Skip to main content

Posts

Showing posts from April 1, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Afungwa miaka 30 kwa kusafirisha mihadarati*

Mkinga MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi  Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Mwaki Mwakanjila Mwaki, baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi, ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya biashara haramu ya mihadarati mkoani hapa. Hukumu hiyo imetolewa Machi 31, 2026, na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mkinga, Mheshimiwa Aziz Hamis Mzee, katika shauri la jinai namba CC 03556/2026.  Hakimu Mzee amesema Mahakama imeridhika pasipo shaka na ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka, uliothibitisha kuwa mshtakiwa alijihusisha na usafirishaji wa dawa hizo kinyume cha sheria. Mapema, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Kelvin Kisanga, aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaojihusisha na biashara hiyo haramu ambayo inahatarisha nguvu kazi ya Taifa na usalama wa jamii. Kisanga alisisitiza kuwa Serikali haitasita kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote wanaojaribu kutumia mko...

Nchimbi Akisalimiana Na Baba Mtakatifu Baada ya Ibada ya Hija Vatican

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, akisalimiana na Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Leo XIV, mara baada ya Ibada ya Hija iliyofanyika katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro – Vatican, leo tarehe 01 April 2026

Ufunguzi wa Kanisa na Harambee ya Ujenzi wa Shule na Zahanati Kijiji Cha Musati Serengeti Sasa ni Aprili 18

  TAASISI ya Nyansaho Foundation imendaa harambee kubwa kwa ajili ya kutafuta fedha za ujenzi wa Zahanati na Shule ya msingi ya kisasa katika kijiji cha Musati wilayani Serengeti mkoani Mara.  Jaji Mkuu wa Tanzania mh George Masaju anatarajia kuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo inayotarajiwa kufanyika Aprili 18 mwaka huu wa 2026, sambamba na ufunguzi wa kanisa la Waadventista Wasabato Musati Central.  Imeelezwa kuwa mwenyeji wa harambee hiyo anatarajiwa kuwa mwenyekiti wa taasisi ya Nyansaho foundation ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa mhe.Rhimo Nyansaho huku waziri wa ujenzi mhe. Abdallah Ulega akitarajia kuwa mgeni maalum.  Awali ufunguzi wa kanisa Hilo jipya na harambee hiyo ulipangwa kufanyika machi 28 mwaka huu lakini ukiahirishwa baada ya kutokea kifo cha waziri William Lukuvi. 

Shilingi Trilioni 1.77 Zahitajika Kukidhi Miundombinu ya Elimu Mwaka 2028

JUMLA ya sh. trilioni 1.77 zinahitajika kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, maabara, ajira mpya za walimu, ruzuku ya mitihani, ya vitabu na uendeshaji kwa wanafunzi zaidi ya milioni tatu wanaotarajiwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2028. Hayo yamesemwa Bungeni, jijini Dodoma leo (Jumatano, Aprili mosi, 2026) na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba wakati akiwasilisha Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa Mwaka 2026/2027. “Tathmini inaonesha kuwa wanafunzi 3,021,177 wanatarajiwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2028. Jumla ya gharama zinazohitajika ni shilingi trilioni 1.77 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 23,226; matundu ya vyoo 46,632; maabara 9,366; ajira mpya za walimu 40,192; ruzuku ya vitabu na uendeshaji pamoja na ruzuku ya mitihani na upimaji,” amesema. Amesema mahitaji hayo yanatokana na uamuzi wa Serikali kuimarisha sekta ya elimu kwa kuzingatia Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2...

Rais Samia Akutana Na Waliokuwa Wagombea Urais wa Vyama Vya Upinzani

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Wagombea wa Nafasi ya Urais na Wagombea Wenza kutoka vyama vya Siasa 16 vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba, 2025. Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 31 Machi, 2026. #KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #maendeleoendelevu  #diplomasiayakiuchumi

Zuhura Yunus Leads Tanzanian Delegation to Visit Permanent Mission in Geneva

By Prosper Makene  The Tanzanian delegation participating in the 356th session of the International Labour Organization (ILO) Governing Body has today visited the Permanent Mission of Tanzania in Geneva.  Led by Deputy Permanent Secretary, Office of the Prime Minister - Labour, Employment and Relations, Zuhura Yunus, the delegation met with officials at the mission. The visit aimed to strengthen cooperation and discuss key labour and employment issues on the agenda of the ILO session.  Yunus was accompanied by Judge Yose Mlyambina of the High Court (Labour Division). The Tanzanian delegation is representing East African countries at the ILO session, focusing on promoting cooperation in labour and employment. Their participation includes delivering statements on key issues, showcasing Tanzania's commitment to international labour standards. The delegation includes representatives from institutions under the Office of the Prime Minister, such as PSSSF, NSSF, OSHA, WCF, and ...

Utekelezaji wa Dira 2050 Uanze - Dkt. Mwigulu

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba ameagiza kuanza utekelezaji wa Dira 2050 kupitia Mpango na Bajeti iliyoandaliwa na kuendelea kuishirikisha sekta binafsi na wadau wa maendeleo katika kuharakisha utekelezaji wake ili kujenga uchumi jumuishi, shindani na unaotegemea uzalishaji wenye tija. Aidha, Waziri Mkuu ameilekeza Tume ya Mipango kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu Dira 2050 ili kuwezesha kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wake kwa sababu suala hilo litawezekana ikiwa wadau wote watakuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu vipaumbele vilivyoainishwa katika Dira 2050. Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumatano, Aprili 1, 2026) wakati akiwasilisha hotuba yake kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa Mwaka 2026/2027 Bungeni jijini Dodoma. Amesema Dira 2050 iliyozinduliwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mnamo tarehe 17 Julai, 2025, itaongoza mipango ya maendeleo katika miaka 25 ...