Skip to main content

Posts

Showing posts from December 6, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Kiruswa Atatua Mgogoro wa Wachimbaji Longido

Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dkt. Steven Kiruswa ametatua mgogoro wa wachimbaji wadogo wa Madini ya Ruby Wilaya ya Longido Mkoani Arusha uliodumu zaidi ya miaka mitano kati ya Kampuni ya Paradiso Mineral (T) Limited na Mzee Malulu Ole Moringo kwa Kampuni hiyo kukubali kumlipa fidia Mzee Malulu Ole Moringo ya jumla ya shillingi milioni miamoja na hamsini ili kupisha shughuli za uchimbaji madini. Makubaliano hayo yameafikiwa leo Desemba 6, 2025 wakati Mhe. Dkt. Kiruswa alipofanya ziara ya kutatua mgogoro huo katika Kata ya Mundarara Wilaya ya Longido Mkoani Arusha.  Mhe. Dkt. Kiruswa ameielekeza kampuni ya Paradiso kutekeleza makubaliano walioafikiana na Mzee Malulu Ole Moringo ya kulipa fidia hiyo kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza wanatakiwa kulipa milioni 100 ifikapo Januari 30, 2025 na milioni 50 ifikapo Machi 30, 2025. Aidha, Dkt. Kiruswa amesisitiza makubaliano hayo kutekelezwa kwa wakati na endapo kampuni ya Paradiso itakiuka makubaliano hayo Serikali itachukua hatua za kis...

Kaya 19,530 Kunufaika na Majiko ya Gesi ya Ruzuku Mkoani Arusha

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia mkataba na mtoa huduma Kampuni ya Lake Gas Limited kwa ajili ya kutekeleza mradi wa shilingi milioni 406.7 wa kusambaza majiko ya gesi 19,530 (LPG) ya kilo sita kwa bei ya ruzuku ya 50% katika maeneo ya vijijini ndani ya Wilaya ya Arusha, Karatu, Longido, Meru, Monduli na Ngorongoro Mkoani Arusha. Kaimu Meneja Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi REA, Mhandisi Emanuel Yesaya amebainisha hayo Desemba 6, 2024 Mkoani Arusha wakati wa kumtambulisha mtoa huduma katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo. "Tumeanza utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ambao unasisitiza miaka 10 kutoka sasa 80% ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia, na hili linaweza kufikiwa kupitia mbinu na mikakati mbalimbali ikiwemo hii ya usambazaji wa majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku," alisema Mhandisi Yesaya. Alifafanua kuwa REA imeandaa programu mbalimbali ili kufanikisha azma hiyo ya Serikali ambayo imeasisiwa ...

Naibu Waziri Mkuu ahimiza wadau kuchangia ujenzi wa kituo cha wanafunzi UDSM

Awashukuru Wadhamini wa UDSM Marathon UDSM Marathon kuboresha maisha ya wanafunzi. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameeleza amefurahishwa kwake na uendeshaji wa UDSM Marathon na kusema kuwa inasaidia kufanikisha malengo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuendelea kutoa elimu bora na kuboresha mazingira ya wanafunzi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Desemba 7, 2024 mara baada ya kushiriki mbio hizo za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM MARATHON) zilizofanyika chuoni hapo. “ Ni dhahiri kwamba mbio hizi zimekuwa muhimu kwa Chuo hiki na jamii kwa ujumla. Tukio hili limeleta pamoja wadau mbalimbali na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika juhudi za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia,” amesema Dkt. Biteko. Ameongeza “Natambua kwa misimu mitano mbio hizi zimekua zikichangia katika ujenzi wa Kituo cha Wanafunzi kinachojengwa hapa katika Kampasi Kuu ya Mwalimu Nyerere Mlimani. Ujenzi wa kituo hiki ulianza kwa michango kutoka kwa wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar ...

Msigiwa atoa maagizo kwa waajiri Nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa amewataka waajiri na viongozi katika ofisi za umma kuwapa fursa Waandishi Waendesha Ofisi (Masekretari) kuwasidia katika uandishi wa Kiswahili sanifu na fasaha katika nyaraka mbalimbali. Msigwa amesema hayo mkoani Morogoro wakati akifunga Mafunzo ya Matumizi ya Kiswahili Sanifu na Fasaha kwa Waandishi Waendesha Ofisi yaliyosimamiwa na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA). Amesema, kwa kuwa viongozi na waajiri wengi wana kazi nyingi za kufanya zinazo wafanya wakose muda wa kuandika Kiswahili Sanifu na Fasaha, inabidi wawape fursa Waandishi Waendesha Ofisi wao kwasababu wamepata mafunzo ya namna ya kuandika kiswahili Sanifu na Fasaha. Aidha, Msigwa amewataka Viongozi kuwapeleka Waandishi Waendesha Ofisi wao katika Mafunzo ya Matumizi ya Kiswahili Sanifu na Fasaha na Mafunzo mengine ya ndani na nje ya nchi ili waweze kuwasaidia vyema kwakuwa ndio wasaidizi wao wa karibu katika uandaaji wa taarifa na nyaraka mbalimbali za ...

Jwtz yaendelea kung'ara ndani na nje kimataifa katika ulinzi wa amani