Tanzania imepongezwa kwa utendaji mzuri wa kushughulikia changamoto za kiusalama katika kanda ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), baada ya kuwa Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Pongezi hizo zimetolewa Agosti 15, 2025, wakati wa Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama unaofanyika Madagascar chini ya mwenyekiti wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo. Katika hotuba yake ya ufunguzi, Balozi Kombo alisema katika uenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama, Tanzania iliongoza juhudi za pamoja za kutafuta ufumbuzi wa migogoro ya kikanda, kuimarisha utawala wa kidemokrasia na kuimarisha miongozo ya kulinda amani. Hayo yalifanyika chini ya uongozi imara wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama. Katika kipindi cha mwaka mmoja, Tanzania iliitisha mikutano mitano ya dharur...
Marato tv - Sauti ya Jamii