Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Mhe. Ghati Zephania Chomete ameendelea kushiriki katika shughuli za **Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo**, ambayo tarehe 14 Machi ilifanya ziara ya kikazi katika Kituo cha Uhakiki cha Misugusugu kilichopo Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani. Ziara hiyo ya Kamati iliongozwa na Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Deodatus Philip Mwanyika, ikiwa na lengo la kukagua mradi wa Wakala wa Vipimo (WMA) pamoja na kujionea utekelezaji wa majukumu ya wakala huo katika kuhakikisha usahihi wa vipimo vinavyotumika nchini. Katika ziara hiyo, Kamati ilikagua mitambo mbalimbali inayotumika katika uhakiki wa vipimo, ikiwemo mitambo ya uhakiki wa mita za umeme, mita za maji pamoja na mifumo ya uhakiki wa matenki ya kupimia mafuta. Hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuwa vipimo vinavyotumika katika shughuli za kiuchumi vinakuwa sahihi ili kulinda haki za watumiaji na wafanyabiashara. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Deodatus Phil...
Marato tv - Sauti ya Jamii