Watumishi Wlwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Watakiwa Kuendelea Kuzingatia Maadili ya Utumishi wa Umma
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari amewataka Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma ili waweze kutoa huduma bora kwa Wananchi. Mwanasheria Mkuu wa Serikali amezungumza hayo wakati akifungua Mafunzo elekezi kwa Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yaliyofanyika tarehe 13 Machi, 2025 Jijini Dodoma. Akizungumza wakati akifungua Mafunzo hayo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amewakumbusha Watumishi umuhimu wa utoaji wa huduma za ushauri wa kisheria, ushughulikiaji wa malalamiko ya wananchi kwa kuzingatia Katiba, Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali ambayo imetolewa wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku. *“Tunatakiwa kuendelea kuzingatia Sheria na Kanuni tulizojiwekea ili tuweze kutoa huduma bora na stahiki kwa wananchi.”* Amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali Aidha, Mhe. Johari amewahimiza Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuendelea kusoma Mpango Kazi w...