Na Mwandishi Wetu CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE),kimesema kimeendelea kufanya vizuri kitaaluma ambapo utafiti uliofanyika mwaka jana ulikiweka kwenye nafsi ya nane kati ya vyuo 47 vya elimu ya juu. Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Edda Lwoga, wakati wa kongamano la kitaaluma lililofanyika chuoni hapo. Alisema chuo hicho kikongwe kimetimiza miaka 60 ya kubobea kwenye kufundisha biashara, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano TEHAMA na kwa muda wote wa uhai wake kimemudu kuzalisha idadi kubwa ya wataalamu wa kada mbalimbali. Alisema kwa sasa chuo hicho kina kampasi nne za Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Mbeya na mwakani kinatarajia kujenga kampasi yake nyingine mkoani Kilimanjaro kutimiza ahadi iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa kampeni zake. Alisema katika kudhihirisha ubora wake utafiti uliofanyika mwaka jana ulionyesha chuo hicho kushika nafasi ya nane kati ya vyuo 47 vya elimu ya juu nchini na kwamba mafanikio hayo yamewezes...
Marato tv - Sauti ya Jamii