Skip to main content

Posts

Showing posts from April 17, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Samia Ameridhia Milioni 544 Ziletwe Bahi Kujenga Shule ya Sekondari Chifutuka - Prof. Shemdoe

Na OWM - TAMISEMI, Bahi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amesema Mhe. Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amemuarifu kuwa, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la wananchi wa Kata ya Chifutika lililowasilishwa na Mbunge wa Jimbo la Bahi Mhe. Kenneth Nollo la kupatiwa shilingi milioni 544 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Chifutuka ambayo itakidhi uhitaji wa wananchi wa kata hiyo.  Prof. Shemdoe amesema hayo leo Aprili 17, 2026 wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa darasa la nne, darasa la saba, kidato cha pili na kidato cha nne wilayani Bahi, iliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Chiona wilayani humo.  “Mhe. Mbunge alinifuata kabla sijasimama kuzungumza, akiomba shule ya sekondari ijengwe Kata ya Chifutika, nikawasiliana na Mhe. Waziri Mkuu na kuliwasilisha ombi hilo kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye...

Bulaya ni Vitendo sio Maneno

 Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Mhe. Ester Amos Bulaya, amekabidhi mashine ya kunakili nyaraka (photocopy machine) katika Shule ya Sekondari Nyamakokoto, ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa wanafunzi na walimu. Katika hafla hiyo, Mheshimiwa Mbunge aliambatana na Diwani wa Kata ya Nyamakokoto Mhe. Lucas Daniel Marco ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, Viongozi hao walisisitiza umuhimu wa vifaa vya kisasa katika kuinua kiwango cha elimu na kurahisisha upatikanaji wa nyaraka muhimu shuleni. Utoaji wa mashine hiyo unatarajiwa kusaidia kupunguza changamoto ya uchapishaji wa mitihani, nyaraka za kujifunzia pamoja na kazi mbalimbali za kiutawala shuleni hapo. *Imetolewa na:* *Ofisi ya Mbunge* *Jimbo la Bunda Mjini*

Prof. Shemdoe Atangaza Kibano Kwa Ma- Rc na Ma Dc Kuhusu Matumizi ya Magari

Na OWM - TAMISEMI, Bahi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini kutekeleza maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kupunguza matumizi ya mafuta kwa kutumia magari machache kwenye ziara za kikazi, huku akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule kwa kutumia gari moja katika ziara ya kikazi wilayani Bahi. Prof. Shemdoe ametoa maelekezo hayo leo Aprili 17, 2026 wakati wa kikao chake na viongozi wa mkoa  wa Dodoma na Wilaya ya Bahi kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bahi, kabla ya kuongoza hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa darasa la nne, darasa la saba, kidato cha pili na kidato cha nne iliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Chiona wilayani Bahi.  “Wakuu wa Mikoa na Wilaya muendelee kupunguza misafara yenu mnapokuwa kwenye ziara za kikazi kama ambavyo mmeona juzi Mhe...

Dkt. Kijaji Akutana na Maafisa na Askari wa Tanapa Makao Makuu Arusha

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) leo tarehe 17, Aprili 2026 amefanya kikao kazi na maafisa na askari wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Makao Makuu jijini Arusha katika ukumbi wa Phase II.  Akizungumza na watumishi hao, Waziri alielekeza changamoto mbalimbali za kiutendaji zinazokabili shughuli za uhifadhi na usimamizi wa rasilimali za taasisi zitatuliwe. Vilevile, ametoa maelekezo ya namna bora ya kushughulikia na kuzitatua changamoto hizo kwa ufanisi na kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa. Kwenye kikao hicho Mhe. Dkt. Kijaji aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas na Mkurugenzi wa Wanyamapori Dkt. Alexander Lobora huku akipokelewa na mwenyeji wake Kamishna wa Uhifadhi TANAPA CPA Musa Nassoro Kuji

