Skip to main content

Posts

Showing posts from June 7, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Bilioni 916.7 zipo tayari, wenye sifa ombeni mikopo ya elimu

Na: Dk. Reubeni Lumbagala, Tanga Elimu ni gharama. Wahenga wakaweka wazi ukweli huu kwa kusema "Ikiwa unaona elimu ni ghali, basi jaribu ujinga." Ni ukweli ulio dhahiri kuwa gharama za kupata elimu ziko juu, ndiyo maana serikali ikachukua jukumu la kuja na kutekeleza kwa vitendo Sera ya Elimumsingi Bila Ada kuanzia Elimu ya Awali hadi Kidato cha Sita. Hili limefanyika kwa lengo la kuwapunguzia wazazi na walezi mzigo mkubwa wa gharama za kugharamia elimu za watoto na ndugu zao. Serikali sasa inatoa Ruzuku ya Uendeshaji (Capitation Grants) kwa shule zake zote za msingi na sekondari ili kufanikisha shughuli za taaluma, utawala, mitihani, michezo, ukarabati na shughuli nyinginezo ndogondogo katika ngazi ya shule. Kwa upande wa elimu ya kati na ya juu, serikali inatoa mikopo kwa wanafunzi kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa  Elimu ya Juu (HESLB) ili waweze kumudu gharama za elimu na hatimaye waweze kutimiza ndoto zao za kupata elimu ya juu na hatimaye waweze kujiajiri au kuajir...

Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango Kushiriki Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Bahari

Na Ada Ouko, GMTV. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango, leo tarehe 07 Juni 2025 ameondoka nchini kuelekea Ufaransa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari (UNOC3), utakaofanyika Jijini Nice, kuanzia tarehe 09 hadi 13 Juni, 2025. UNOC3 ni jukwaa muhimu la kimataifa la kuhamasisha utekelezaji wa Lengo la Maendeleo Endelevu namba 14 (SDG 14) linalolenga kuhifadhi na kutumia kwa uendelevu rasilimali za bahari, bahari kuu na mazingira ya pwani. Mkutano huo unawakutanisha Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, Mashirika ya Kimataifa, Asasi za Kiraia pamoja na Sekta binafsi. Aidha, Makamu wa Rais anatarajiwa kushiriki katika Mikutano ya Uwili yenye lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania, Mashirika na Mataifa yanayoshiriki Mkutano huo. Mkutano huo utasaidia kuimarisha nafasi ya Tanzania kimataifa, kujenga mpya na...

Rufiji Wamwombea Rais Samia, Sikukuu ya Eid Al Adha

 Na Mwandishi Wetu - Rufiji  Waumini wa dini ya kiislam wilayani Rufiji wamefanya dua maalum ya kumwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na  amani ya Tanzania kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa wananchi kwa ujumla. Mwenyekiti wa Baraza la waislam Tanzania Wilaya ya Rufiji Shehe Ally Mbwana  amesema katika kuadhimisha sikukuu ya Idd leo Juni, 7, 2025 waislam wa Rufiji wameamua kumwombea Mhe.Rais Samia na Tanzania ili nchi iwe na amani na kuwa na mafanikio. "Ndugu zangu leo tunakwenda kuliombea taifa letu liendelee kuwa na amani pia kumwombea Mhe. Rais wetu ili Mwenyezi Mungu amwezeshe aendelee kuliongoza vema taifa letu." Amesema Shehe Mbwana. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye pia ameshiriki kwenye dua hiyo amefafanua kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na amani hivyo ni muhimu kuilinda amani hiyo kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye  " Watanzania wenzangu,wa dini zote ni muhimu tukatambua...

Serikali inatambua Mchango wa Viongozi wa Dini - Majaliwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita inawaamini na inathamini mchango wa viongozi wa dini wa madhehebu yote. Amesema serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano kati yake na viongozi hao ili kujenga amani, mshikamano na ustawi wa jamii ya watanzania. "Tunaamini mtaendeleza jukumu la kuwasihi watanzania waone umuhimu wa kila mmoja kuwa sehemu ya mchango wa kulifanya taifa hili kuwa tulivu na kuimarisha mshikamano miongoni mwetu." Ameyasema hayo leo (Jumamosi  Juni 7, 2025) alipokuwa mgeni rasmi katika Sala na Baraza la Eid Al Adha iliyofanyika katika Msikiti wa Mohamed VI Kinondoni, Dar es Salaam. Amesema viongozi wa dini wanayo nafasi kubwa ya kuwajenga waumini wao kuwa na staha, ustaarabu, uvumilivu na kutambua kuwa wao ni miongoni mwa wanajamii na kushiriki katika shughuli za kimaendeleo. "Kwa upande wa serikali tunaendelea kujenga misingi ya mshikamano kati ya waumini wa dhehebu moja na dhehebu jingine, tukiwa tunaamini kuwa dini zimeendelea ku...