Skip to main content

Posts

Showing posts from June 8, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

SERIKALI YAAGIZA TATHMINI YA HARAKA IFANYIKE KORONGO LA STAREHE TARIME MJINI

Serikali imeahidi kuchukua hatua za kudumu kukabiliana na tatizo la mmomonyoko wa ardhi na mafuriko yanayosababishwa na Korongo la Starehe katika Jimbo la Tarime Mjini, mkoani Mara. Kauli hiyo imetolewa leo Juni 10, 2026, Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Festo Dugange, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini, Esther Matiko, kuhusu hatua za Serikali kudhibiti korongo hilo ambalo limeendelea kuhatarisha maisha, mali na makazi ya wananchi. Dkt. Dugange amesema Serikali imeweka kipaumbele katika kuondoa maeneo hatarishi na kuboresha miundombinu ya kudhibiti mafuriko na mmomonyoko wa ardhi katika maeneo mbalimbali nchini. "Tutafanya tathmini ya kina kubaini sababu zinazofanya korongo hili kuendelea kuharibika licha ya jitihada zilizowahi kufanyika, na tutachukua hatua za kitaalamu kuhakikisha suluhisho la kudumu linapatikana," amesema. Aidha, ameelekeza Meneja wa TARURA Mkoa wa Mara pamoja na Meneja wa TARURA Tarime Mjini ...

SERIKALI KUJENGA MADARAJA YA NYASAUNGU NA TUGUTI MUSOMA VIJIJINI

  Akiuliza swali bungeni, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Agnes Marwa, alitaka kujua ni lini Serikali itajenga Madaraja ya Nyasaungu na Tuguti yaliyopo katika barabara ya Musoma Busekela, ambayo ni miongoni mwa barabara muhimu za kiuchumi katika Wilaya ya Musoma Vijijini. Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, amesema Serikali inatambua umuhimu wa barabara hiyo katika kukuza shughuli za kiuchumi na kurahisisha usafiri wa wananchi wa eneo hilo. Mhandisi Kasekenya amesema tayari zabuni ya ujenzi wa kilomita 40 za barabara hiyo imeshatangazwa, huku madaraja ya Nyasaungu na Tuguti yakitengwa na mradi huo ili yajengwe kwa utaratibu maalum utakaochochea utekelezaji wake kwa haraka zaidi. "Tunafahamu barabara hii ni muhimu kwa uchumi wa wananchi, na madaraja hayo ni muhimu. Serikali inaendelea na taratibu za kuyajenga pamoja na utekelezaji wa kilomita 40 za barabara ambayo tayari imeshatangazwa," amesema Mhandisi Kasekenya. Ujenzi wa madaraja hay...

RAIS WA SINGAPORE AWASILI TANZANIA KWA ZIARA YA KISERIKALI YA SIKU TATU

Rais wa Jamhuri ya Singapore, Mhe. Tharman Shanmugaratnam, amewasili nchini Tanzania kwa ziara ya Kiserikali ya siku tatu kuanzia Juni 8 hadi 10, 2026. Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam, Rais Tharman Shanmugaratnam akiwa ameambatana na mkewe, Bi. Jane Ittogi Shanmugaratnam, alipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Mhandisi Peter Ulanga. Ziara hii ya Kiserikali ni ya kwanza kufanywa na Rais wa Singapore nchini Tanzania tangu mataifa hayo mawili yalipoanzisha uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1980. Ziara hiyo inaashiria hatua muhimu katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Singapore. Wakati wa ziara yake, Rais Tharman atapokelewa rasmi n...

WILAYA YA LUSHOTO YAPOKEA MRADI NA USAMBAZAJI NA UUZAJI WA MITUNGI YA GESI KWA BEI YA RUZUKU

📍 *Lushoto, Tanga* Wananchi wa Wilaya ya Lushoto wamepata fursa mpya ya kunufaika na nishati safi ya kupikia baada ya wilaya hiyo kupokea rasmi mradi wa usambazaji na uuzaji wa mitungi ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Mradi huo umepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Mheshimiwa Zephania Sumaye, kwa niaba ya wananchi wa wilaya hiyo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuhakikisha nishati safi ya kupikia inawafikia Watanzania wengi zaidi. Hafla ya mapokezi ya mradi huo imefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Lushoto na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, maafisa kutoka REA pamoja na wawakilishi wa kampuni ya Manjis Logistics Limited, ambayo imepewa jukumu la kutekeleza mradi huo kwa kushirikiana na REA. Mradi huo ni miongoni mwa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na REA nchini kwa lengo la kuharakisha upatikanaji wa nishati safi na salama kwa wananchi, kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa, pamoja na kuunga m...

