Mataifa 132 Duniani ikiwemo Kenya na Tanzania ambayo yalikuwa yakinufaika moja kwa moja na ufadhili kutoka kwa Shirika la Ustawi wa Kimataifa la Marekani (USAID), ziko hatarini kupoteza jumla ya watu 14 milioni kufikia mwaka 2030 baada ya kufungwa rasmi kwa shirika hilo la kutoa misaada. Utafiti mpya uliochapishwa katika jarida la sayansi la Lancet unaeleza kwa kina jinsi hatua zilizopigwa katika miongo miwili iliyopita kupunguza vifo vya watoto na watu wazima, zitaporomoka. “Makadirio yetu yanaonyesha kuwa, isipokuwa hatua za kupunguza ufadhili zilizotangazwa na kutekelezwa katika nusu ya kwanza ya mwaka 2025 ziondolewe, idadi kubwa ya vifo vinavyoweza kuepukika vinaweza kutokea kufikia mwaka 2030,” walisema watafiti. Tofauti na tafiti za awali ambazo zilijikita tu kwenye athari za moja kwa moja za kiafya, utafiti huu mpya umeangazia pia athari mbadala ambazo pia zinaweza kusababisha vifo na kupoteza njia za kujikimu, na kueleza kuwa pia zinaathiri afya ya watu. Mipango isiyo ya ...
Marato tv - Sauti ya Jamii