Kipangula: Uandishi usiozingatia maadili unahatarisha umoja wa Kitaifa

Na Mwandishi Wetu Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema uandishi wa habari usiozingatia maadili unaweza kuhatarisha umoja wa kitaifa, amani na utulivu wa jamii. Akizungumza leo Ijumaa Aprili 17, 2026 jijini Dar es Salaam, Kipangula alisema waandishi wa habari wanapaswa kutambua uzito wa nafasi yao katika jamii, hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya kijamii, kisiasa na kiuchumi, ambapo taarifa wanazozitoa zina athari kubwa kwa mwenendo wa jamii. Alifafanua kuwa amani ni hali ya kutokuwepo kwa migogoro au vurugu, huku utulivu ukimaanisha usalama na uhakika wa maisha ya wananchi bila hofu, akibainisha kuwa hali hizi mbili haziwezi kudumu bila uwepo wa umoja wa kitaifa unaojengwa juu ya mshikamano wa wananchi bila kujali tofauti zao. “Pale ambapo uandishi hauzingatii maadili, unaweza kuchochea migawanyiko, kupotosha ukweli na hatimaye kuvuruga mshikamano wa kitaifa. Hivyo, ni muhimu kwa waandishi wa habari kutekeleza ...

Tpa Yawakutanisha Wadau wa Bandari Kavu

 NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM MENEJIMENTI ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imewakutanisha Wadau wa Bandari Kavu katika kikao kilicholenga kujadili changamoto,kupokea mawazo na kubadilisha panapohitajika ili kuongeza ufanisi katika uhudumiaji wa shehena. Kikao hicho kilichofanyika Alhamisi Aprili 16, 2026 Makao Makuu ya TPA kiliongozwa na Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano Dk.George Fasha ambaye katika hotuba yake ya ufunguzi alisema TPA inatambua umuhimu wa Bandari Kavu katika ufanisi wa shughuli za kibandari nchini. Aidha Dk. Fasha aliwataka washiriki wa kikao hicho kujadili kwa uwazi kuhusu maeneo yanayohitaji maboresho na ufanisi katika kuhamisha,kuhifadhi na kushughulikia shehena ndani na nje ya eneo la Bandari Kuu. Akizungumza kikaoni hapo,Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Bandari Kavu Nchini (CIDAT)Melickzed Kishange alisema vikao aina hii vina umuhimu mkubwa kwa wadau Bandari Kavu kwani ndio jukwaa litakalojadili na kutatua changamoto zitokanazo na shughul...

Watanzania Tuendelee Kudumisha Amani-Dkt. Mwigulu

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba ameendelea kuwasisitiza Watanzania waendelee kudumisha amani nchini kwa sababu inawawezesha kushiriki katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo. “Tuwe makini na watu wanaohamasisha uvunjifu wa amani kwa kuwa wengine walipwa kwa vitendo hivyo. Kama wao wamechagua maisha hayo wasiiuze nchi yetu. “Lazima tulinde amani ya nchi yetu.” Amesema wanufaika wa kwanza wa amani ni wale wanaoishi katika eneo husika, hivyo hawana budi kuendelea kulinda amani na umoja wa kitaifa ili waendeleze shughuli mbalimbali za maendeleo. Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Aprili 17, 2026) alipozungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kona ya Mbauda akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Arusha. Waziri Mkuu amesisitiza hayo mara baada ya kukagua barabara ya Kilombero-Mbauda-Kisongo na Mbauda Losinyai zinazojengwa kwa njia nne pamoja na kuwekewa taa. Ujenzi wa barabara hizo zenye jumla ya urefu wa kilomita 13 ni miongoni mwa maandalizi ya Mashindano ya Mpira wa Miguu ya M...

Katibu Tawala Mkoa wa Mara Afungua Mafunzo ya Kuwanoa Maafisa Elimu

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndugu Gerald Musabila Kusaya leo amefungua mafunzo ya mfumo wa kobotoolbox wa ukusanyaji wa takwimu kwa Maafisa Elimu wa Halmashauri zote tisa za Mkoa wa Mara yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda.  Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Kusaya amewataka washiriki kuzingatia mafunzo na kwenda kusimamia matumizi ya mfumo huo katika kuinua taaluma ya Mkoa wa Mara.  "Hali ya Taaluma inategemea takwimu sahihi, ambazo zitaonyesha hali halisi iliyopo na kuwezesha kutatua changamoto kama zipo" amesema Kusaya.  Ameushukuru Mradi wa Shule Bora kwa kufadhili mafunzo kwa Maafisa wa ngazi mbalimbali na hususan mafunzo ya ukusanyaji wa takwimu ambayo amesema yanasaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia na taaluma kwa ujumla.  Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndugu Ayoub Mbilinyi amesema mafunzo hayo yametokana na maelekezo ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara baada ya kupokea taarifa za m...