Skip to main content

Posts

Showing posts from May 13, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tanzania na Kenya Kuharakisha Utekelezaji Miradi ya Kuunganisha Njia za Umeme

📌*Mhandisi Mramba afanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Mafuta Kenya* Tanzania na Kenya zimekubaliana kuharakisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya njia za umeme zinazounganisha gridi za nchi hizo mbili pamoja na kuboresha mifumo ya usafirishaji wa umeme ili kuimarisha usalama wa nishati, kuongeza uhakika wa upatikanaji wa umeme na kukuza biashara ya umeme katika ukanda wa Afrika Mashariki. Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Felchesmi Mramba, kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Mafuta wa Kenya, Bw. Alex Wachira, jijini Nairobi, Kenya. Mazungumzo hayo yalijikita katika kuimarisha ushirikiano katika sekta ndogo ya umeme na nishati jadidifu, hususan biashara ya umeme, utekelezaji wa miradi ya uunganishaji wa gridi za umeme pamoja na maboresho ya mifumo ya usafirishaji na usambazaji wa umeme kati ya Tanzania na Kenya.  Viongozi hao pia walijadili hatua mba...

Watumishi Wapya Tume ya Madini Watakiwa Kuzingatia Maadili Sehemu ya Kazi

Dodoma Watumishi wapya 37 wa Tume ya Madini wametakiwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, uwajibikaji na uzalendo katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuimarisha usimamizi wa Sekta ya Madini na kuongeza mchango wake katika Pato la Taifa. Wito huo umetolewa wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi kwa waajiriwa hao kabla ya kuripoti katika vituo vyao vya kazi mbalimbali nchini. Akizungumza katika Ofisi za Tume ya Madini Makao Makuu jijini Dodoma, Meneja wa Utawala wa Tume ya Madini, Jacob Mnyenyelwa, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala, Nsajigwa Kabigi, amesema watumishi hao wanapaswa kuzingatia maadili ya kazi, weledi na uwazi wanapotoa huduma kwa wananchi na wadau wa sekta ya madini. Amesema wananchi wana matarajio makubwa kutoka katika Sekta ya Madini, hivyo watumishi wapya wanapaswa kuwa mfano bora wa uadilifu, ubunifu na uzalendo ili kuhakikisha rasilimali madini zinasimamiwa kwa manufaa ya Taifa.  Amesisitiza kuwa utendaji wenye maadili utaong...

Waziri Mavunde Asimamisha Uchimbaji wa Madini kwenye Mto Katavi

▪️Ni kutokana na mapungufu ya mpango wa usimamizi wa mazingira ▪️Aelekeza kupewa hati za makosa wamiliki wa Leseni za Utafiti mkoani Katavi ▪️Aelekeza ukaguzi wa mikataba ya msaada wa kiufundi(TSA) nchi nzima ▪️Wachimbaji wadogo wampongeza Rais Samia kwa kupatiwa Leseni tatu kubwa zilizofutwa ▪️Ziara hii ya utatuzi wa migogoro ni maelekezo ya Waziri Mkuu Mwigulu aliyotoa mkoani Katavi ▪️Wachimbaji waishukuru serikali kwa utatuzi wa changamoto zilizokuwa zinawakabili *Katavi* Kufuatia ukaguzi uliofanywa kwa wamiliki wa leseni wanaofanya uchimbaji kwenye mto na kuathiri mazingira, Waziri wa Madini *Mheshimiwa Anthony Mavunde (Mb)* atoa maelekezo ya kusimamishwa kwa shughuli za uchimbaji madini kwenye mto huo Mkoani Katavi. Ametoa kauli hiyo tarehe 13 Mei, 2026 alipofanya ziara ya ukaguzi wa shughuli za uchimbaji madini katika Manispaa ya Mpanda na Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi. "Mhe. Rais ametupa maelekezo mahsusi Wizara ya Madini kuhakikisha shughuli zote za uchimbaji zinafan...

MV. Liemba 70% Complete, Set to Resume Service on Lake Tanganyika in July 2026

  By Prosper Makene  Residents of Kigoma, Katavi, and Rukwa regions are set to benefit once the historic MV. Liemba completes rehabilitation and resumes official service in July 2026 on Lake Tanganyika. As of early May, the overhaul had reached 70% completion. The restoration of the decades-old vessel, vital to the economy of Tanzania’s western corridor, is part of the Sixth Phase Government’s efforts under President Dr. Samia Suluhu Hassan to improve transport services, boost trade, and raise living standards for communities along Lake Tanganyika.  MV. Liemba suspended operations in 2018 due to engine and infrastructure deterioration. The major rehabilitation began in July 2024 at a cost of more than USD 13 million and is scheduled for completion in July 2026. The project is being implemented by Tanzania Shipping Agency Corporation, with technical support from international partners. Speaking on the project’s progress, Project Manager Elias Kivara said the refurbishment ...

