Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi akiambatana na Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Mara ametembelea eneo lenye mgogoro wa ardhi katika mpaka wa Kata ya Mwema na Regicheri, Wilaya ya Tarime na kuwataka wananchi kujifunza kutatua changamoto zao kwa amani. “Sio kila changamoto inahitaji utatuzi wa kutumia nguvu na mapanga, changamoto nyingine zinazungumzika kwa amani na utulivu na inapatikana suluhu ya kudumu” amesema Mhe. Mtambi na kuongeza kuwa “hapa hamna mshindi wala bingwa katika mgogoro huu”. Mhe. Mtambi amewataka wananchi kuhakikisha kuwa mgogoro huu unatatuliwa kwa amani na utulivu na kuwahakikishia wakiendelea na mgogoro huo atatoa kipande kinachogombewa kwa uongozi wa JKT ili wenye mashamba katika eneo hilo wafanye kazi chini ya uongozi wa kijeshi. Mhe. Mtambi amemwagiza Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Mara kutambua mpaka wa Kata hizo na kuuangalia mpaka wa Inglam uliowekwa na Serikali ya Wakoloni sambamba na utambuzi wa wamiliki halali wa...
Marato tv - Sauti ya Jamii