Skip to main content

Posts

Showing posts from December 23, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rc Mtambi Atakakia Kheri ya Krismas na Mwaka Mpya Wananchi Mkoa wa Mara

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Kanali Evans Alfred Mtambi, leo tarehe 24 Disemba, amewatakia heri ya Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya wananchi wa Mkoa wa Mara, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara. Mheshimiwa Mtambi amesema anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kuwajaalia Watanzania, ikiwemo wananchi wa Mkoa wa Mara, afya njema hadi kufikia mwisho wa mwaka na kipindi cha sikukuu.  Ameeleza kuwa kwa muda wote Mungu amekuwa karibu na Taifa kwa kulijalia amani na usalama, pamoja na fursa mbalimbali za kiuchumi zilizowawezesha wananchi kujipatia kipato kwa mwaka mzima. Hivyo, amewahimiza wananchi kutumia kipindi hiki cha sikukuu kumtukuza Mungu kwa kuwafikisha salama mwisho wa mwaka. Sambamba na hayo, Mheshimiwa Kanali Mtambi amewatoa hofu wananchi wa Mkoa wa Mara kwa kuwahakikishia kuwa mkoa uko salama, hivyo waendelee kusherehekea sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya kwa amani na utulivu. Amesisitiza umuhimu wa wananchi kulinda afya zao na...

Jaji Warioba Usiwagawe Watanzania Waunganishe

Na David Maphone. Nimemsikiliza kwa utulivu sana na umakini mkubwa mno Waziri Mkuu mstaafu Mheshimiwa Jaji Joseph Sinde Warrioba kwenye Video clips akihojiwa na Mharri Mkuu wa Gazeti la Jamhuri Tz, Ndugu Jackson M. Manyerere Kwamba, kwa Kitendo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba mara baada ya mazungumzo yao, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 17 Desemba, 2025.kilijenga matumani makubwa sana Mara baada ya kutoka taarifa hiyo. mamilioni ya Watanzania walifarijika sana kwa kudhani Kwamba Hekima na Busara za Jaji Warrioba na Mkuu wa nchi Rais Samia Suluhu Hassan kunaweza kuleta mshikamono maelewano ili kuliponya Taifa. Pamoja na kwamba Mhe, Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba alipewa heshima kubwa ya kuwa kiongozi mkubwa mstaafu wa mwanzo kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Samia mara baada ya kuapishwa kuwa Rais Novemba 03, 2025. Katika nyakati Taifa linahitaji upon...

Wachimbaji Wadogo Vijana 4000 Kupewa Leseni za Uchimbaji Madini Wilayani Bukombe

■ Ni maelekezo ya Rais.Dkt.Samia Suluhu Hassan  ■ Maeneo ya utafiti yasiondelezwa kufutwa na kugawiwa kwa vikundi  ya vijana na wanawake kupitia Programu ya MBT. ■ Waziri Mavunde asisitiza kila Mtanzania ana haki ya kumiliki leseni ya uchimbaji madini. ▪️Aelekeza ofisi ya Madini Mkoa kutatua changamoto ya migao ya madini *Bukombe, Geita* Serikali kupitia Wizara ya Madini chini ya utekelezaji wa Programu ya Mining for A Brighter Tommorow (MBT) imeweka utaratibu mzuri na kugawa leseni kwa vikundi vya wachimbaji wadogo wanawake na vijana takribani 4000 kwa ajili ya shughuli  za uchimbaji. Hayo yameelezwa leo Desemba 23, 2025 na Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara na wachimbaji katika machimbo ya Msasa, Wilayani Bukombe. "*Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan* ametuelekeza kuhakikisha tunawasimamia na kuwapanga wachimbaji wadogo ikiwa ni pamoja na kuwapatia maeneo ya uchimbaji ili kurasimisha shughuli zao. "Na ndiyo maana sis...

Serikali Kutatua Changamoto Zinazowakabili Vijana Nchini

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana amesema Serikali inalenga kuwa na kampuni zaidi ya laki moja hadi kufikia miaka mitano ijayo ambapo lengo likiwa ni kuongeza idadi kubwa ya wawekezaji vijana pamoja na soko la uzalishaji la ndani ya ili kuepuka kutegemea masoko ya nje. Akizungumza mapema hii leo Disemba 23, 2025, Waziri Joel Nanauka, katika kikao kazi cha mawaziri kilichoandaliwa na ofisi ya idara ya habari maelezo na kufanyika katika kituo cha urithi wa ukombozi jijini dar es salaam ambapo pia amesema matarajio ya serikali ni kuona zaidi ya ajira milioni moja zinazalishwa. Aidha, Waziri Nanauka amesema kuwa serikali imebaini kuwa katika idadi kuwa ya vijana waliofanikiwa kupatiwa mikopo wamekosa elimu ya malezi katika uwajibikaji wa biashara mbalimbali kupitia mikopo hiyo, hivyo serikali inalenga kuja na programu ya malezi itakayoweza kuwasaidia vijana kuepukana na changamoto ya kupoteza mitaji yao. Hata hivyo, Waziri Nanauka ameongeza kuwa serikali imeanza mc...

Rais Samia akutana na Waziri Mkuu Mwigulu Ikulu Zanzibar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Ikulu ndogo Tunguu, Zanzibar, tarehe 23 Desemba, 2025.

Serikali yasisitiza usalama,mapato mpakani Mutukula

Na Mwandishi Wetu,KAGERA Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene amehimiza ushirikiano kati ya  watumishi wa serikali waliopo katika Kituo cha Forodha cha Pamoja cha Mutukula kilichopo wilayani Misenyi mkoani Kagera ambapo ni mpaka kati ya nchi ya Tanzania na Uganda huku akiwaasa kutilia mkazo masuala ya usalama na ukusanyaji wa mapato kwa maendeleo ya nchi ambapo uhitaji wa usalama na mapato ni muhimu ili nchi iweze kukua kiuchumi. Ametoa rai hiyo wakati wa ziara ya ukaguzi wa shughuli mbalimbali za kiforodha katika kituo hicho  akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Kagera ambapo awali alipowasili mkoani humo alipata ripoti ya hali ya ulinzi na usalama kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Hajjat Fatma Mwassa,ripoti iliyoonyesha kuwepo kwa sintofahamu katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo ikiwemo wingi wa vipenyo vinavyotumiwa na wahamiaji haramu na watu wanaoweza kuingia nchini kwa nia ovu ya kuvuruga amani iliyopo. ‘Kwanza ni usalama wa nchi yetu, kw...