Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amesema suala la usalama wa kimtandao ni muhimu ili kuhakikisha upatikanaji wa taarifa, huduma na bidhaa za mtandaoni ni salama na hazimuathiri mwananchi na Taifa kwa ujumla. Akizungumza wakati wa ziara yake makao makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) tarehe 18 Julai, 2024 Mhandisi Mahundi ameishukuru timu zima ya TCRA kwa umahiri mkubwa katika usimamizi wa sekta hasa katika eneo la usalama mtandao. Amesema, umahiri wa TCRA kunaifanya Wizara kuonekana inawajibika na kuendelea kulipa Taifa heshima huko duniani ambapo mpaka sasa tupo katika nafasi nzuri kimataifa katika masuala ya usalama mtandao. Aidha, ametoa rai kwa TCRA kuendelea kukimbizana na mabadiliko ya teknolojia kwa wataalam kujifunza na kuongeza ujuzi mara kwa mara ili kuweza kukabiliana na wahalifu wa mtandaoni wanaoenda sambamba na kasi ya ukuaji wa teknolojia kwa kubuni mbinu mpya za kufanya uhalifu. Mhandisi Mahund...
Marato tv - Sauti ya Jamii