Skip to main content

Posts

Showing posts from April 5, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu awataka Mabalozi kuishi farsafa za Rais Dkt.Samia

  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka mabalozi kuiishi falsafa ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha mahusiano na kukuza diplomasia ya kiuchumi kati ya Tanzania na mataifa mbalimbali duniani. Mheshimiwa Majaliwa amesema kufanya hivyo kutaiwezesha Tanzania kuvutia wawekezaji katika sekta mbalimbali zikiwemo za viwanda, kilimo, biashara pamoja na kupata masoko ya bidhaa zinazozalishwa nchini. Ameyasema hayo leo (Jumapili, Aprili 6, 2025) alipokutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Balozi Hamad Khamis Hamad Balozi wa Tanzania nchini Msumbuji na Mheshimiwa Balozi Holmes Matinyi, Balozi wa Tanzania nchini Sweden. Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali ina mategemeo makubwa na mabalozi hao, hivyo wanapaswa kwenda kuendeleza mahusiano mazuri ya muda mrefu yaliyopo baina ya Tanzania na mataifa hayo.  Waziri Mkuu amesema pamoja na mambo mengine mabalozi hao wanatakiwa wahakikishe wanasimamia vizuri matumizi ya fedha katika ofisi zao pamoja na kuanzisha au kuend...

Majaliwa - Mei Mosi inalenga kuboresha ustswii wa wafanyakazi

  _Achangisha zaidi ya sh. Bilioni 1.6 katika harambee ya Mei Mosi 2025_ WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani yana lengo la kuhamasisha utoaji wa haki za wafanyakazi, kuboresha masharti ya kazi na ustawi wa wafanyakazi kwa ujumla. Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo jana usiku, Aprili 5, 2025 katika hafla ya chakula cha jioni kwa ajili ya kuchangisha fedha za kugharamia maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambayo kitaifa yatafanyika mkoani Singida. Hafla hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa Royal Village jijini Dodoma. Amesema dhumuni jingine la maadhimisho hayo ni kutambua na kuenzi michango ya wafanyakazi katika maendeleo ya jamii na uchumi, Mei Mosi ni fursa ya kuonesha mshikamano kati ya wafanyakazi na kuhimiza usawa na haki katika maeneo ya kazi duniani kote. Waziri Mkuu amesema mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Katika hafla hiyo jumla ya shilingi bilioni 1.62 zilikusanywa ...

Butiku-Rais Samia Amefanya Mambo Makubwa,Aungwe Mkono

-Ampa asilimia 85 kiutendaji -Ashangaa wanazungumzia ukubwa wa deni la taifa bila kujivunia miradi iliyopo -Atoa heko kwa CCM  kumteua kuwa mgombea wake  -Awaonya Chadema,asema hakuna mwenye mamlaka kuzuia uchaguzi Na George Marato-gmtv Mwenyekiti wa taasisi ya Mwalimu Nyerere mzee Joseph Butiku,amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo,ikiwemo inayolenga kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi hapa nchini. Mzee Butiku ameyasema hayo ofisini kwake jijini  Dar es Salaam katika mahojiano maalum,ambapo amesema kazi kubwa ya utekelezaji wa miradi hiyo hasa ya sekta ya nishati,maji,elimu,afya,Reli na barabara katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia imewaziba midomo baadhi ya watu. Amesema kuwa hakuna ubishi kuwa Rais Samia ameonesha utashi na mapenzi makubwa kwa taifa lake hasa katika kukamilisha miradi mikubwa ya kimkakati ukiwemo wa Reli,Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere na ujenzi wa madaraja makubwa likiwemo la Busisi. A...

Wakazi wa Jiji wajitokeza kwa wingi kupata huduma za macho bure

📍 Wampongeza mbunge Ummy kwa kutatua changamoto zinazowagusa 📍Wasema ni mbunge wa aina yake kutokea katika Jimbo la Tanga  📍 Mwenyewe ampongeza Rais kujenga vituo vingi vya afya 📍 Daktari wa macho asema ulaji mihogo chanzo cha tatizo la macho nchini 📍Bilal Muslim Mission wasema wamekuja kutekeleza ombi la mbunge  📍Yas wafurahia ushiriki wao kambi ya macho. Na Mwandishi Wetu, Tanga WANANCHI wa Jiji la Tanga, wamelazimika kutoa machozi ya furaha kufuatia Mbunge wa Jimbo la Tanga, Mhe Ummy Mwalimu maarufu Oddo Ummy, kuleta kambi ya huduma ya macho ya bure ambayo wananchi hao wamepimwa na kupata dawa, miwani pamoja na ushauri wa namna ya kuishi kuepuka magonjwa ya macho. Wakizungumza katika kambi hiyo inayofanyika kwa siku tatu katika shule ya sekondari ya Usagara baadhi ya wananchi, walisema kuwa mbunge wa Jimbo la Tanga anajua kugusa changamoto zinazowakabili wananchi wake. "Namshukuru sana mbunge, kiukweli amenitibu macho yangu, ni mbunge tunayetakiwa kumshikilia, anajua ...

Dk Carreen Rose Rwakatale achangia mbati 50 ujenzi nyumba ya Katibu wa Wazazi CCM

Na Mwandishi Wetu, Ifakara MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Mkoa wa Morogoro Dk. Careen-Rose Rwakatale amewataka viongozi wa (CCM) Wilaya mbalimbali mkoani hapa kuhakikisha wanajitoa katika ujenzi wa wa chama hawadhalilishwi kwa kufukuzwa kwenye nyumba za kupanga. Dk. Rwakatale alisema hayo jana wakati akikabidhi bati 50 zenye jumla ya thamani ya shilingi milioni 1.5 kwa viongozi wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kilombero kama ahadi yake aliyoitoa wakati ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Jumuiya hiyo ulioanza hapo mwaka Jana 2023. Alisema watumishi wamekuwa wakipata tabu sana kwa sababu kupanga nyumba sio vizuri, ambapo ikitokea wenye nyumba wamekasirika wanaweza kumfukuza au kumtolea vyombo nje na hiyo ni kumdhalilisha mtumishi na kukidhalilisha chama. “Nyumba za kupanga kwa mtumishi siyo nzuri anaweza kudhalilishwa yeye au chama hasa pale anapokosa hela za pango lakini kwenye nyumba zetu atakuwa amekaa kwa kutulia huku akitekeleza majukumu yake bila wasiwasi wa kufukuzwa” alisema. Aid...

Balozi Dkt Nchimbi azungumza na wananchi wa Mbamba Bay wilayani Nyasa

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza na wananchi wa Mji wa Mbamba bay, wilayani Nyasa, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Bandari, leo Jumamosi tarehe 5 Aprili 2025, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya siku tano katika Mkoa wa Ruvuma.