Skip to main content

Posts

Showing posts from September 27, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

AZANIA YATANGAZA MKOPO BILIONI 5 BILA DHAMANA KWA WACHIMBAJI WA DHAHABU GEITA

  Benki ya Azania imeeleza kuwa inatoa huduma mbalimbali za mikopo kwa wafanyabiashara, wawekezaji na wadau wa sekta ya madini, ikiwa ni pamoja na mikopo ya mitaji, uwekezaji na ununuzi wa mitambo na vifaa vya uzalishaji. Kwa mujibu wa benki hiyo, baadhi ya mikopo hutolewa kwa ajili ya kuendesha shughuli za biashara na kulipwa kwa vipindi vya miezi mitatu, huku mikopo ya uwekezaji ikitolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali. Benki hiyo pia inatoa mikopo ya ununuzi wa mitambo na vifaa mbalimbali kwa ajili ya shughuli za uzalishaji, ikiwemo mashine, vifaa vya kutengeneza betri na vifaa vingine vya viwandani. Aidha, mikopo hutolewa kwa ajili ya ununuzi wa vyombo vya usafirishaji kama magari, malori na matipa. Katika sekta ya madini, Benki ya Azania imeeleza kuwa ina bidhaa maalumu inayolenga kuwasaidia wachimbaji na wafanyabiashara wa dhahabu wanaouza madini yao kupitia Benki Kuu ya Tanzania. Kupitia bidhaa hiyo, mteja anaweza kupata mkopo wa hadi Shilingi bilioni tano bil...

SANGU - BILA NBS HAKUNA MIPANGO YA TAIFA INAENDA

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, amesema hakuna mipango ya maendeleo ya Taifa inayoweza kufanikiwa bila mchango wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS). Sangu ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea banda la NBS katika Maonesho ya Tisa ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Geita. Waziri huyo amesema upatikanaji wa takwimu sahihi na kwa wakati ni nguzo muhimu katika kufanikisha mipango ya maendeleo ya Taifa, kwa kuwa takwimu zinazokusanywa, kuchambuliwa na kuhifadhiwa na NBS husaidia Serikali pamoja na wadau wengine kufanya maamuzi yanayozingatia uhalisia wa mahitaji ya wananchi. Kwa mujibu wake, uwepo wa takwimu sahihi unawezesha kuweka vipaumbele vya maendeleo, kuandaa mipango na kufuatilia utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Taifa. Amesisitiza umuhimu wa NBS kuendelea kuboresha mifumo ya ukusanyaji na uchambuzi wa takwimu, huku akitoa wito wa kuhakikisha taarifa hizo zinapatikana kwa wa...

KIRUSWA AWATAKA WADAU KUBADILISHA MAAZIMIO KUWA MIRADI DIRA 2050

  Na Richard Mrusha A24TV  Serikali imesisitiza umuhimu wa matumizi ya teknolojia za kisasa na uwekezaji katika kuongeza tija, usalama na thamani ya madini nchini, huku ikiwataka wadau wa sekta hiyo kuwajibika kwa pamoja kuhakikisha rasilimali za madini zinawanufaisha Watanzania. Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, leo Septemba 27, 2026, wakati akifungua rasmi Maonesho ya Tisa ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Geita. Dkt. Kiruswa amesema kaulimbiu ya mwaka huu, "Madini ni Utajiri - Tuwajibike kwa Pamoja Kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050," inaweka wajibu kwa Serikali, wawekezaji, wachimbaji na wananchi kuhakikisha sekta ya madini inachangia kwa dhati katika utekelezaji wa Dira hiyo. Amesisitiza kuwa Maonesho ya Geita hayapaswi kubaki kuwa maonesho tu, bali yanapaswa kuwa chachu ya kubadilisha maazimio kuwa miradi, ubia na matokeo yanayopimika. "Uwajibikaji...

WACHUUZI WA DAGAA WAUMIZWA NA TOZO YA USHURU MANISPAA YA MUSOM

Na Mwandishi wetu Jovina Massano. Makamu Mwenyekiti Wa chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Wegesa Heche amesema kuwatoza ushuru mara mbili wachuuzi wa dagaa Manispaa ya Musoma ni kuwaumiza. Amesema hayo kwenye mkutano wa hadhara wakati akihutubia wananchi katika viwanja vya Shule ya sekondari Mara Septemba 25,2026. Kauli hiyo ameitoa mara baada ya Mwenyekiti CHADEMA Wilaya ya Musoma Urasa Jackson kuelezea changamoto zilizopo upande wa wajasiriamali wa dagaa. Heche amesema kuwatoza ushuru mara mbili ni kuwaumiza wachuuzi kwa kuwa vipato vyao ni vidogo watawezaje kumudu ghalama za maisha na kuziendesha familia zao. " Nchi hii ina madini mengi ambayo yanaweza kuchangia fedha nyingi kupitia tozo mbalimbali kwa nini wawaumize wauza dagaa wenye biashara ndogo huu ni uonevu ,"amesema Heche. Urasa amesema kuwa wachuuzi hutozwa ushuru wa Dagaa ndoo ya lita 20 hulipia Shillingi 1000 kwa mwezi 30,000/= ambapo kwa Mwaka ni 360,000/=na ya lita 10 wanalipia shillingi 500 kw...

