Skip to main content

Posts

Showing posts from July 18, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mradi wa Uchimbaji Madini ya Urani Kuongeza Upatikanaji wa Umeme Nchini

▪️Kiasi cha tani milioni 139 ya mashapo ya urani yakadiriwa kuwapo,* ▪️Madini ya Urani kutumika kuzalishia umeme nchini ▪️ Rais Samia apongezwa kwa kuvutia uwekezaji ▪️Ujenzi wa kiwanda cha majaribio cha uchenjuaji wa Urani wakamilika ▪️Mradi kugharimu Trilioni 3.06 mpaka kukamilika kwake Namtumbo,Ruvuma Waziri wa Madini, *Mheshimiwa Anthony Mavunde (Mb)* abainisha kuwa mradi wa kimkakati wa uchimbaji wa madini ya Urani kuanza hivi karibuni baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda cha majaribio cha uchenjuaji wa madini hayo. Ameyasema hayo jana tarehe 18 Julai, 2025 Wilayani Namtumbo alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo unaokadiriwa kugharimu zaidi ya Tsh 3.06 Trilioni unaotekelezwa  na Kampuni ya Mantra Tanzania Limited. "Moja kati ya vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa *Mhe. Dkt. Samia S.Hassan* kwenye sekta ya madini ni suala la uongezaji thamani madini ndani ya nchi yetu, na Mhe. Rais ametupa maelekezo mahsusi Wiz...

Umoja Wa Mataifa Wazidi Kuliamini Jwtz

 *Lakabidhiwa mradi wa ujenzi wa madaraja kupitia* *MINUSCA*  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeendelea kuthibitisha umahiri na uaminifu wake katika operesheni za kimataifa baada ya Umoja wa Mataifa kupitia Ujumbe wa Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA), kwa kulipatia jukumu la ujenzi wa mradi muhimu wa madaraja katika Mkoa wa Mambere-Kadei. Ujenzi wa madaraja hayo matatu ni yale yaliyoharibika kwa muda mrefu, yakitatiza mawasiliano kati ya vijiji na miji, na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma muhimu kama elimu, afya, na masoko. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa ujenzi huo, Katibu Mkuu wa Mkoa wa Equatorial, Mheshimiwa Zouketchia Emmanuel, amelishukuru JWTZ kwa kujitolea kwao na mchango wao mkubwa kwa wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. > "Tumepata shida ya usafiri kwa muda mrefu kwa sababu ya madaraja haya. Leo tunaona mabadiliko yanayoletwa na MINUSCA kupitia marafiki  zetu wa kweli kutoka Tanzania. Asanteni sana JWT...

Tanzania na Kenya wazindua mawasiliano ya pamoja

Na MASHAKA MHANDO, Horohoro SERIKALI za Tanzania na Kenya zinakwenda kuimarisha diplomasia ya kidijitali, biashara na uchumi baada ya kuzindua mkongo wa mawasiliano baina ya nchi hizo. Wakizindua mkongo huo Leo Julai 18 Waziri wa Mawasiliano na teknolojia ya Habari Jerry Silaa alisema uzinduzi wa maunganisho ya mkongo wa Taifa wa mawasiliano (NICTBB) wa TTCL na mikongo ya bahari iliyopo Mombasa kupitia ICTA Kenya katika eneo la Horohoro wilayani Mkinga mkoani Tanga, utakuwa na faida kubwa kwa wananchi. Alisema kupitia mkongo huo wananchi wataweza kupata huduma nafuu ya mtandao ambayo itasaidia kuimarisha shughuli za kibiashara na uchumi kutokana na kuimarika kwa miundombinu hiyo ya mawasiliano itakayokuwa na kasi zaidi. "Tunakwenda kuangalia sera zetu katika maeneo ya kutolea huduma baina ya nchi zetu ili wananchi waweze kupata huduma bora za mawasiliano lakini zinazozingatia maadili na weledi"alisema Waziri Silaa. Alisema kazi ya kujenga miundombinu ya nchi zinazoshirikiana ...