Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 21, 2024 amewasili mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa tenki la kuhifadhi maji la Kisesa, mkoani Mwanza ikiwa ni Mpango wa muda wa kati wa kuboresha huduma ya maji Mwanza ambao unatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 3.54. Mradi huo ambao unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (France Development Agency) hadi kukamilika kwake na mpaka sasa umefikia asilimia 93 na unatarajiwa kuhudumia wananchi 75,000 wa maeneo ya Kisesa Bujora, Igudija na swhemu za jirani. Akizungumza na wananchi wa eneo la Kisesa baada ya kukagua mradi huo Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa ya utekelezaji wa miradi mikubwa inayowagusa wananchi moja kwa moja kwenye sekta za elimu, afya, maji, kilimo, uvuvi na barabara. Kwa Upande wake, Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema wizara hiyo itaendelea kusimamia maagizo ya Rais ...
Marato tv - Sauti ya Jamii