Skip to main content

Posts

Showing posts from April 27, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Uwasilishaji wa bajeti ya Wizara ya Nishati 2025/2026 Bungeni Dodoma

  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akiwasilisha Hotuba ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa mwaka 2025/2026 bungeni jijini Dodoma. @biteko @wizara_ya_nishati_tanzania @onwm_tanzania @judith__kapinga @bunge.tanzania

Naibu Waziri Mkuu Dkt Biteko ahimiza kanisa kuliombea Taifa

  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Serikali chini ya Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inalojukumu la kuhakikisha uchaguzi Mkuu unafanyika kwa amani na haki. “Wito wangu kwa kanisa ni kuendelea kuliombea Taifa liendelee kuwa na amani,” amesema na kuongeza kuwa atamtaatifu Mhe. Rais kuhusu ahadi ya maaskofu kuliombea taifa hili kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao. s Dkt. Biteko amesema hayo Aprili 27, 2025 Iringa Mjini alipomwakilisha Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni maalum katika sherehe ya kusimikwa na kuwekwa wakfu kwa Askofu wa Jimbo la Iringa, Mhashamu Romanus Mihali.

Romanus Mihali asimikwa rasmi kuwa Askofu Jimbo la Iringa

  📌 Dkt. Biteko amwakilisha Rais Samia kuwa mgeni maalum Kusimikwa Askofu Romanus Mihali 📌 Asema Serikali itahakikisha uchaguzi unakuwa wa huru na haki 📌  TEC yaipongeza Serikali kwa kuendeleza Uhuru wa kuabudu nchini Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewaomba viongozi wa dini nchini kuliombea Taifa wakati huu wakati Tanzania inaelekea katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani ili kuendelea kuwa na amani. Dkt. Biteko amesema hayo Aprili 27, 2025 Iringa Mjini alipomwakilisha Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni maalum katika sherehe ya kusimikwa na kuwekwa wakfu kwa Askofu wa Jimbo la Iringa, Mhashamu Romanus Mihali. Dkt. Biteko amesema Serikali chini ya Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inalojukumu la kuhakikisha uchaguzi Mkuu unadanyika kwa amani na haki. “Wito wangu kwa kanisa ni kuendelea kuliombea Taifa liendelee kuwa na amani,” amesema na kuongeza kuwa atamtamtaatifu Mhe...

Waziri Mkuu aagiza ufuatiliaji wa Watendaji wa vyama vya ushirika

  ▪️Awasisitiza Watendaji hao wazingatie maadili ya utumishi, uwazi na utawala bora WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo iimarishe na kufanya ufuatiliaji wa Watendaji wa Vyama vya Ushirika ili wazingatie maadili ya utumishi wa ushirika, uwazi, uwajibikaji na utawala bora, na hivyo kuwavutia wanachama na wawekezaji. Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo, pamoja na Tume ya Maendeleo ya Ushirika, iharakishe na kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mikakati yote iliyopitishwa, hususan katika maeneo ya teknolojia ya kilimo, upatikanaji wa pembejeo, na masoko ya mazao. Ametoa maagizo hayo leo (Jumapili, Aprili 27, 2025) alipozindua mdahalo wa Upatikanaji Mitaji ya Fedha za Maendeleo ya Ushirika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete, jijini Dodoma. Pia, Waziri Mkuu amezindua ripoti ya Mwaka ya Kilimo kwa mwaka 2022/2023, 2023/2024. Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuzisisitiza taasisi za kifedha, zikiwemo benki na mifuko ya maendeleo, ziendelee kushiri...

Serikali yatunga kanuni kuzuia wageni kuingia kwenye leseni ndogo za uchimbaji madini bila utaratibu

  Serikali kupitia Wizara ya Madini imetunga kanuni za msaada wa kiufundi katika Leseni ndogo za uchimbaji wa Madini ambapo zitaratibu ushiriki wa wageni katika Leseni ndogo za uchimbaji wa Madini(PML) ambazo kwa mujibu wa kifungu cha 8 cha Sheria ya Madini sura ya 123,kimezitamka Leseni hizi kama maalum kwa ajili ya Watanzania. Kifungu cha 8(3) cha Sheria ya Madini kinatoa ruhusa kwa mmiliki wa Leseni ndogo ya uchimbaji madini kuingia ubia na mgeni kwa makubaliano ya msaada wa kiufundi(𝙏𝙚𝙘𝙝𝙣𝙞𝙘𝙖𝙡 𝙎𝙪𝙥𝙥𝙤𝙧𝙩). Akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka 2024/25 Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde alisema Serikali inatarajia kutunga kanuni za kuratibu ushiriki wa wageni katika Leseni ndogo kwa kuwa kumejitokea wimbi kubwa la wageni kuingia katika maeneo ya wachimbaji wadogo kwa mgongo wa “Msaada wa Kiufundi”ambao haukuwa na utaratibu mzuri na hivyo kupelekea wachimbaji wengi wadogo kutopata manufaa yaliyokusudiwa ya kujiimarisha kupitia Leseni ndogo za u...