Skip to main content

Posts

Showing posts from September 17, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Askari Kata ya Kamnyonge Boniphace Lazaro Asisitiza Nidhamu Mashindano ya Polisi Jamii Cup Musoma 2024

Na Shomari Binda-Musoma WACHEZAJI wanaoshiriki mashindano ya Polisi Jamii Cup Musoma 2024 wametakiwa kuzingatia nidhamu ili kulinda vipaji vyao. Ujumbe huo umetolewa Septemba 17 na askari Kata wa Kata ya Kamnyonge Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Boniphace Lazaro kwenye mchezo kati ya Lake Victoria na Kamnyonge. Amesema nidhamu ndio njia ya kuweza kufika kwenye mafanikio ya kimichezo kwa mchezaji yoyote.  Lazaro amesema mchezaji yoyote mwenye kipaji kisha akazingatia nidhamu ni rahisi kupata mafanikio na kufika mbali na Kila mchezaji kulinda usalama wa mchezaji mwenzake kutokuumizana. " Tuzingatie nidhamu tunapokuwa uwanjani ili kuvilinda vipaji vyenu na ndio njia itakayowawezesha kufika mbali. Kupitia mashindano haya pia tunapeana elimu ya kuzuia uhalifu kwa kutoa taarifa tufanye  hivyo kwenye Kata zetu kupitia polisi Kata",amesema. Katika mchezo huo uliofanyika uwanja wa Mara sekondari timu ya Lake Victoria imechomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kamnyonge fc. Mashindano hayo...

Dkt. Emmanuel Nchimbi Ashiriki Kikao Cha UVCCM Dodoma

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi leo ameshiriki kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) na mafunzo kwa Wajumbe wa Baraza Kuu. Kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Komredi Mohammed Ali Mohammed (Kawaida), kimefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), jijini Dodoma, leo Septemba 17, 2024.

Waziri Gwajima alia na mbinu mpya za ukeketaji

Wakati serikali na wadau mbalimbali wakipiga vita vitendo vya ukeketaji,baadhi ya wakazi wa wilaya Tarime mkoani mwanza wanadaiwa kubuni mbinu mpya kwa ajili ya kukwepa mkono wa dola. Miongoni mwa mbinu zilizobuniwa wilayani humo ni pamoja na kupunguza umri wa ukeketaji kufikia chini ya miaka mitano pamoja na kuwapeleka watoto kwenda kukeketwa nchi Jirani ya Kenya. Mbinu hizo zimebainika katika kijiji cha borega kata ya Ganyange wakati wa kampeni ya kuamsha ari ya kutokomeza vitendo vya ukeketaji,mimba na ndoa katika umri mdogo pamoja na ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Wakizungumza wakati wa kampeni hiyo,baadhi ya wakazi wa kijiji cha ganyange wameiomba serikali kuchukua hatua stahiki ili kukomesha vitendo vya ukeketaji. Msimu wa ukeketaji unatarajia kufanyika wilayani Tarime mwishoni mwa mwaka huu ambapo Jeshi la polisi Mkoa maalum wa kipolisi Tarime rorya limesema kuwa tayari kwa kushirikiana na wadau mbalimbali  limetoa elimu ya kutosha kwa Jamii kuhusu madhara ya ukatili u...

Mradi wa kimkakati wa ujenzi wa soko kuu la Mwanza wafikia asilimia 96

Ujenzi wa soko kuu la mwanza unaotekelezwa na serikali kwa gharama ya zaidi ya shilingi billioni 23 umefikia asilimia 96 Waziri wa fedha Dkt.Mwigulu Nchemba amekagua maendeleo ya ujenzi wa soko hilo la kimkakati na kueleza kuridhishwa kiwango cha ubora wa kazi.  Dkt.Nchemba amesema kuwa soko hilo ambalo ujenzi wake utakamilika hivi karibuni utaboresha mazingira ya biashara na kuchochea ukuaji wa uchumi.  Aidha amemtaka mkandarasi kampuni ya Mohamed builders kukamilisha ujenzi wa soko hili kwa wakati ili wananchi wa mwanza waweze kunufaika kiuchumi na uwepo wake. "Hatua ya ujenzi iliyofikiwa na soko hilo ni kielelezo cha uthubutu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kiuchumi na kijamii,Niwaombe watanzania wenzangu tuendelee kumuunga mkono kwa kumchagua kwa kura nyingi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ili aendeleze Jitihada za kuleta maendeleo"alisema waziri Mwigulu Kaimu mkurugenzi wa Jiji la mwanza Erick Mvati akitoa taarifa kuhusu mradi wa uje...

Mbunge Agnes Mathew Marwa Achangia Mbao 415 Kwa Ajili ya Kuezeka Nyumba ya Katibu wa UWT Musoma Mjini

MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Mara Mhe. Agnes Mathew Marwa amechangia mbao 415 kwa ajili ya kuezeka nyumba ya Katibu wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM ( UWT ) Musoma mjini iliyoanza kujengwa toka 2023. Mhe. Agnes Mathew amekabidhi mbao hizo wakati wa sherehe ya maadhimisho ya wiki ya Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) iliyofanyika Septemba 16 Kamnyonge manispaa ya Musoma. Akizungumza wakati wa kukabidhi mbao hizo kwa niaba ya Mhe. Agness Mathew diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Musoma amesema katika ametoa mchango huo ili kuweza kukamilisha nyumba hiyo ili kumuwezesha katibu kutekeleza majukumu ya Jumuiya na Chama kwa ufanisi.. Stella Mtani ni mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Musoma akizungumza katika madhimisho ya sherehe hizo amesema nyumba hiyo ya katibu ilianza kujengwa tangu mwaka 2023 na wamekua wakipokea vifaa kutoka kwa viongozi mbalimbali huku akieleza kuwa Mhe. Agness mbali na kuchangia mbao hizo 415 lakini pia aliwahi kuchangia mifuko 40 ya sementi wakati jengo hilo lilipoanza kujengwa...