Na Angela Sebastian; Biharamulo Kuongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Ismail Ali Ussi amewataka mkuu wa mkoa wa Kagera,wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri zote na Manispaa ya Bukoba kuwahamasisha wananchi kutumia Nishati safi ili kuepukana na athari za kiafya zitokanazo na nishati chafu. Ametoa ushauri huo akiwa Wilayani Biharamulo ambapo amesema viongozi hao wanakumbuka kwamba Rais Dk Samia Suluhu Hassan amekuja na kampeni ambayo ina lengo la kuwasaidia wananchi wa Tanzania ikiwemo Biharamulo ambapo inaenda kuwajali na kuwagusa wananchi moja kwa moja kwa kuweka Afya zao kuwa imara. "Dk.Samia amekuja na utaratibu wa uhamasishaji wa matumizi ya gesi na Nishati safi mbadala katika maeneo mbalimbali ndani ya Taifa hili ,ndiyo maana yapo maelezo yaliyotolewa kwa wakuu wa mikoa,Wilaya na wakurugenzi kuwataka wahamasishe kampeni hiyo katika maeneo ambayo yana mkusanyiko wa kuanzia watu 100 na kuendelea ikiwa ni ya binafsi au Serikali kuhakikisha wanatumia gesi ambapo shu...
Marato tv - Sauti ya Jamii