Skip to main content

Posts

Showing posts from May 30, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

WAZIRI MAVUNDE ATOA WITO WAMILIKI WOTE WA LESENI ZA UCHIMBAJI WA MADINI KINYWE KUANZA SHUGHULI ZA UCHIMBAJI MARA MOJA

■ Lengo ni kuifanya Tanzania kuwa kinara wa uzalishaji wa madini kinywe ifikapo Mwaka 2030 ■ Serikali yasaini mkataba wa ubia na  Kampuni za Grafica na Eminent. ■ Aitaka Timu ya majadiliano ya serikali kuanza mchakato wa majadiliano na Wamiliki wa Leseni 27 ■ Amshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha sekta ya madini, ■ Ruangwa kuwa sehemu ya mnyororo wa thamani na teknolojia ya madini kinywe duniani. *Ruangwa, Lindi* Waziri wa Madini, *Mheshimiwa Anthony Mavunde (Mb)* ameielekeza Timu ya Majadiliano ya Serikali kwenye Sekta ya Madini (GNT) kuwaita na kufanya nao majadiliano wamiliki wote wa leseni za uchimbaji madini kinywe nchini Tanzania kujadiliana kuhusu ubia wa serikali katika Kampuni hizo na kuwataka kuanza utekelezaji wa uchimbaji kwa mujibu wa masharti ya leseni na Sheria ya Madini Sura ya 123. Ameyasema hayo leo tarehe 30 Mei, 2026 Wilayani Ruangwa aliposhiriki zoezi la utiaji saini na Kampuni za Grafica Resources na Eminent Minerals Limited zenye ubia wa...

DKT. MWIGULU AAGIZA WALIOIBA MILIONI 500 MANYONI KUKAMATWA

*_▪︎ Aagiza watumishi waliohusika na ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni 500 Manyoni wakamatwe na fedha zirudishwe_* *_▪︎ Akemea rushwa, wizi wa fedha za umma na matumizi mabaya ya madaraka_* *_▪︎ Aonya viongozi wanaowaza vyeo badala ya kutatua changamoto za wananchi_* WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba ameagiza watumishi waliohusishwa na ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni 500 katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni watafutwe popote walipo, wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria na kinidhamu huku fedha hizo zikirejeshwa serikalini. "Wamechota fedha za wananchi. Watafutwe hata ambao walishahamishwa, popote walipo wakamatwe, wawekwe ndani na fedha za Serikali zirudi. Hii si fedha ya mtu binafsi, ni fedha ya wananchi," alisema Dkt. Mwigulu. Dkt. Mwigulu ametoa agizo hilo leo Jumamosi Mei 30, 2026 alipozungumza na wananchi wa Wilaya ya Manyoni katika Viwanja vya Tambukareli mkoani Singida akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kusi...

SKIMU ZA UMWAGILIAJI ZINAVYOPELEKA FURAHA KWA WAKULIMA MBARALI

Wakulima wa zao la mpunga wilayani Mbarali Mkoa wa Mbeya wameiomba Serikali kuendelea na utekelezaji wa miradi 10 ya skimu za umwagiliaji inayotekelezwa wilayani humo, wakisema tayari imeanza kuleta matokeo chanya katika uzalishaji wa mazao. Wakulima hao wanasema licha ya miradi hiyo kutokukamilika kwa asilimia zote, uzalishaji wa mpunga umeongezeka kwa zaidi ya asilimia 80 kutokana na upatikanaji wa uhakika wa maji. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakulima hao wameridhishwa na ongezeko la mavuno katika msimu huu na kubainisha kuwa miradi ya Umwagiliaji imekuwa chachu ya maendeleo ya kilimo katika wilaya hiyo. Meneja wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mkoa wa Mbeya, mhandisi Banzi Abdallah amesema utekelezaji wa miradi hiyo umefikia asilimia 60 na kwamba hatua mbalimbali zinaendelea kuhakikisha inakamilika kwa wakati ili kuwanufaisha wakulima wengi zaidi. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Raymond Mweli amesema skimu za Umwagiliaji zina mchango mkubwa katika...

WAZIRI MKUU APONGEZA KILIMO CHA KOROSHO MANYONI, AHIMIZA UONGEZAJI THAMANI WA MAZAO KUPITIA VIWANDA

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imeweka mazingira wezeshi kwa ajili ya kukuza uchumi wa viwanda na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, huku akiwataka vijana, sekta binafsi na wawekezaji kutumia fursa zilizopo kuanzisha viwanda vya kuchakata korosho na mazao mengine ya kilimo. “Serikali haipaswi kufanya jukumu hilo peke yake la kujenga viwanda. Lakini kwa kuwa zao hili halikuwa zao la asili lililozoeleka kwa Mkoa wa Singida, ni lazima hatua za aina hii ziweze kufanyika. Baada ya hapo vijana na sekta binafsi wachukue jukumu hilo la kutengeneza viwanda vya kutosha vya kubangua korosho zinazozalishwa hapa Mkoa wa Singida na pengine hata mikoa mingine,” alisema Dkt. Mwigulu. Dkt. Mwigulu amesema hayo leo Jumamosi Mei 30, 2026 alipokagua Mradi wa Mnyororo wa Thamani wa Korosho kupitia Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho (KIDAKUKO) cha CAMARTEC kilichopo Masigati wilayani Manyoni, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Singida. Waziri Mkuu aliwapongeza wananchi wa Manyoni kwa...

WALIOBOMOLEWA NYUMBA, MWANAFA AWAAHIDI WATALIPWA FIDIA

📍 Ni zile familia 67 zilizobomolewa nyumba na Amboni Plantation  Na Mwandishi Wetu, Kigombe MBUNGE wa Muheza, Mhe. Hamis Mwinjuma (MwanaFA), amewahakikishia wananchi wa kaya 67 waliobomolewa nyumba zao na Kampuni ya Amboni Plantation kuwa watalipwa fidia zao kikamilifu. Uharibifu huo wa dharura ulioacha familia hizo za Kitongoji cha Maisha Plus mkoani Tanga zikilala nje, ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kwa madai ya wananchi hao kuvamia eneo la shamba la mkonge la mwekezaji huyo. Akizungumza jana Mei 29, 2026 aliporejea kijijini hapo kutoa mrejesho wa kikao chake cha ndani na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian, MwanaFA alisema Serikali imejipanga vizuri kulinda utu wa wanyonge hao. "Sitaki kuwaambia ni kiasi gani mtalipwa, lakini sisi kama viongozi wenu tunawahakikishia jambo lenu litakwenda vizuri na mtalipwa fidia kabla ya kuondoka hapa. Suala hili linanikosesha usingizi na sitarudi kwenye majukumu ya kitaifa hadi dharura hii iishe," alisema MwanaFA. M...