Skip to main content

Posts

Showing posts from August 5, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

RAIS SAMIA AMPOKEA MGENI WAKE RAIS MUSEVENI IKULU DAR ES SALAAM

Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni baada ya kuwasili katika Viwanja vya Ikulu Jijiji Dar es Salaam na kupokelewa na Mwenyeji wake Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 06 Agosti, 2026.

ADEM YAJENGA VIONGOZI WA ELIMU KUELEKEA DIRA YA TAIFA 2050

 Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) umeendelea kuwa nguzo muhimu katika kuimarisha ubora wa uongozi kwenye sekta ya elimu nchini kwa kuwajengea uwezo viongozi na watendaji kupitia mafunzo ya kitaalamu, tafiti na ushauri elekezi unaolenga kuongeza ufanisi wa usimamizi wa taasisi za elimu. Akizungumza kuhusu utekelezaji wa Mwaka wa Fedha 2025/26 na mwelekeo wa mwaka 2026/27 katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dodoma, Mtendaji Mkuu wa ADEM, Dkt. Maulid Maulid, amesema taasisi hiyo imeendelea kutoa programu mbalimbali zinazolenga kuwawezesha viongozi wa elimu kukabiliana na changamoto mpya za sekta hiyo, ikiwemo matumizi ya teknolojia, usimamizi wa rasilimali, utekelezaji wa mitaala iliyoboreshwa na uboreshaji wa mazingira ya kufundishia na kujifunzia. Amesema kwa zaidi ya miaka 25 ya utekelezaji wa majukumu yake, ADEM imekuwa ikitoa mchango mkubwa katika kuandaa viongozi wenye uwezo wa kusimamia mabadiliko na kusaidia Serikali kufikia malengo ya kujenga mfumo ...

UWT TAIFA YATUA TANGA MJINI: MHE. SEKIBOKO AKAGUA MIRADI YA MIKOPO YA ASILIMIA 10

 Na Mashaka Mhando, TANGA UMOJA wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Tanga Mjini umepata ugeni mzito kutoka ngazi ya Taifa, katika ziara iliyolenga kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hususan uwezeshaji wa wanawake kiuchumi kupitia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Serikali. Ziara hiyo iliyofanyika jana, Agosti 5, 2026, iliongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UWT Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga, Mhe. Husna Sekiboko. Lengo kuu la ufuatiliaji huo ilikuwa ni kujionea kwa vitendo namna mabilioni ya fedha yanayotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, yanavyoendelea kuboresha maisha ya wananchi, hasa wanawake na makundi maalum. Ukaguzi wa Miradi ya asilimia 10 Akiwa wilayani humo, msafara wa Mhe. Sekiboko ulianza kwa kutembelea eneo la mradi wa ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi wa UWT lililopo Mtaa wa Amboni Kihongwe, katika Kata ya Mzizima. Baada ya hapo, viongozi hao walifanya ziara ...

DC MBEYA AKAGUA KIWANDA CHA BILIONI 15.5, APONGEZA MAPINDUZI YA AJIRA NA UCHUMI

 Na Mwandishi Wetu, MBEYA SERIKALI wilayani Mbeya imepongeza uwekezaji mkubwa wa zaidi ya Shilingi Bilioni 15.5 uliofanywa katika Kiwanda cha U Fresh kilichopo Mbalizi, ikieleza kuwa mradi huo ni chachu muhimu katika kuzalisha ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi wa viwanda mkoani humo. Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mhe. Solomon Itunda, alipoongoza Kamati ya Usalama ya Wilaya hiyo kufanya ziara ya ukaguzi wa shughuli za uzalishaji katika kiwanda hicho kilichopo mkabala na Uwanja wa Ndege wa Songwe. Akizungumza mara baada ya Kamati hiyo kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji zinazoendelea, Mhe. Itunda alisema uwepo wa uwekezaji wa kiwango hicho unasaidia kukuza uzalishaji wa ndani, kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa nchini, na kutoa fursa nyingi za ajira kwa wananchi. Mkuu huyo wa wilaya alitumia fursa hiyo kumshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisema uwekezaji huo ni matunda ya mazingira wezeshi ...