MAGEREZA YAWIKA BAMMATA 2026, JKT NA NGOME JWTZ ZAKUBALI KICHAPO

 Na Ssgt Mawazo Mtondo – MWANZA Timu ya mpira wa wavu wanaume ya Jeshi la Magereza imeendeleza ushindani katika Mashindano ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) 2026, baada ya kuibuka na ushindi wa seti 3–1 dhidi ya Timu ya JKT Tanzania, katika mchezo mkali uliofanyika leo Septemba 27, 2026 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Mchezo huo uliokuwa wa kusisimua na wenye mashambulizi makali kutoka pande zote mbili, uliwashuhudia wachezaji wa Magereza wakitumia vyema mipango ya ushambuliaji na kuweka ulinzi imara, hali iliyowawezesha kutawala mchezo na hatimaye kupata ushindi wa seti 3–1. Ushindi huo umeongeza nguvu kwa timu hiyo katika mwendelezo wa mashindano hayo, huku Magereza ikiendelea kuonyesha ushindani mkubwa dhidi ya timu za majeshi na vyombo vya ulinzi na usalama vinavyoshiriki BAMMATA 2026. Katika mchezo uliotangulia, Timu ya Kanda ya Magereza ilikutana na Timu ya Ngome ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambapo Magereza ilipata ushindi wa...

WAZIRI MKUU: SEKTA BINAFSI NI MUHIMU KUFIKIA UCHUMI WA DOLA TRILIONI MOJA

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema ushirikishwaji wa sekta binafsi ni muhimu katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya Tanzania, hasa azma ya kufikisha thamani ya uchumi wa Taifa hadi dola za Marekani trilioni moja ifikapo mwaka 2050. Dkt. Mwigulu ameyasema hayo leo, Jumapili, Septemba 27, 2026, jijini Doha, Qatar, alipokutana na Makamu wa Kwanza wa Chama cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda cha Qatar (QCCI), Bw. Mohammed bin Ahmed bin Twar Al Kuwari, pamoja na ujumbe wake katika kikao kilichofanyika katika Hoteli ya Kempinski. Waziri Mkuu amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekuwa akisisitiza umuhimu wa kuishirikisha sekta binafsi katika mipango ya maendeleo ya nchi, kupitia Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050. “Tunaamini kwamba Serikali peke yake haiwezi kufanikiwa katika uwekezaji huo bila kushirikisha wawekezaji wa ndani au wa nje. Ndiyo maana Serikali imeweka vivutio vya kiuwekezaji ili kuvutia mitaji,” amesema Dkt. Mwigulu. Katika k...

TANZANIA-MISRI KUSHIRIKIANA KATIKA UONGEZAJI THAMANI MADINI YA KUZALISHA MBOLEA

 ▪️Waziri Mavunde na Waziri Badawi wakubaliana kuimarisha uhusiano kwenye sekta ya madini ▪️Watalaamu wa nchi mbili kubadilishana uzoefu kwenye utafiti na uendelezaji wa Phosphate ▪️Wawekezaji wakubwa wa Viwanda vya mbolea kutembelea Tanzania kuangalia fursa za uchimbaji na uongezaji thamani ▪️Misri yaipongeza Tanzania kwa mchango wa wachimbaji wadogo kwenye uchumi *Cairo, Misri* Pembezoni mwa Mkutano wa Madini wa Misri (Egypt Mining Forum), Waziri wa Madini *Mheshimiwa Anthony P. Mavunde* amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Petroli na Rasilimali Madini wa Misri, *Mheshimiwa Karim Badawi* ambapo wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika uongezaji thamani madini ya kuzalisha mbolea ili kuchochea ukuaji wa uchimbaji wa madini na ukuzaji wa sekta ya kilimo. Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 27 Septemba, 2027 walipokutana wakati wa Mkutano wa Madini wa Misri, unaofanyika katika Hoteli ya St. Regis Jijini Cairo. "Tanzania na Misri zina historia ya muda mrefu wa mashirik...

