Taasisi ya Mwanamke na Nguvu ya kijani TANZANIA imewaasa wanawake na vijana kuwa makini katika kulinda amani huku ikiwataka kuwa mabalozi wa amani ili kusaidia kujenga kizazi chenye utu na heshima katika jamii . Hayo yamebainishwa mapema Oktoba 26 mwaka huu 2025, na Mwenyekiti wa Taasisi ya mwanamke na nguvu ya kijani ambaye pia ni Mwenyekiti wa makampuni ya PMM Group Dkt Judith Mhina Spendi katika kongamano la amani la kitaifa lililoandaliwa na taasisi hiyo lenye lengo la kutoa elimu kwa Watanzania kuhusu amani na umuhimu wake katika jamii. Amesema kuwa Tanzania imejijengea sifa ya kuwa nchi ya amani, utulivu na mshikamano kupitia juhudi mbalimbali zinazoendelea kufanywa na Serikari ikishirikiana na wadau nchini katika kuimarisha hali ya amani. Hata hivyo Dkt Judith Mhina amewataka watanzania kutotamani nafasi zisizozao katika jamii kwani kufanyq hivyo ni mojo ya sababu ya kuchochea uvunjifu wa amani katika jamii ya watanzania hasa katika kuelekea siku ya uchaguzi oktoba 29. Ai...
Marato tv - Sauti ya Jamii