MAPINDUZI RELI YA KASKAZINI: TRC YAPOKEA VIFAA VYA DOLA MILIONI 56, RC BATILDA APONGEZA

 Na Mashaka Mhando, TANGA HATUA ya Serikali ya Awamu ya Sita kuboresha miundombinu ya usafirishaji imepata msukumo mpya mkoani Tanga, kufuatia Shirika la Reli Tanzania (TRC) kupokea shehena ya vipande 17,006 vya reli na vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya takribani Dola za Marekani Milioni 56. Kupatikana kwa vifaa hivyo ni sehemu ya mkakati wa kuboresha Reli ya Kaskazini inayounganisha Bandari ya Tanga na mikoa ya Kilimanjaro na Arusha, hatua inayotarajiwa kuchochea biashara na kukuza uchumi wa mkoa huo na Taifa kwa ujumla. Akizungumzia mapokezi hayo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian, amelipongeza Shirika la TRC huku akibainisha kuwa uwekezaji huo unaenda sambamba na utekelezaji wa miradi ya Reli ya Kisasa (SGR) inayoendelea nchini. "Serikali inaendelea kuwekeza kwa nguvu katika miundombinu ya reli. Maboresho haya ya Reli ya Kaskazini yanalenga kuongeza kasi ya treni na uwezo wa kubeba mizigo mizito, hivyo kuongeza ufanisi mkubwa wa usafirishaji wa mizigo na a...

KISHINDO CHA NGORONGORO SCHOLARSHIP FUND

 Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) kwa kushirikiana na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu  (HESLB) imetoa elimu kwa jamii ya Ngorongoro kuhusu  mfuko wa  Ngorongoro Scholarship Fund  unaolenga kuwezesha wanafunzi wanaoishi ndani ya hifadhi ya Ngorongoro kupata fursa ya masomo ya elimu ya juu kupitia ufadhili Ngorongoro Fund.   Elimu hiyo iliyotolewa katika ofisi za Ngorongoro ilijumuisha wadau muhimu wanaoguswa na mpango huo ambao ni viongozi wa jamii, wanafunzi pamoja na wadau mbalimbali ambao wamepewa uelewa kuhusu vigezo vya mkopo, sifa za waombaji pamoja na kupitia na kujadili mwongozo wa programu ya Ngorongoro Scholarship Fund. Katika kikao hicho, viongozi wa jamii wamepongeza hatua ya Mamlaka ya kushirikiana na HESLB katika kuandaa na kuboresha mwongozo wa mfuko huo, wakieleza kuwa utasaidia kuweka utaratibu unaozingatia usawa, uwazi na mahitaji ya wakati katika kuwawezesha wanafunzi wenyeji kupata fursa za elimu ya juu. Mw...

CDICD YAONGEZA THAMANI YA BLACK GRANITE

 🔸Uchakataji wa kisasa waongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika soko la ndani na nje 🔸Uwekezaji wa kampuni wafungua ajira kwa vijana na kuchochea maendeleo ya viwanda 📍Dodoma Kampuni ya CDICD Group Limited imeendelea kuimarisha mnyororo wa thamani katika Sekta ya Madini kwa kuchakata madini ya black granite na kuzalisha bidhaa mbalimbali za ujenzi zinazouzwa katika soko la ndani na nje ya nchi, hatua inayochochea ukuaji wa viwanda, kuongeza ajira na kukuza mauzo ya bidhaa zenye thamani. Akizungumza jijini Dodoma kwenye Maonesho ya Nane Nane, Meneja wa CDICD, Shija Shimba, amesema kampuni hiyo imewekeza katika kiwanda cha kisasa cha uchakataji wa black granite kinachobadilisha mawe ghafi kuwa bidhaa mbalimbali zikiwemo countertops za majiko, paving stones, slabs za ujenzi na headstones zinazotumika katika makaburi. Amesema shughuli za uchimbaji na uchakataji zinafanyika katika kijiji cha Manyemba, wilayani Chamwino mkoani Dodoma, ambapo kampuni imejikita katika kuonge...