ZUNGU ASISITIZA KASI YA UJENZI WA SHULE YA MFANO YA CRDB UPANGA

 Mbunge wa Jimbo la Ilala na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu, amemtaka mkandarasi anayejenga Shule ya Sekondari ya Mfano ya CRDB iliyopo Kata ya Upanga Mashariki jijini Dar es Salaam kuongeza kasi ya ujenzi ili mradi huo ukamilike kwa wakati na kuanza kutumika Januari 2027. Mhe. Zungu ametoa maelekezo hayo Juni 7, 2026 alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo akiwa ameambatana na TullyEsther Mwambapa. Akizungumza katika ukaguzi huo, Mhe. Zungu ameipongeza CRDB Bank chini ya uongozi wa Abdulmajid Nsekela kwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha sekta ya elimu nchini. Amesema mradi huo wenye thamani ya takribani shilingi bilioni tano ni uwekezaji muhimu utakaosaidia kuongeza upatikanaji wa elimu bora kwa wanafunzi wa Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi. Kabla ya ukaguzi huo, Mhe. Zungu alishiriki mkutano wa kikanuni wa maendeleo wa wananchi wa Kata ya Upanga...

CCM IMEAGIZA KERO YA MAJI IMALIZWE HARAKA WILAYANI SAME

*Asisitiza Tsh Trilioni 1.2 zimewekezwa Kilimanjaro, sasa ni zamu ya mfumo wa Usambazaji.* MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Baraa, Stephen Wasira, ameiagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Same (SAUWASA) kuhakikisha inatatua kwa haraka changamoto ya upatikanaji maji inayowakabili wananchi wa mji wa Same. Wasira alitoa agizo hilo leo Juni 8, 2026 alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM wa Shina Namba 9, Tawi la Same, Kata ya Same, wilayani Same mkoani Kilimanjaro. Akijibu malalamiko ya wananchi kuhusu ukosefu wa maji, alisema haikubaliki kwa wakazi wa Same kuendelea kukosa huduma hiyo muhimu wakati maji yanapatikana kwa wingi kupitia miradi iliyotekelezwa na serikali. “Ninaiagiza SAUWASA kuhakikisha wananchi wa Same wanapata maji. Haiwezekani watu wa Same waendelee kuyasikia au kuyaona maji bila kuyapata kwa matumizi yao ya kila siku, mfumo wa usambazaji uharakishwe ili wananchi wanufaike na huduma hiyo muhimu,” alisema Wasira. Alibainisha kuwa, serika...

AHMED ALLY WA SIMBA ATOA MAAGIZO HAYA HUKO MKOANI KAGERA

 Na Angela Sebastian ;Muleba ‎MSEMAJI wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amemtaka mwaandaaji wa Mashindano ya Mwijage Cup ambayo yanahusisha timu 20 za ndondo kutoka katika Tarafa ya Kamachumu Wilayani Muleba mkoani Kagera, kuyafanya kwa malengo ya muda mrefu na yawe yenye kuibua vipaji kuliko kusubiri muda wa kuomba kura au jambo fulani linalohusu maslahi binafsi. Ally ametoa rai hiyo jana wakati akizindua mashindano hayo katika uwanja wa mpira wa polisi Kamachumu ulioko katika kata ya Kamachumu ambayo yanalenga kuwasaidia vijana kujengewa uwezo wa kucheza mpira wenye viwango vya kimataifa,kuinua vipaji na kutengeneza vipaji vipya kwenye mpira wa miguu kutoka ngazi za chini watakaokwenda kucheza kwenye timu kubwa hapo baadaye. "Mwanzilishi na mdhamini wa mashindano haya (Paul Mwijage) jamii mnapaswa kumuunga mkono ili aendeelee kuwafanyia mema wana michezo hasa wakazi wa Tarafa Kamachumu kwani malengo yake ni kuwaunganisha nyinyi hususani vijana kupitia michezo hivyo yawe endelevu...

ZUNGU:AITAKA NHC KUJENGA NYUMBA ZA BEI NAFUU ILALA

Mbunge wa Jimbo la Ilala na Spika wa Bunge, Mussa Zungu, ameibeba ajenda ya makazi na ustawi wa wananchi kwa kuitaka NHC kujenga nyumba za gharama nafuu zitakazowawezesha wananchi wa kipato cha chini na cha kati kupata makazi bora bila kubanwa na gharama kubwa za upangaji. Akizungumza katika mkutano wa wananchi wa Mitaa ya Kibasila na Kitonga, Kata ya Upanga Mashariki, Zungu alisema maendeleo ya miji yanapaswa kwenda sambamba na kulinda maslahi ya wananchi, akisisitiza kuwa uwekezaji wa makazi usiwe chanzo cha kuwaondoa au kuwaumiza wananchi waliotegemea nyumba hizo kwa miaka mingi. "Tunataka maendeleo yanayowajali wananchi. Nyumba za gharama nafuu zinawezekana na zina hadhi. NHC inapaswa kujenga nyumba zitakazowapa wananchi fursa ya kuishi kwa heshima na usalama," amesema Zungu. Katika mkutano huo, wananchi waliwasilisha kero mbalimbali ikiwemo uchakavu wa miundombinu ya maji, ukosefu wa vivuko salama vya waenda kwa miguu katika maeneo ya shule pamoja na changamoto zinazowak...