Skip to main content

Posts

Showing posts from August 9, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Kombo Ajitambulisha Kwa Rais wa Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar bado inahitaji wawekezaji zaidi kuja kuwekeza nchini kupitia nyanja mbalimbali. Ameeleza kuwa zipo fursa nyingi za uwekezaji Zanzibar ambazo wawekezaji wanaweza kuja kuwekeza katika nyanja mbalimbali na kuielekeza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuweka mkazo katika eneo hilo. Dkt. Mwinyi aliyasema hayo tarehe 09 Agosti, 2024 wakati alipokutana na Waziri na Manaibu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika walipofika Ikulu kujitambulisha baada ya kuteuliwa hivi karibuni. Dkt. Mwinyi amesema ni vema Wizara ijikite kutafuta wawekezaji wa kuja kuwekeza nchini pamoja na kunufaika kidiplomasia na mataifa mengine. Pia ameilekeza Wizara kuangalia pia masoko mengine ya kuleta wawekezaji na watalii ikiwemo kutoka nchi za Asia na Mashariki ya Mbali.

Balozi Kombo na Cosato Chumi Wakutana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

Na Andrew Chale-Zanzibar  WAZIRI  wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki, Mhe Balozi Mahmoud Thabit Kombo na Naibu wake katika Wizara hiyo, Mhe. Cosato Chumi wamejitambulisha rasmi na kufanya mazungumzo Ofisini kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman,  Agosti 09, 2024 Migombani, Mkoa wa Mjini-Magharibi, Unguja. Tukio hilo la kujitambulisha, baada ya Mabadiliko ya hivi karibuni, aliyoyafanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ndani ya Baraza lake la Mawaziri. Akitoa Salamu zake mbele ya Ujumbe huo, Mhe.Othman amesema ni vyema kwa Taifa kutumia fursa zilizopo katika Muunganiko wa Afrika Mashariki, ili kujiimarisha kiuchumi. Amesema, Afrika Mashariki siyo Jumuiya tu, bali ni  Shirikisho la kufungua fursa nyingi za kiuchumi ambazo zikitumika vyema, zitaleta tija kwa Taifa. Aidha amewaelekeza Viongozi wanaosimamia Wizara hiyo, pia kuzitumia fursa zilizopo katika Taasisi za Kimataifa ili kuenda...

Dkt.Emmanuel Nchimbi Ataka Kero za Wananchi Karagwe Zishughulikiwe

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amemuelekeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki kuifanyia kazi na kupata ufumbuzi wa changamoto ya wanyama waharibifu wanaovamia makazi ya watu, kuharibu mazao na kutishia uhai wa binadamu, Wilaya ya Karagwe. Vile vile, Katibu Mkuu Balozi Dkt. Nchimbi amezielekeza mamlaka husika mkoani Kagera, kwa kushirikiana na wizara za kisekta husika, kushughulikia na kumaliza tatizo la matumizi ya ardhi, mipaka kati ya wananchi na Kampuni ya Ranchi za Taifa NARCO, wilayani Karagwe.  Balozi Nchimbi ametoa maelekezo hayo alipokua akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kituco cha Mabasi cha Kayanga, wilayani Karagwe, mkoani Kagera, akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya siku sita mkoani humo, ambapo miongoni mwa kero za wananchi wa jimbo alizotaarifiwa, ni pamoja na uvamizi wa wanyama hao wakali katika vijiji vya Kata ya Kihanga (Kihanga, Kibwela na Mshabaiguru), ambako Tembo wanavamia mashamb...

Bilioni 25.4 Kutumika Kusambaza Nishati ya Umeme Musoma Vijijini

Na Shomari Bunda-Musoma KIASI cha shilingi bilioni 25.4 kimetengwa kwa shughuli ya usambazaji Nishati ya umeme kwenye vitongoji 374 vilivyopo kwenye vijiji 68 vya jimbo la Musoma vijijini. Kauli hiyo imetolewa jana agosti 8 na mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sosperer Muhongo wakati akielezea shughuli ya usambazaji wa umeme itakayoanza jumatatu ya agosti 12. Amesema REA na TANESCO wanayo maombi ya kusambaziwa umeme kwenye vitongoji hivyo na mipango inayoendelea na utasambazwa kwa awamu endelevu. Muhongo amesema upo mradi wa vitongoji 68 kila Kata ambapo mradi huo unatekelezwa sasa kwenye (Lot V) Mbunge huyo amesema viongozi  wa Kata, Vijiji na Vitongoji wanapaswa kuwa na orodha ya maeneo yao kuanza kusambaza nguzo kupitia mkandarasi Alpha TND Ltd Amesema upo mradi wa Vitongoji 15 ambapo mradi huu ni utekelezaji wa ahadi ya Wizara ya Nishati kwa wabunge wote kila jimbo litasambaziwa umeme kwenye Vitongoji 15 mkandarasi ikiwa kampuni ya Dieynem Co Ltd "Mkandarasi anaendele...

Bashungwa Atoa Wito Kwa Watanzania Kujitokeza Katika Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura

Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa ametoa wito kwa watanzania wenye sifa za kujiandikisha katika Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, kujitokeza katika vituo ili kupata Kitambulisho cha Mpiga Kura kitakachowawezesha kupata haki ya kuchagua Viongozi katika Uchaguzi. Bashungwa ametoa wito huo leo Agosti 09, 2024 mara baada ya kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Kituo cha Shule ya Msingi ya Ahakishaka, Kata ya Nyabiyonza Wilayani Karagwe Mkoani Kagera. “Tukitaka kupata viongozi wazuri hatua ya kwanza ya kufanya ni kujiandikisha kwenye daftari ili tuweze kutumia haki yetu ya kidemokrasia muda utakapofika wa uchaguzi”, amesema Bashungwa. Bashungwa ameipongeza Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuboresha zoezi hilo na kufanya kazi kwa weledi inayoimarisha Demokrasia nchini. Aidha, Bashungwa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kinara wa kuendelea kuimarisha Demokrasia nch...