Skip to main content

Posts

Showing posts from October 5, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Naibu waziri mkuu Biteko aipongeza wizara ya madini kwa mpango wa kuongeza akiba ya dhahabu nchini

📍 Bombambili,Geita Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Doto Mashaka Biteko ameipongeza Wizara ya Madini kwa mkakati wanaoutekeleza ambao unawazesha upatikanaji wa  akiba ya Dhahabu  kupitia Benki kuu ya Tanzania jambo ambalo ni muhimu kwa maendeleo ya Uchumi wa Tanzania. Hayo yamesemwa jana Oktoba 05 2024 wakati wa ufunguzi wa maonesho ya saba ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yenye kauli mbiu ya “Matumizi ya Teknolojia sahihi ya Nishati safi  katika sekta ya Madini kwa maendeleo endelevu” yanayofanyika Mkoani Geita.  “Sisi utajiri ambao Mungu ametujaalia ni utajiri wa madini ikiwemo Dhahabu, lazima madini haya yawe chachu katika ukuaji wa uchumi wetu. Naipongeza Wizara ya Madini kwa bidii kubwa mlioifanya sasa ya kuanzisha na kusukuma uwepo wa akiba ya Dhahabu kupitia Benki kuu ya Tanzania”, alisema Mh. Biteko.  Kwa upande wake Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde ameeleza kwamba kwa sasa baada ya kukaa pamoja baina ya serikali na wadau wamefikia mua...

Wananchi Kagera Watakiwa Kutumia Elimu ya Watu Wazima Kujiendeleza na Kujifunza Stadi za Maisha

  Na Angela Sebastian-Bukoba Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa ametoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kutumia fursa inayotolewa na Serikali ambayo ni hupatikanaji wa  elimu kwa watu wazima na nje ya mfumo rasmi ili kujiendeleza na kupata kujua stadi za maisha zitakazowasaidia kuwepo  na jamii ya watu walioelimika. Katika taarifa iliyosomwa na Afisa elimu wa mkoa wa Kagera  Michael Ligola akisoma risala ya kufunga maadhimisho ya kilele cha wiki ya elimu ya watu wazima kwa niaba mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Mwassa jana ,katika viwanja vya mji mdogo wa Kayanga Wilaya Karagwe ambapo alisema kuwa maadhimisho hayo ni utekelezaji wa sera ya elimu.  "Sera hiyo iliaksi malengo yaliyoko katika dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 1925 na malengo endelevu ya dunia (SDG)  ambapo moja ya lengo la dira  ya mwaka 2025 ni kuhakikisha kuwa Tanzania ifikapo 2025 inakuwa na watu waliosoma na jamii iliyoelimika sambamba malengo endelevu ya dunia yanayosema elimu kwa ...

Nataka musoma ya kazi,mazoezi, michezo na bata;Dc Chikoka

Na Shomari Binda-Musoma Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amesema anataka Musoma iwe ya kufanya kazi,mazoezi na michezo na kupata burudani ya starehe. Kauli hiyo ameitoa leo oktoba 5 kwenye bonanza kubwa la michezo mbalimbali lililofanyika kwenye uwanja wa Posta. Amesema anataka kuiona Musoma iliyochangamka kwa watu wake kufanya kazi kwa bidii awe mtumishi wa umma au binafsi na baadae kushiriki mazoezi ,michezo na starehe" kula bata". Chikoka amesema bila kuwa na afya njema mtu awezi kufanya kazi na kushiriki mazoezi na michezo kunafanya mwili kuchangamka. Mkuu huyo wa Wilaya amesema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imempendeza kumleta Musoma na anataka Wilaya ichangamke kwa kufanya kazi,mazoezi na matukio ya kimichezo ya mara kwa mara. " Leo tumekutana kwenye bonanza letu hili ikiwa ni katika kuweka mwili sawa na hii sio mwisho bali itakuwa endelevu. " Nimeshukuru kuona Kata zote 16 wakiwemo wanawake,wanaume kwa vijana wamejitokeza kushiriki bonanza hili na nimefar...

Rais Samia kutimiza ndoto ya hayati baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

 Na NIRC;Korogwe, Tanga Waziri wa Kilimo Hussein Bashe  ametangaza neema katika mradi wa Umwagiliaji Mkomazi uliopo Korogwe mkoani Tanga na kusema ndoto ya Mwalimu Julius Nyerere inatimizwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan. Akizungumza mara baada ya kukagua miradi ya Umwagiliaji Mkoani Tanga, Waziri Bashe ametangaza neema ya kukamilishwa miradi yote ya umwagiliaji. Amesema, miradi hiyo ya umwagiliaji ukiwemo mradi mkubwa wa Mkomazi wenye gharama zaidi ya bilioni 18.2 ni ndoto ya Mwalimu Julius Nyerere inayotimizwa serikali ya awamu ya sita, chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan Amesema bwawa hilo litahifadhi maji mita za ujazo bilioni 17.5. Bashe ameongeza kuwa azma ya serikali kutekeleza miradi ya Umwagiliaji katika Bonde la Mkomazi, wilaya ya Korogwe, Mkoa wa Tanga kutawasaidia wananchi kuondokana na Umasikini wa kipato na kuchangia katika pato la taifa  “Hatua inayochukuliwa na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, imetatua changamoto ya muda mrefu ya utekeleza...

