Na Dawati la Habari Polisi Mwanza Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na wadau wa uvuvi limefanikiwa kudhibiti uhalifu ukiwemo uharamia uliokuwa ukitendaka ndani ya ziwa viktoria kwa kufanya doria, misako na operesheni mbalimbali zilizofanikisha kukamata watuhumiwa , mali za wizi pamoja na zana haramu za uvuvi. Mafanikio hayo yamebainishwa Oktoba 25, 2024 wilayani Busega mkoani Simiyu wakati wa kikao kazi cha Saba cha Makamanda wa Polisi mikoa ya kanda ya ziwa na wadau wa uvuvi kutoka mikoa ya Mwanza, Geita, Simiyu, Tarime Rorya, Kagera na Mara kwa lengo la kujadili usalama ndani ya ziwa viktoria. Akitoa taarifa ya Utekelezaji wa mikakati na maazimio ya kikao kilichopita, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Wilbrod Mutafugwa amesema zaidi ya watuhumiwa 10,000 pamoja na zana haramu za uvuvi zikiwemo zaidi ya nyavu haramu 10,000 zilizokuwa zikitumika kuharibu mazao ya uvuvi zimekamatwa katika kipindi cha miezi sita iliyopita. Kwa upande wake,Mku...
Marato tv - Sauti ya Jamii