wanapata fursa ya kwenda katika vituo walivyojiandikisha ili kupiga kura kwa uhuru ili kuchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani. Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kujinadi katika mikoa mbalimbali hapa nchini kuomba ridhaa ya kuongoza wananchi. Aidha, katika mikutano hiyo, Dkt. Samia anawaombea kura pia wagombea Ubunge na Udiwani watokanao na CCM ili kukamilish...