Skip to main content

Posts

Showing posts from November 30, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kampuni ya The Wheel Imefungua Kituo Kinachotumia Teknolojia ya Akili Bandia Kutengeneza Magari Dodoma

  Na Mwandishi Wetu-Dodoma SEKTA ya matengenezo ya magari inakaribia kushuhudia mapinduzi makubwa baada ya kampuni ya THE WHEEL kuzindua teknolojia mpya ya kisasa inayolenga kuboresha utendaji wa mafundi na kuongeza ufanisi wa kazi zao.  Teknolojia hiyo, inayotumia akili bandia (AI) na mifumo ya uchambuzi wa data, inatarajiwa kubadilisha jinsi matatizo ya magari yanavyogunduliwa na kutatuliwa, hivyo kuokoa muda na kuongeza usalama kazini. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi msemaji wa kampuni ya The Wheel Amesema wamefungua kituo Cha utoaji huduma za urekebishaji wa haraka na utunzaji wa magari jijini Dodoma na wamefurahi kupanua  huduma hadi Dodoma ambapo lengo ni kuboresha uzoefu wa Uendeshaji Kwa wateja wao huku kituo hicho Ikiwa ni kituo cha saba Cha kutoa huduma nchini Tanzania. Chris Mendoza, ameeleza kuwa teknolojia hii itawapa mafundi uwezo wa kugundua hitilafu kwa haraka zaidi, kupunguza muda wa matengenezo, na kuhakikisha magari yanarejeshwa kwa wateja katika h...

Waziri Mkuu Kushiriki Siku ya Ukimwi Duniani Kitaifa Mkoani Ruvuma

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Novemba 30, 2024 amewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea ambapo kesho Disemba 01, 2024 atashiriki katika Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya UKIMWI Duniani. Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa ni Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango.

Ruto achaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Rais wa Kenya William Ruto amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), akichukua nafasi ya mwenzake wa Sudan Kusini Salva Kiir. Ruto atashikilia wadhifa huo kwa mwaka mmoja ujao. Aliteuliwa kushika wadhifa huo wakati wa mkutano wa 24 wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Arusha, Tanzania. Mkutano wa 24 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unawaleta pamoja viongozi wa kanda hiyo ili kujadili masuala muhimu yanayochagiza mustakabali wa Afrika Mashariki. Mkutano huo wa hadhi ya juu, uliofanyika chini ya kaulimbiu kuu ya Maadhimisho ya Miaka 25 ya EAC, unatumika kama jukwaa la kutathmini mafanikio ya miaka 25 iliyopita huku ukielekeza njia ya kusonga mbele kwa utangamano wa kina.

Dkt Biteko amewahimiza kuongeza utu,umakini kazini,kukuza ubunifi,ufanisi na tija

*📌 Naibu waziri mkuu amwakilisha Dkt. Mpango Tuzo za Mwajiri Bora mwaka 2024* *📌 TBL, BARIC GOLD, TPA Zang’ara Ushindi wa jumla Mwajiri Bora 2024* *📌 ILO yashauri Utambuzi wa Sekta isiyo rasmi* *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza waajiri nchini kuongeza umakini na kuzingatia misingi ya utu mahali pa kazi ili iwe motisha na chachu kwa watumishi kuongeza ubunifu na ufanisi kazini. Dkt. Biteko amesema hayo wakati akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Phillip Mpango katika usiku wa Tuzo kwa mwajiri Bora wa mwaka 2024 ambapo Kampuni ya bia nchini (TBL) imeibuka mshindi wa jumla ikifuatiwa Kampuni ya Barick Gold huku Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA ikishika nafasi ya tatu.  Amewapongeza waandaaji wa tuzo hizo na kuwataka kupanua wigo wa makundi ya ushiriki huku akisisitiza umuhimu wa utoaji wa motisha mahala pa kazi ili watumishi waongeze ari ya kufanya kazi ...

Mkutanowa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Waendelea Jijini Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akiwasili eneo la Ukumbi wa Mikutano AICC Mkoani Arusha kushiriki Mkutano wa 24 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC leo November 30,2024. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na baadhi ya Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kabla ya kuanza kwa Mkutano wa kawaida wa 24 wa viongozi hao pamoja na maadhimisho ya miaka 25 ya Jumuiya hiyo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Jijini Arusha tarehe 30 Novemba, 2024.

Waziri Kikwete ateta na Viongozi wa Vijiji Chalinze

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu mh Ridhwani Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na viongozi wa Serikali za mitaa walichaguliwa Nov 27 mwaka huu 2024 na kuwapa pongezi kwa kuchaguliwa huku akiwakumbusha wajibu wao kwa chama na Serikali katika kuwatumikia wananchi katika maeneo yao. Mh Kikwete amepata nafasi hiyo ya kutoa nasaha katika mkutano na Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na wajumbe wa Halmashauri za Vijiji katika makundi yote wapatao 1919 uliofanyika Lugoba, Chalinze mapema leo tarehe 30Nov.2024. Ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wajibu wao kwa Wananchi, Serikali zao na kwa Chama Chao. Pia nimewatakia kheri katika majukumu yao kwa jumla na kuwaahidi ushirikiano mkubwa sana toka kwangu na ofisi yangu.