Skip to main content

Posts

Showing posts from April 3, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mavunde Azindua Rasmi Shughuli Za Uchimbaji Madini Porcupine North- Chunya Mbeya

▪️Ni Leseni Hodhi zilizorudi Serikalini baada ya kumalizika kesi na wawekezaji ▪️Mapato ya Serikali kuongezeka kupitia mrabaha na kodi mbalimbali ▪️ Waziri Mavunde asisitiza kuongeza utafiti zaidi ili kuongeza uzalishaji wa dhahabu ▪️Wachimbaji wadogo nao wapatiwa Leseni kuongeza uzalishaji 📍 *Chunya- Mbeya* Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amezindua rasmi shughuli za uchimbaji madini katika mgodi wa Porcupine North- uliopo Makongorosi Wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya unaomilikiwa na Kampuni ya Shanta Gold Mining Limited na kusema kuwa hatua hiyo ni matunda ya uamuzi wa Serikali kurudisha leseni ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha unawekwa utaratibu mzuri wa kuongeza mapato ya nchi kupitia sekta ya madini. Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Aprili 03, 2025 katika hafla ya Uzinduzi wa Shughuli za Uchimbaji Madini Porcupine North – Kata ya Mkola, Makongorosi Wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya. “Eneo hili ni eneo ambalo Leseni hodhi zimerudi se...

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Wa Serikali Zaingia Makubaliano na Baraza la Taifa la Ujenzi

 Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Baraza la Taifa la Ujenzi zimeingia makubaliano kwa ajili ya ushirikiano wa kitaalamu katika Sekta ya Ujenzi. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini, Dar es Salaam tarehe 03 Aprili, 2025 Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari amesema kuwa wameingia makubaliano hayo kwa sababu taasisi hizo zinashabihiana kwenye suala la ujenzi na hasa katika miradi mikubwa ya kimkakati. Amesema kupitia makubaliano hayo wanatarajia kuboresha zaidi kwa ujuzi na umahiri wao katika mikataba ya ujenzi. “Tumeshuhudia Serikali ya Awamu ya Sita ikiendelea na jitihada zake za kufanya miradi mikubwa na ya kimkakati ya ujenzi, kwa hiyo sisi kama wanasheria, wataalamu wa ujenzi tunatakiwa kuhakikisha kwamba tunakuwa na ujuzi na utaalamu stahiki kuhakikisha miradi hii ya ujenzi mikubwa inafanyika vizuri na mikataba inaandaliwa na kutekelezwa vizuri, pia usimamizi wake unakuwa mzuri,” amesema Mhe. Johari Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameeleza kuwa ...

Balozi Dkt Nchimbi Atikisa Namtumbo

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza na umati mkubwa wa wananchi Namtumbo, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Namtumbo, leo Alhamis tarehe 3 Aprili 2025.  Katika mkutano huo, viongozi wa vyama vya ACT Wazalendo na Chadema, wakiwaongoza wanachama wao, waliamua kurejesha kadi na vifaa vingine vya vyama hivyo, kisha wakajiunga CCM. Viongozi hao, akiwemo Ndugu Alifa Jafa, Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Songea, Ndugu Mohamed Said Ndauka, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ntungwe na Azarius Lucas Ngonyani, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Miembeni, walieleza jinsi ambavyo uongozi wa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuteuliwa kwa Balozi Nchimbi kuwa mgombea mwenza wa Urais, kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2025, umewavutia kuhamia CCM.

Diwani Gumbo Aelezea Namna Kituo Cha Afya Makoko Kilivyowasaidia Wananchi

Na Shomari Binda-Musoma  DIWANI wa Kata ya Makoko na Meya wa manispaa ya Musoma Patrick Gumbo ameelezea namna kituo cha afya kilichojengwa kwenye Kata hiyo kilivyosaidia utoaji huduma za afya. Akizungumza na GMTV kuhusiana na huduma za kijamii ndani ya Kata hiyo zinavyotolewa zikiwemo za afya amesema hawana shida juu ya upatikanaji na utoaji huduma hizo baada ya kupata kituo hicho. Amesema huduma muhimu za mama na mtoto  zinazotolewa kwenye kituo hicho kwa ufanisi mkubwa zikiwemo huduma nyingine za kulazwa wagonjwa. Gumbo amesema wananchi wa Kata ya Makoko na maeneo jirani ya kituo hicho wanapata huduma na kuepuka kwenda kwenye hospitali ya manispaa au hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. " Kituo hiki cha afya kimekuwa msaada kwa wananchi ndani ya Kata na majirani zetu wanao tuzunguka wakiwemo hadi wa Musoma vijijini. " Tunaishukuru sana serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha za ujenzi wa kituo hiki cha afya ambacho sasa kinato...

JWTZ lajivunia Ushirikiano na Jeshi la Ujerumani

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  Nchini Jenerali Jacob John Mkunda amekabidhiwa Rasmi Hospitali ya Daraja la  Nne ya viwango vya Umoja wa Mataifa iliyojengwa kwa Ushirikiano wa Serikali  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya  Shirikisho la Ujerumani  leo tarehe 03 Aprili 2025  Msalato Jijini Dodoma. Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Jenerali Mkunda ameishukuru Serikali ya  Shirikisho la Ujerumani kupitia Jeshi la Nchi hiyo kwa namna linavyoshirikiana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika nyanja mbalimbali kama vile Mafunzo, Mazoezi pamoja na Ujenzi wa Miundombinu mbalimbali ikiwemo Hospitali za JWTZ kama vile Hospitali kuu ya Jeshi Lugalo, Chuo cha Tiba cha Kijeshi na Hospitali ya Jeshi ya Kanda ya Arusha. Aidha Jenerali Mkunda amewataka Madaktari na wauguzi watakaokuwa wakitoa huduma katika Hospitali hii kuitunza ili iendelee kutoa huduma bora kwa kizazi cha sasa na cha baadae kwani miundombinu iliyowekwa katika Hospitali hiyo ...