Skip to main content

Posts

Showing posts from May 17, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jkt Kusomwa Kesho Mei 19-2026

  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. *Dkt. Rhimo Nyansaho, (Mb)* amewasilisha hati za randama za makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026 /2027.  Uwasilishaji rasmi wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 utafanyika kesho Jumanne Mei 19, 2026 bungeni jijini Dodoma.

Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jkt Kusomwa Kesho Mei 19-2026

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. *Dkt. Rhimo Nyansaho, (Mb)* amewasilisha hati za randama za makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026 /2027.  Uwasilishaji rasmi wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 utafanyika kesho Jumanne Mei 19, 2026 bungeni jijini Dodoma.

Waziri Mkuu Amuaga Mkurugenzi Mkazi wa Benki Ya Dunia Kanda ya Malawi, Tanzania, Zambia na Zimbabwe

▪️Apongeza mchango wake katika maendeleo nchini. WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Mei 17, 2026 ameshiriki katika hafla ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Kanda ya Malawi, Tanzania, Zambia na Zimbabwe, Nathan Belete, iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Mwigulu alimpongeza Nathan kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia pamoja na kuunga mkono juhudi za maendeleo katika sekta mbalimbali nchini. Amesema kuwa imeshuhudiwa ongezeko kubwa na la kihistoria la ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia, ambapo takribani dola za Marekani bilioni 4.27 zilipatikana kupitia miradi na programu mbalimbali. “Niruhusuni kwa mara nyingine kutoa shukrani zangu za dhati kwa Nathan kwa huduma yake ya kujitolea na mchango wake mkubwa katika safari ya maendeleo ya Tanzania, na kumtakia mafanikio mema katika majukumu yake mapya,” amesema Dkt. Mwigulu. Aliongeza kuwa m...

Kazala: Migogoro ya Ardhi Kero Kubwa Kasulu Vijijini

MBUNGE wa Jimbo la Kasulu Vijijini, Mhe. Edibilly Kazala amesema ameendelea kuwa karibu na wananchi kupitia mikutano ya hadhara inayolenga kusikiliza changamoto zao na kutafuta suluhisho la kudumu kwa kushirikiana na Serikali. Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mei 17, 2026, Mhe. Kazala amesema tangu achaguliwe ameweza kufanya zaidi ya mikutano 50 ya kuzunguka na kufungua maeneo mbalimbali ya jimbo hilo, huku baada ya uchaguzi akifanya tena mikutano 58 ya kuwashukuru wananchi kwa imani waliyoionesha pamoja na kupokea kero zao moja kwa moja. Amesema kero kubwa inayowakabili wananchi wengi wa Kasulu Vijijini ni migogoro ya ardhi, hususan katika maeneo ya vijijini, ambapo wananchi wamekuwa wakikumbana na changamoto za mipaka, matumizi ya ardhi pamoja na maeneo ya makazi na shughuli za kilimo na ufugaji. “Migogoro mingi ya ardhi imekuwa ikiwatesa wananchi kwa muda mrefu, lakini Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inaendelea kuchukua hatua kuhakikisha wananchi wanapatiwa haki zao...

Dkt. Mwigulu Awahakikishia Wananchi Kasi ya Utekelezaji wa Miradi

_▪️ Asema utekelezaji wa Bwawa la Farkwa kuanza baada ya kukamilika kwa taratibu za manunuzi_ _▪️ Aagiza kukomeshwa kwa ukamataji usio na msingi wa vitendea kazi vya wananchi_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali imejipanga kuhakikisha miradi yote ya maendeleo iliyopungua kasi ya utekelezaji inaanza tena kutekelezwa kwa kasi inayotakiwa ili wananchi waendelee kunufaika na huduma za kijamii na kiuchumi. Amesema hayo leo Jumapili, Mei 17, 2026, alipowahutubia wananchi wa Wilaya ya Chemba katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kambi ya Nyasa, akiwa katika ziara ya kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi. Dkt. Mwigulu amesema baadhi ya miradi ilipungua kasi baada ya Serikali kuelekeza nguvu kubwa katika kukamilisha miradi ya kimkakati ya kitaifa iliyokuwa imefikia hatua za mwisho, ikiwemo Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere, reli ya kisasa pamoja na Daraja la Kigongo–Busisi.  “Kilichosababisha baadhi ya miradi kupungua kasi haikuwa uzembe wala kupuuza. Ilikuwa ni mka...

Hakuna Kutoka Mikono Mitupu Aweso Vijana Cup 2026

NA: MWANDISHI WETU, PANGANI  Timu zote 16 zilizoshiriki mashindano ya mpira wa miguu ya Aweso Vijana Cup 2026, zimeneemeka kushiriki mashindano hayo. Hii inatokana na uamuzi mfadhili wa mashindano hayo ambaye ni Mbunge wa Pangani na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, kuamua kupeleka tabasamu kwa timu zote. Katika hotuba yake aliyoitoa Mei 16, 2026, katika uwanja wa Kumba wilayani Pangani, siku ya fainali iliyozikutanisha timu za Kata za Bweni na Kimang'a, Aweso ameahidi kuzipa zawadi timu zote zilizoshiriki mashindano hayo. "Ndugu zangu, nazipongeza timu za Bweni na Kimang'a kwa mechi nzuri iliyokuwa na ushindani mkubwa katika fainali hii. Pamoja na hayo, naahidi kuzipa timu zote zilizoshiriki mashindano haya shilingi 500,000, jezi seti moja na mpira ili kuendeleza kukuza michezo wilayani kwetu," amesema Aweso. Maamuzi haya ni motisha kwa wachezaji wa timu zilizoshiriki mashindano hayo kuendelea kucheza kwa bidii ili kukuza vipaji vyao.  Katika mashindano hayo, timu 16 zili...

