Skip to main content

Posts

Showing posts from June 1, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Matunda Mazuri ya Uvuvi wa Vizimba yaanza Kuonekana Musoma Vijijini

  Jimbo la Musoma Vijijini lenye jumla ya Kata 21, lina Kata 18 zilizoko pembezoni mwa Ziwa Victoria. Kwa hiyo, uvuvi ni kazi inayoajiri watu wengi wa Jimboni mwetu. Wataalamu wa uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wakiwemo wa TAFIRI, walishirikiana na NEMC kubaini maeneo mazuri yanayokidhi vigezo vya kufanya uvuvi wa vizimba ndani ya Jimbo letu. Mbali ya mikopo nafuu iliyotelewa na Serikali yetu kwenye uvuvi wa vizimba, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo anaendelea kuwashawishi wavuvi wa Jimboni mwetu kwenda Benki za CRDB na NMB kuchukua mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya uvuvi wa vizimba. Mbunge huyo ameishawasiliana na Benki hizo mbili kuhusu mikopo hiyo. *Matunda mazuri yaanza kuonekana:* Wavuvi wa Jimbo la Musoma Vijijini wameanza kupata matunda mazuri kutokana na uvuvi wa samaki kwa kutumia vizimba. Mvuvi mmoja (pichani) wa Kijijini Kigera, Kitongoji cha Kurukiri anavuna samaki takribani Tani 40 kutoka kwenye vizimba vyake 4 vyenye upenyo wa mita ...

Waziri Mkuu Amwakilisha Rais Samia Katika Tuzo za Wanamichezo

  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Juni 01, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika tuzo za wanamichezo waliofanya vizuri katika mashindano ya kimataifa zinazoandaliwa na Baraza la Michezo Taifa. Lengo la tuzo hizo ambazo zimetolewa katika ukumbi wa Superdome Masaki, Jijini Dar es Salaam ni kuwaenzi na kuwatambua watanzania wanaiowakilisha nchi katika michezo mbalimbali duniani na kuiletea sifa Tanzania kwa maslahi yao na Taifa kwa ujumla. Akizungumza Katika hafla hiyo, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali ya awamu ya Sita itaendelea kuwekeza katika sekta ya michezo kwa kuwa inatambua michezo ni afya, ajira, mshikamano, maendeleo lakini pia michezo ni burudani.  Katika hafla hiyo Mheshimiwa Majaliwa alipokea kwa niaba ya Rais Dkt. Samia tuzo ya kutambua mchango wake katika kukuza na kuendeleza sekta ya michezo nchini. Aidha, Mheshimiwa Majaliwa pia alikabidhiwa tuzo ya kutambua mchango wake katika kusimamia michezo nchini.

Kikwete na Balozi wa China wajadiliana ukuzaji ujuzi wa vijana na maendeleo

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China , Balozi Chen Mingjian na Ujumbe wake Ofisini kwake Dodoma.  Majadiliano hayo yalilenga kujadili mambo mengi ya ushirikiano baina ya Tanzania na China hasa katika maeneo ya ukuzaji ujuzi, maendeleo na mabadilko ya teknolojia duniani n.k Kikwete amewahakikishia kuwa Tanzania itaendelea kuenzi uhusiano uliopo baina ya nchi zetu hizi na kuwa Tanzania itaendeleza uhusiano huu kwa kuimarisha maeneo yote ambayo yanakutanisha katika mashirikiano haya. Pia kuwashukuru serikali ya China kwa mabadiliko makubwa ambayo yanaelekea kukuza ujuzi kwa vijana wa Kitanzania na nia yao ya kufanya maonyesho makubwa ya kazi yanayolenga kufunua fursa za vijana wa kitanzania kujiajiri na kufungua milango ya kuajiriwa na makampuni makubwa ya kigeni yakiwemo ya China nchini hapa. 

CCM inavyoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu ikiwa na mtaji mkubwa wa wapigakura.

  Na: Dk. Reubeni Lumbagala, Tanga Kwa mwaka huu wa 2025, moja ya tukio kubwa kabisa katika kalenda ya nchi yetu ni uwepo wa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba, 2025. Hili ni tukio la kidemokrasia na la kikatiba ambapo Watanzania wanapata fursa ya kutimiza haki yao ya kisheria na kikatiba ya kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani watakaowaongoza katika kipindi cha miaka mitano ijayo yaani 2025-2030. Kwa kuzingatia kuwa lengo la kwanza la chama chochote cha kiasi ni kushinda uchaguzi ili kushika dola, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wake kimejizatiti si tu kushiriki katika Uchaguzi Mkuu lakini pia kushinda kwa kishindo kikubwa.  Pamoja na sera nzuri ambazo CCM inazo, lakini uwekezaji mkubwa umefanyika wa kusajili wanachama kwa njia ya kieletroniki ili kuwa na uhakika wa ushindi ikizingatiwa watu ni mtaji muhimu wa kufanikisha ushindi. Mei 29, 2025, jijini Dodoma kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa CCM, Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Tanzania Dk. Samia...

CCM yampongeza Rais Samia kwa kupewa Tuzo na Bunge