Mv Liemba Kurejea Tena Julai Mwaka Huu

  Na Prosper Makene  Wananchi wa mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa wanatarajia kunufaika mara baada ya kukamilika kwa ukarabati wa Meli  ya Kihistoria ya MV. Liemba inayotarajiwa kurejea rasmi kutoa huduma Julai 2026 katika mwambao wa Ziwa Tanganyika ambapo hadi mwanzoni mwa mwezi Mei imefikia asilimia 70 Kukamilika kwa meli hiyo kongwe na muhimu kwa uchumi wa ukanda wa Magharibi ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji, kuchochea biashara na kuinua maisha ya wananchi wa mwambao wa Ziwa Tanganyika.  MV. Liemba ambayo ilisimamisha safari zake mwaka 2018 kutokana na uchakavu wa mitambo na miundombinu yake, ipo kwenye hatua za mwisho za ukarabati mkubwa ulioanza Julai 2024 kwa gharama ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 13, huku ukitarajiwa kukamilika Julai 2026. Akizungumza kuhusu maendeleo ya mradi huo, Meneja wa Mradi, Elia...

Bilioni 171 kutikisa Sekta ya Meli nchini

WAZIRI wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema Serikali imejipanga kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya usafiri wa majini baada ya kutenga Shilingi bilioni 171 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya, ukarabati wa meli kongwe na utekelezaji wa miradi mikubwa kupitia Tanzania Shipping Company Limited (TASHICO). Akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi leo Mei 13, 2026 Bungeni jijini Dodoma, Prof. Mbarawa amesema uwekezaji huo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuimarisha uchumi wa buluu, kuongeza usalama wa usafiri wa majini na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara ya usafiri wa maji katika ukanda wa Afrika Mashariki. Katika mpango huo, Serikali itajenga meli mpya ya mizigo yenye uwezo wa kubeba tani 3,500 katika Ziwa Tanganyika, sambamba na kuanza ujenzi wa meli mbili za mafuta zenye uwezo wa kubeba lita 600,000 kila moja. Pia, Serikali itajenga meli mpya ya abiria yenye uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 400 za mizigo katika ziwa hilo, hatua inayota...

Bilioni 171 kutikisa Sekta ya Meli nchini

WAZIRI wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema Serikali imejipanga kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya usafiri wa majini baada ya kutenga Shilingi bilioni 171 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya, ukarabati wa meli kongwe na utekelezaji wa miradi mikubwa kupitia Tanzania Shipping Company Limited (TASHICO). Akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi leo Mei 13, 2026 Bungeni jijini Dodoma, Prof. Mbarawa amesema uwekezaji huo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuimarisha uchumi wa buluu, kuongeza usalama wa usafiri wa majini na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara ya usafiri wa maji katika ukanda wa Afrika Mashariki. Katika mpango huo, Serikali itajenga meli mpya ya mizigo yenye uwezo wa kubeba tani 3,500 katika Ziwa Tanganyika, sambamba na kuanza ujenzi wa meli mbili za mafuta zenye uwezo wa kubeba lita 600,000 kila moja. Pia, Serikali itajenga meli mpya ya abiria yenye uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 400 za mizigo katika ziwa hilo, hatua inayota...

Serikali Kujenga Uwanja wa Kimataifa Mwanza

_▪︎ Dkt. Mwigulu asema Serikali imejipanga kujenga jengo lenye hadhi ya kimataifa_ _▪︎ Asema Mwanza itaendelea kuwa kitovu muhimu cha shughuli za kiuchumi Kanda ya Ziwa_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua kuhakikisha Uwanja wa Ndege wa Mwanza unaboreshwa na kujengwa katika hadhi ya kimataifa ili kuendana na hadhi ya jiji la Mwanza kama kitovu muhimu cha shughuli za kiuchumi Kanda ya Ziwa. Amesema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akitoa kauli ya Serikali kuhusu hoja ya maendeleo ya Uwanja wa Ndege wa Mwanza iliyowasilishwa na Mbunge wa Magu, Mhe. Boniventura Kiswaga, katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwenye Kikao cha 28 cha Mkutano wa Tatu wa Bunge la 13, leo Mei 13, 2026. Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua umuhimu wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza na imeendelea kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha unakuwa na uwezo wa kuhudumia ndege kubwa pamoja na kukidhi viwango vya kimataifa. “Zipo jitihada ambazo zimekuwa zikifanyika kuhakik...