Waziri Mkuu aagiza Mkurugenzi Mkuu wa Nemc kwenda Temeke Jumatatu

Waziri mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa amemuagiza  Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) aende mara moja Wilaya ya Temeke na kutembelea viwanda vinavyolalimikiwa kutiririsha maji kwenye makazi ya watu na barabara. Mh Waziri mkuu,ametoa agizo hilo leo jumamosi Oktoba 05,2024 wakati akihutubia wa Temeke eneo la Mbagala Kizuiani  siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Dar es salaam. Amesema amepata malalamiko mengi ya wananchi kuhusu baadhi ya viwanda kutiririsha maji kwenda kwenye makazi ya watu na maeneo yasiyostahili hivyo kumtaka Mkurugenzi huyo wa NEMC  kufika wilayani Temeke jumatatu  ya Oktoba 07 ili aweze kutembelea maeneo hayo na kuchukua hatua za kutatua kero hiyo  kwa wananchi. Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye sekta zote ikiwemo Afya, Maji, Elimu na Miundombinu ya Barabara. ...

WAZIRI MKUU AAGIZA MKURUGENZI MKUU WA NEMC KWENDA TEMEKE JUMATATU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye sekta zote ikiwemo Afya, Maji, Elimu na Miundombinu ya Barabara. Amesema hayo leo (Jumamosi, Oktoba 05, 2024) alipozungumza na wakazi wa Mbagala Kizuiani, Temeke jijini Dar es Salaam ambapo yupo kwenye ziara ya kikazi. Amesema kuwa Serikali ipo imara na imedhamiria kuendelea kuwatumikia watanzania wote. “Niwahakikishie kuwa Rais wetu Dkt. Samia yupo imara na anaupendo kwa Watanzania, dhamira, mipango na mienendo yake ya utawala ipo safi”. Katika hatua nyungine, Mheshimiwa Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) aende Wilaya ya Temeke na kutembelea viwanda vinavyolalimikiwa kutiririsha maji kwenye makazi ya watu na barabara. Aidha, amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Ndg. Jomaary Satura kuhakikisha anatumia fedha za mapato ya ndani kuweka taa za barabarani katika maeneo yo...

Waziri Mkuu atoa onyo kwa wanaokwamisha elimu kwa mtoto wa kike

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa onyo kali kwa wale wote wajihusha na vitendo vya kukatisha masomo watoto kwa kike na kusema kuwa serikali ya awamu ya sita imeweka mikakati mbalimbali ya kumlinda mtoto wa kike, ikiwa ni pamoja na kutunga sheria kali dhidi ya watu hao. Waziri mkuu ametoa kauli hiyo Oktoba 05,2024 wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam baada ya kuzindua jengo la bweni kwa ajili ya wanafunzi wa kike likiwemo jengo bwalo la chakuka katika shule ya Sekondari ya Kibasila. Amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan,imetoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya sekta ya elimu ukiwemo ujenzi wa mabweni hayo ili kusaidia watoto wa kike,wakiwemo wa kiume kupata elimu bora na ya uhakika. Amesema haiwezekani serikali iwezekeze fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya elimu kisha juhudi hizo zikahujumiwa na baadhi ya watu wachache kwa kujihusisha na vitendo vinavyoweza kukatisha elimu kwa mtoto wa kike. Kwa sababu hiyo mh waziri mkuu,amesem...

Naibu Waziri Mkuu apongeza Tume ya Madini kwa ukusanyaji wa maduhuli

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amepongeza Tume ya Madini kwa kuendelea kuvuka lengo la ukusanyaji wa maduhuli na kusisitiza kuendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha wanavuka lengo walilopewa na Serikali la kukusanya kiasi cha shilingi Trilioni Moja katika mwaka wa fedha 2024/2025. Dkt. Biteko ameyasema hayo leo Oktoba 05, 2024 alipotembelea banda la Wizara ya Madini na Taasisi zake akiwa ameambatana na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde katika Maonesho ya Saba ya Kitaifa ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini Geita yaliyoanza Oktoba 2, kwenye viwanja vya Bombambili mkoani Geita. "Mnafanya kazi nzuri sana Tume ya Madini, lengo mlilopewa ni kukusanya Shilingi Trilioni Moja katika mwaka wa fedha 2024/2025, naamini mtalivuka," amesema Dkt. Biteko. Taasisi nyingine chini ya Wizara ya Madini zinazoshiriki katika maonesho ni pamoja na Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia ( TEITI), Taas...