Skip to main content

Posts

Showing posts from September 25, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

EWURA YAWEKA MAZINGIRA RAFIKI KWA WAWEKEZAJI NA WATOA HUDUMA KANDA YA ZIWA

GEITA: Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Ziwa, Nyirabu Musira, amesema mamlaka hiyo imeendelea kuweka mazingira rafiki kwa wananchi, wawekezaji na watoa huduma kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa huduma bora za nishati na maji katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. Musira ameyasema hayo leo, Septemba 25, 2026, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la EWURA kwenye Maonesho ya Tisa ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Geita. Amesema EWURA inatumia maonesho hayo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu udhibiti wa huduma za nishati na maji, pamoja na kuwaeleza haki na wajibu wao kama watumiaji wa huduma hizo. Kwa mujibu wa Musira, Kanda ya Ziwa inayojumuisha mikoa ya Mwanza, Geita, Simiyu, Mara na Kagera, imeendelea kupewa elimu kuhusu fursa za uwekezaji katika sekta zinazodhibitiwa na EWURA, pamoja na taratibu za kupata huduma na vibali. Amesema moja ya ...

C-CEOs FORUM KUWA CHACHU YA UTEKELEZAJI WA DIRA 2050

Na Mwandishi wa OTR - Arusha. Serikali imesema Mkutano wa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma (C-CEOs Forum) 2026, unaotarajiwa kuwakutanisha viongozi kutoka Mashirika zaidi ya 300 ya Umma, pamoja na wawakilishi wa Sekta Binafsi na washiriki wengine zaidi ya 700 kuanzia Septemba 28 hadi 30, 2026, utakuwa jukwaa muhimu la kuimarisha utendaji, tija na mchango wa Mashirika hayo katika utekelezaji wa Dira 2050. Forum hiyo, inayoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR), ni ya nne kufanyika tangu kuanzishwa kwake mwaka 2023 na inalenga kuwakutanisha Wenyeviti wa Bodi, Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Umma na wadau mbalimbali kujadili namna ya kuongeza ufanisi wa taasisi hizo na kuhakikisha mipango na shughuli zao zinaendana na vipaumbele vya kitaifa vilivyoainishwa katika Dira 2050. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ijumaa, Septemba 25, 2026, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla, alisema kuwakutanisha viongozi wa Mashirika ya Umma katika...

BoT YANUNUA ZAIDI YA TANI 30 ZA DHAHABU

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imefanikiwa kununua zaidi tani 30 za dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo, wa kati na wakubwa walio rasmi, hatua ambayo imechangia kuongeza akiba ya fedha za kigeni ya nchi kwa takribani Dola za Marekani bilioni 2.05. Akizungumza kuhusu mpango huo na waandishi wa habari Septemba 25,2026 katika Maonesho ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini kwenye viwanja Vya Dkt.Samia Suluhu Hassan mkoani Geita, Mchambuzi wa Fedha Mwandamizi kutoka BoT, Idara ya Masoko ya Fedha za Nje, Glory Gabriel Maembe,  amesema mpango wa Benki Kuu wa kununua dhahabu nchini umetekelezwa kwa takribani miaka miwili kwa lengo la kuongeza akiba ya fedha za kigeni. Kwa mujibu wa Maembe, ununuzi huo umewezesha BoT kupata kiasi kikubwa cha dhahabu kutoka ndani ya nchi na hivyo kuongeza mchango wa sekta ya madini katika kuimarisha akiba ya taifa ya fedha za nchi. Mbali na kuongeza akiba hiyo, mpango huo umeendelea kutoa soko la uhakika kwa wachimbaji wa dhahabu nchini, huku ukichochea urasimish...

RC ARUSHA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI HOYCE TEMU WAKATI TANZANIA IKIJIANDAA NA MKUTANO WA 153 WA BUNGE LA DUNIA

 Na Prosper Makene  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla leo Alhamisi Septemba 24, 2026 Ofisini kwake Jijini Arusha, amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Muwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa- Geneva Uswisi, Balozi Dkt. Hoyce Anderson Temu. Balozi Temu yupo Mkoani Arusha kushirikiana na Serikali katika maandalizi ya Mkutano wa 153 wa Bunge la dunia (IPU), utakaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) kuanzia tarehe 05 hadi 09, Oktoba mwaka huu, Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuandaa mkutano huu mkubwa wa kihistoria utakaowakutanisha Maspika na Wabunge kutoka Nchi 183 wanachama wa IPU, Mkutano ukiwa na kaulimbiu isemayo "Kuimarisha utawala bora na kuwezesha jamii kupitia ushirikishwaji, imani na fursa kwa wote."

VETA SHINYANGA YAJA NA TEKLOJIA YA KUONGEZEA THAMANI MADINI

Na Mwandishi wetu  Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Mkoa wa Shinyanga kimewahamasisha vijana na wachimbaji wadogo nchini kote kuchangamkia fursa ya mafunzo ya ukataji na ung'arishaji wa madini ya vito, hatua inayolenga kukuza uongezaji thamani ya rasilimali hizo hapa nchini. Wito huo umetolewa na Mkufunzi wa Thamani ya Madini wa chuo hicho, Robert Onesmo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari katika Maonesho ya Tisa ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, mkoani Geita. Onesmo amesema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya Serikali ya kuhakikisha hakuna madini ghafi yanayosafirishwa nje ya nchi bila kuongezewa thamani. Lengo kubwa ni kuongeza thamani ya madini yetu hapa hapa nchini kabla ya kusafirishwa au kuuzwa, ili nchi na wananchi wanufaike zaidi," amesema Onesmo. Ameongeza kuwa chuo kinatoa mafunzo katika ngazi mbili ili kumwezesha kila mwenye nia kupata ujuzi kulingana na muda wake....