■ Waziri Mavunde aeleza fursa zilizopo kwenye utafiti, ■ Balozi Burns abainisha utayari wa Makampuni ya Canada kuwekeza nchini Tanzania, ▪️Canada yaonesha utayari wa kusaidia teknolojia kwa wachimbaji wadogo ■ *Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais yaweka Mazingira wezeshi kwa wawekezaji nchini. *Dodoma* Waziri wa Madini, *Mheshimiwa Anthony Mavunde (Mb)* amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Canada nchini Tanzania, *Mheshimiwa Emily Burns* katika ofisi ndogo za Wizara zilizopo katika jengo la Tume ya Madini, Kilimani Jijini Dodoma. Katika mazungumzo hayo, Waziri Mavunde alibainisha kuwa moja ya kipaumbele kikuu cha sekta ya madini ni utafiti ambao utapelekea kutambua aina na kiwango cha rasilimali madini tulizobarikiwa nchini kwetu na kuvutia uwekezaji. "Tunafamu kuwa Nchi yetu tumeweza kufanya utafiti wa kina wa kurusha ndege kwa asilimia 16 tu. Hivyo, tuna uhitaji mkubwa wa kupata uwekezaji zaidi katika eneo hili ili kuongeza mchango wa sekta ya madini kweny...
Marato tv - Sauti ya Jamii