Wasira: Waliosababisha Vurugu Wapatikane, Ndipo Tuingie Maridhiano

*Ampongeza Rais Samia kuunda Tume kuchunguza kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu* MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema kabla ya kuanza kwa mchakato wa maridhiano ya kisiasa, ni vyema kuwabaini kuwachukulia hatua za kisheria kupitia vyombo vya haki watu waliohusika na vurugu zilizosababisha madhara vikiwamo vifo. Amempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuunda Tume ya Kuchunguza Vurugu za Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 kwa lengo la kujua kiini cha tatizo hilo. Wasira lieleza hayo jana  alipohutubia mkutano wa hadhara Mjini Kigoma akiwa katika ziara ya kichama mkoani humo. "Mimi sijasema jina la mtu, lakini wenye kujua hayo mambo wanajijua, waache jinai ichunguzwe kama walihusika waende kwenye vyombo vya haki na sio wengi, wanaobaki watu wema tukae tufanye nao maridhiano," alisema. Alimpongeza Rais Samia kwa kuunda tume ya kusaidia kujua chanzo cha vurugu hizo, pia alipongeza kazi nzuri iliyofanywa na tume hiy...

Tanzania Yaunga Mkono Maazimio ya Un Kutafuta Amani ya Kudumu Mashariki ya Kati

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesisitiza kuunga mkono kikamilifu maazimio yote ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) na jitihada za kimataifa zinazolenga kuleta amani ya kudumu katika ukanda wa Mashariki ya Kati kupitia njia za kidiplomasia. Msimamo huo umetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe (Mb), wakati wa maadhimisho ya miaka 78 ya Siku ya Nakba ya Taifa la Palestina yaliyofanyika Mei 16, 2026 jijini Dar es Salaam. Akizungumza mbele ya wajumbe wa mashirika ya kidiplomasia na viongozi mbalimbali wa kiserikali, Dkt. Maghembe alieleza kuwa msimamo wa Tanzania katika suala la Palestina na Israel unajengwa juu ya misingi thabiti ya Sera ya Kutofungamana na Upande Wowote (Non-Alignment Policy). “Katika muktadha huu, Tanzania inaendelea kuunga mkono maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na juhudi nyingine za jumuiya ya kimataifa zinazolenga kuendeleza mazungumzo ya kidiplomasia na utek...

Dkt. Mwigulu Asisitiza Kukamilika kwa Mradi wa Maji Chemba

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kuhakikisha Mradi wa Maji wa Miji 28 katika Mji wa Chemba unakamilika kwa wakati ili kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa Wilaya ya Chemba. “Wilaya ya Chemba ni moja ya wilaya zenye shida ya ukame na maji, lakini pia ni wilaya za uzalishaji, kwa hiyo tunahitaji sana mradi huu ukamilike haraka,” amesema. Waziri Mkuu amesema hayo leo Jumapili, Mei 17, 2026 wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Miji 28 katika Mji wa Chemba unaotekelezwa kupitia Wizara ya Maji kwa kushirikiana na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Chemba. Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Mkurugenzi wa Usambazaji Maji kutoka Wizara ya Maji, Eng. Charles Mafie amesema mradi huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 11 unatarajiwa kuhudumia wananchi zaidi ya 18,141 wa Mji wa Chemba pamoja na vijiji vya Chemba, Chambalo, Kambi ya Nyasa, Gwandi,...

Dkt. Mwigulu Ahimiza Wananchi Kuiombea Amani ya Nchi

WAZIRI MKUU, amewahimiza wananchi kuendelea kuiombea Tanzania ili amani, umoja na mshikamano wa kitaifa viendelee kuimarika sambamba na nchi kuendelea kupiga hatua za maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi. Amesema hayo leo Jumapili, Mei 17, 2026 aliposhiriki ibada katika (KKKT) Usharika wa Kondoa Mjini, Jimbo la Kondoa, Dayosisi ya Dodoma. Ibada hiyo iliongozwa na Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ya Dodoma, pamoja na Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kondoa Mjini na Mkuu wa Jimbo la Kondoa KKKT, . Waziri Mkuu amesema anaendelea kushirikiana na taasisi za dini nchini akitambua mchango wake katika kujenga jamii yenye maadili, umoja na maendeleo. “Ujumbe wake kwa wananchi wa Kondoa ni kwamba tuendelee kuiombea nchi yetu ili iendelee kuwa ya amani na kuendelea kupiga hatua za maendeleo,” amesema. Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo kwenye Ilani ya Uchaguzi ikiwemo ujenzi wa daraja la kuingia Kondo...