Skip to main content

Posts

Showing posts from September 2, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

CCM Mara Yaridhishwa na Utendaji Kazi wa Tanroads Mkoa Katika Utekelezaji na Usimamizi wa Miradi ya Barabara

  Na Shomari Binda-Musoma  CHAMA cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mara kimedai kuridhishwa na utendaji kazi, utekelezaji na ufatiliaji miradi ya barabara inayofanywa na Wakala wa Barabara Tanroads mkoa wa Mara. Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa CCM mkoa wa Mara Ibrahim Mjanakheri  alipokuwa akizungumza na George Marato TV kwenye mahojiano maalum yaliyofanyika ofisini kwake. Amesema serikali ya awamu ya Sita chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan, imefanya kazi kubwa kuleta fedha za miradi ya maendeleo na mkoa wa Mara umenufaika. Katibu huyo amesema eneo la miundombinu ikiwemo ya barabara imepata fedha na Tanrods mkoa wa Mara imefanya kazi nzuri katika kusimamia na miradi inaendelea vizuri. Amesema katika kipindi cha mvua barabara zote zilikuwa zikipitika na hakuna taarifa yoyote iliyolipotiwa ya barabara kushindwa kupitika kwa kukatika Mjanakheri amesema hali hiyo ni kuonyesha Tanrods mkoa wa Mara inatekeleza vizuri majukumu yake kupitia usimamizi wa meneja wa mkoa mhandisi Vedastus M...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

KURA TATU ZA MNG'ARISHA ELIZABERTH GRWFA

Chama cha Mpira wa Miguu cha Wanawake Mkoa wa Geita (GRWFA) kimefanya uchaguzi wa viongozi wapya ambao watahudumu kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Uchaguzi huo umefanyika katika ofisi za chama hicho, chini ya usimamizi wa Wakili Mark Chota. Katika uchaguzi huo, Elizaberth Makwenda amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa GRWFA baada ya kupata kura 3, huku mpinzani wake, Veronica Samo, ambaye alikuwa akitetea kiti hicho, akipata kura 1 pekee. Matokeo hayo yalitangazwa na msimamizi wa uchaguzi, Wakili Mark Chota, mbele ya wajumbe wanne ambao walipiga kura. “Nataka kutangaza kwamba Elizaberth Makwenda ndiye mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Soka la Wanawake Mkoa wa Geita kwa kura 3 dhidi ya 1 aliyopata Veronica Samo.” Alisema Mark Chota - Msimamizi wa Uchaguzi Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Geita, Salum Kulunge, aliwataka viongozi wapya kuwa wamoja na kuvunja makundi yote yaliyokuwepo wakati wa kampeni ili kuleta mshikamano na maendeleo katika soka la wanawake mkoani humo....

WAUMINI WAMZAWADIA KATEKISTER PIKIPIKI

Waumini wa Kigango Cha Mt. Petro Masawe Parokia ya Misungwi wakishikiana na Wafadhili wamemzawadia Katekister Elias Kabipe Zawadi ya Pikpikipi katika Sherehe ya Somo wa Makatekster Mt.Yakobo Mwaka 2024 iliyofanyika Tarehe 31/8/2024 Kigango cha Mt.Petro Masawe Parokia ya Misungwi iliyotanguliwa na adhimisho la Misa Takatifu. Akizungumza katika Sherehe hizo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Walei Kigango Cha Mt.Petro Masawe Be.Thomas Lutego ameeleza kwamba Waumini hao kwa kushirikiana na Wadau na Wafadhili wameamua kumpatia Pikipiki Aina ya San LG 125 yenye thamani ya shilingi 2,350,000/= ili kumsaidia kutoa huduma ya Utume kwa Waumini kwa urahisi zaidi kwenye Jumuiya ndogo ndogo saba za Kigango hicho zenye Waumini zaidi ya 300. Kwa upande wake Paroko Msaidizi wa Parokia ya Misungwi Padri William Leba amewapongeza Waumini hao na kuwasihi kuendeleza Umoja na ushirikiano ili kuendeleza kumtukuza Mungu na kuongeza juhudi ya Kazi na uwajibikaji katika Kanisa Katoliki.

HATIMAYE RELI YA TAZARA KUFANYIWA UKARABATI MKUBWA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh Dr Samia Suluhu Hassan, anatarajia kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya watu wa China mh Xi Jinping yanayolenga kuimarisha uhusiano mzuri na ya kihistoria kwa mataifa haya mawili ulioasisiwa miaka 60 iliyopita. Rais Samia ambaye ananza ziara ya kikazi nchini China kuanzia Agosti 2 hadi Agosti 06 pamoja na mwenyeji wake Rais wa China,wataungana na Rais Jamhuri ya Zambia Mh Hakainde Hichilema watashiriki na kushuhudia uwekaji saini wa Hati za makubaliano ya uboreshaji wa Reli ya TAZARA. Rais Samia pia anatarajia kushiriki mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika(Forum on China-Africa Cooperation-FOCAC)utakaofanyika jijini Beijing Akiwa nchini China Rais Samia atakaohutubia ufunguzi mkutano wa FOCAC kwa niaba ya kanda ya afrika mashariki.

MIRADI YA MAJI 1,342 KUTEKELEZWA MJINI NA VIJIJINI

  SERIKALI imesema inaendelea na utekelezaji wa miradi ya maji katika maeneo mbalimbali nchini, ambapo kupitia bajeti ya 2024/2025 jumla ya miradi 1,095 inatarajiwa kutekelezwa vijijini na miradi 247 mijini.  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew leo Septemba 2, 2024 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi Noah Saputu aliyeuliza Serikali ina mkakati gani mahsusi wa kukamilisha miradi ya maji mikubwa na midogo nchini. Mhandisi Kundo amesema Miradi hiyo inatekelezwa ili kufikia malengo ya Serikali ya kufikisha huduma ya majisafi na salama kwa asilimia 85 vijijini na 95 mijini ifikapo mwaka 2025/26.  "Mheshimiwa Spika; nia ya Serikali ni kuhakisha miradi ya maji yote mikubwa na midogo iliyopangwa kutekelezwa na inayoendelea na utekelezaji nchini inakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma iliyokusudiwa kwa wananchi" "Mkakati mahususi wa Serikali ni kuhakikisha inepeleka fedha zinazohitajika kwenye utekel...