EQUITY BANK TANZANIA YAPANUA HUDUMA ZA KIFEDHA KWA WADAU WA SEKTA YA MADINI

 Na Wellu Mtaki, Geita Equity Bank Tanzania imeeleza kuwa inaendelea kutoa huduma mbalimbali za kifedha kwa wadau wa sekta ya madini, ikiwa ni pamoja na kuwawezesha katika ununuzi wa mitambo na vifaa, pamoja na kugharamia shughuli za biashara katika mnyororo mzima wa thamani wa madini. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Biashara kwa Wateja Wadogo, wa Kati na Binafsi wa Equity Bank Tanzania, Theresia Aloyce, wakati wa Maonesho ya Tisa ya Madini yaliyofanyika Geita. Aloyce alitoa kauli hiyo baada ya Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, kutembelea banda la benki hiyo na kupata maelezo kuhusu huduma zinazotolewa kwa wadau wa sekta ya madini. Kwa mujibu wa Equity Bank Tanzania, huduma hizo zinalenga kuwafikia wadau mbalimbali wanaoshiriki katika sekta ya madini, wakiwemo wachimbaji, wafanyabiashara pamoja na watoa huduma zinazohusiana na shughuli za uchimbaji na biashara ya madini. Benki hiyo pia inatoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa vitendea kazi na mitambo inayohitajika katika ...

ZANZIBAR MAGAZINE YAZINDULIWA NEW YORK, YAANGAZIA MAONO YA MAMA MARIAM MWINYI KATIKA UCHUMI WA BULUU

 Jarida la Zanzibar Magazine limezinduliwa pembezoni mwa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA 81), jijini New York, Septemba 2026 likiwa na makala maalum inayoangazia kazi zinazofanywa na Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) pamoja na maono ya Mama Mariam Mwinyi katika kuendeleza Uchumi wa Buluu Zanzibar. Makala hiyo, inayoanzia ukurasa wa 12, inaangazia umuhimu wa kuwa na mtazamo shirikishi na jumuishi katika kurndeleza Uchumi wa Buluu, hususan katika sekta ya kilimo cha mwani, kwa kuzingatia nafasi na mchango wa wanawake na vijana. Aidha, makala hiyo inaeleza juhudi zinazofanywa na Serikali pamoja na wadau mbalimbali katika kuwawezesha wanawake na vijana kunufaika na fursa za Uchumi wa Buluu, na kuibadilisha shughuli ya kilimo cha mwani kutoka uzalishaji wa kujikimu na kuwa shughuli endelevu na yenye tija kiuchumi. Uzinduzi wa jarida hilo unaendelea kutoa fursa ya kuonesha juhudi, mafanikio na fursa zilizopo Zanzibar katika kuwawezesha wananchi, hususan wanawak...

MKIIPOTEZA AMANI ILIYOPO TANGA,ITAWAGHARIMU" KIHONGOSI.

 Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga. Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC),Itikadi,Uenezi na Mafunzo Kenani Kihongosi amewataka wananchi wa mkoa wa Tanga kuendelea kuilinda na kutunza amani na utulivu vilivyopo vispotee,kwani vikipotea kuvirejesha tena sio kazi rahisi. Rai hiyo ameitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya lamore alipokuwa akihutubia wananchi na wanachama wa CCM ikiwa ni katika kuhitimisha ziara yake katika mkoa wa Tanga. Aidha Kihongosi ameendelea kusema kuwa wanaochoea vurugu familia zako mara zote huwa salama na wanaoathirika ni wananchi wa hali ya chini hivyo basi ni jambo la kulitafakari kwa kina kabla ya kufanya maamuzi yatakayo chochea uvunjifu wa amani. "Niwaombe sana ndugu zangu wa Tanga kuendelea kuwa na utulivu huu mliouonesha kipindi chote kwani hata oktoba 29 mwaka jana Tanga ilikuwa salama,sehemu yoyote yenye amani na utulivu maendeleo huonekana nadio maana hata miradi ya kimkakati na maendeleo inakuka Tanga sasa kama ujenzi wa...

SERIKALI YAONGEZEA THAMANI MASHINDANO YA SHIMIWI

  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema itaongeza thamani na katika Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara Idara za Serikali(SHIMIWI) ili kuongeza ari na hamasa ya michezo nchini. Hayo yamesemwa leo Septemba 26, 2026 Mkoani Kilimanjaro na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo ambapo amesema pamoja na zawadi za Vikombe pia zitatolewa pesa taslimu kwa timu, na mchezaji mmojammoja aliyefanya vizuri.

MICHEZO YATAJWA CHACHU YA HUDUMA BORA KWA WANANCHI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amewataka watumishi wa umma kuimarisha umoja, mshikamano na ushirikiano kupitia michezo ili kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wananchi kwa uadilifu. Waziri Makonda ametoa kauli hiyo Septemba 26, 2026 wakati akifungua rasmi Michezo ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), inayofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Polisi Moshi, mkoani Kilimanjaro ikishirikisha jumla ya watumishi 2,771 kutoka wizara, mikoa, taasisi, idara na wakala wa Serikali. Mashindano hayo yameanza Septemba 20 na yanatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 7, 2026, yakilenga pia kuwawezesha watumishi kushiriki katika shughuli za michezo na kuimarisha afya na mahusiano kazini.