Skip to main content

Posts

Showing posts from August 22, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Atembelea Mradi wa Gesi Madimba

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari akiongozana na  baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ametembelea  Kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Madimba na Vitalu vya gesi asilia vilivyoko Msimbati Mkoani Mtwara,  tarehe 21 Agosti, 2025. Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema kuwa ziara hiyo itawaongezea maarifa Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Upekuzi wa Mikataba na utoaji wa Ushauri kwenye Miradi mikubwa ukiwemo mradi huo mkubwa wa gesi na mafuta.  *"Tunapoona mradi huu maana yake ni kwamba kuna mikataba ilitangulia mwanzo mikataba ambayo iliandikwa na kupekuliwa vizuri na vihatarishi vyote vikawekwa vizuri na maslahi ya Taifa yakazingatiwa vizuri."* Alisema Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema kuwa ziara hiyo ni sehemu ya mafunzo kwa Wataalamu wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, mafunzo ambayo yatawasaidia kuwaongezea uwezo katika masuala ya kiufundi kuhusiana n...

Sagini Aendelea Kuboresha Miundombinu Shule ya Awali na Msingi Mwalimu Nyerere

Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini ameendelea kuboresha miundombinu ya Shule ya Awali na Msingi Mwalimu Nyerere iliyopo Kijiji cha Butiama ili kuepukana na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo watumishi na wanafunzi ikiwemo wizi wa vifaa vya kujifunzia. Akizungumza katika Mahafali ya Tano ya Darasa la Saba yaliyofanyika Agosti 22, mwaka huu Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini, Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Emmanuel Mayeji aliyemwakilisha Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini amesema kuwa Mhe Sagini alianza kutatua kero hiyo mapema na sasa ni zoezi la ukamilishaji wa ujenzi wa uzio wa shule. "Mhe. Sagini amewaahidi kwamba atakuwa nanyi bega kwa bega katika kukuza elimu wilayani  Butiama kwani ni maelekezo ya Chama cha Mapinduzi kupitia Ilani ya Uchaguzi wa mwaka 2020 – 2025 iliyolenga kuimarisha ubora wa elimu katika ngazi zote kwa kuzingatia falsafa ya kujitegemea yenye kuendana na mazingira ya nchi yetu," amesema May...

Dkt. Biteko Ataka Watumishi Wizara ya Nishati na Taasisi Zake Kuwa Mfano wa Matumizi Nishati Safi ya Kupikia

📌 Lengo ni kutekeleza Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia kwa vitendo 📌Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia yapaa kutoka asilimia 6 hadi 20.3 📌 Agawa majiko yanayotumia umeme kidogo kwa Watumishi wa Wizara ya Nishati na REA 📌 Apongeza REA  kuhamasisha Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia nchini Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, amewataka watumishi katika Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini ya wizara hiyo kuwa mfano katika matumizi ya  Nishati Safi ya kupikia ili kuitekeleza kwa vitendo ajenda iliyoasisiswa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan  inayolenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi na salama kwa afya. Dkt. Biteko ametoa maelekezo hayo tarehe 22 Agosti 2025 jijini Dodoma wakati akigawa majiko yanayotumia umeme kidogo kwa watumishi wa Wizara ya Nishati na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambapo amewataka Watumishi hao  wawe mabalozi katika  kutekeleza ajenda ya Nishati Safi ...

Balozi Dkt Nchimbi Ateta na Watendaji wa Uwt Wilaya na Mikoa

  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akizungumza na Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa na Wilaya wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT) wanaoudhuria mafunzo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, yaliyofanyika leo Ijumaa tarehe 22 Oktoba 2025, katika Ukumbi wa Kilimani Landmark, jijini Dodoma.

Balozi wa Tanzania Nchini Sweden Mhe. Mobhare Matinyi Afanya Mazungumzo na Waziri Wa Mambo ya Nje wa Sweden Jijini Stockholm

  Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Balozi Mobhare Matinyi, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden, Mhe. Maria Malmer Stenergard, katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje jijini Stockholm, leo tarehe 22 Agosti, 2025. Katika mazungumzo hayo, Mhe. Balozi Matinyi aliwasilisha salamu kwa wananchi na Serikali ya Ufalme wa Sweden kutoka kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye ni Mwanadiploamsia namba 1 nchini, na kusisitiza dhamira ya Tanzania kuendeleza uhusiano wa muda mrefu wa kidiplomasia na ushirikiano wa kiuchumi na Sweden. Vilevile, Balozi Matinyi alieleza juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuimarisha ustawi wa uchumi kupitia ushirikiano na Sweden, hususan katika sekta za nishati, elimu, afya, utafiti, mazingira, uzalishaji viwandani, na miradi ya miundombinu kama vile Reli ya Kisasa (SGR).  Katika mzungumzo hayo, Mhe. Balozi Matinyi alibainisha kuwa hadi sasa, jumla ya kampuni 101 kutoka Swed...

Tuwawezeshe Wafanyakazi Kukabiliana na Mabadiliko ya Teknolojia- Majaliwa

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa vyama vya wafanyakazi barani afrika kuweka mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia duniani. Amesema kwa kufanya hivyo kutawawezesha kupunguza hatari ya kupoteza ajira kutokana na ujio wa mashine pamoja na matumizi ya teknolojia mpya ikiwemo za akili mnemba. Ameyasema hayo leo (Ijumaa 22 Agosti 2025,) Alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Afrika (OAUUT) uliofanyika Hoteli ya Johari Rotana Dar es Salaam. Amesema kuwa, katika dunia ya sasa, imeshuhudiwa uwepo wa mabadiliko makubwa yanayochagizwa na mapinduzi ya kiteknolojia ikiwemo matumizi ya akili mnemba pamoja na utandawazi. “Kuna hatari ya watu kupoteza ajira zao kadri mitambo na mifumo ya kisasa inavyochukua kazi ambazo kwa kawaida zingeweza kufanywa na wafanyakazi. Tunapaswa kuweka mpango wa kutoa mafunzo endelevu yanayoendana na mabadiliko ya teknolojia ili kuwandaa wafanyakazi na aina mpya za ajira zinaz...