Skip to main content

Posts

Showing posts from March 4, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Makatibu Wakuu EAC Wakutana Kwa Maandalizi ya Mkutano wa 25 wa Wakuu wa Nchi

Makatibu Wakuu wa Nchi Wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanaosimamia masuala ya mtangamano wamekutana katika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo jijini Arusha, ikiwa ni muendelezo wa maandalizi ya Mkutano wa 25 Wakuu wa Nchi Wanachama wa EAC utakaofanyika tarehe 7 Machi 2026 jijini Arusha.  Kikao hicho cha Makatibu Wakuu ambacho ni sehemu ya Mkutano Maalum wa 59 wa Baraza la Mawaziri wa EAC, pamoja na masuala mengine umepokea na kujadili agenda na taarifa mbalimbali zilizowasilishwa na mkutano wa Ngazi ya Wataalamu uliofanyika tarehe 2 hadi 3 Machi 2026. Agenda na taarifa hizo zitawasilishwa na kujadiliwa kwenye Mkutano wa Mawaziri utakaofanyika tarehe 5 Machi 2026 jijini Arusha. Akifungua mkutano huo Dkt. Caroline W. Karugu PhD, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki nchini Kenya, na Mwenyekiti wa mkutano huo, ameeleza kuwa Jumuiya imeendelea kupiga hatua kubwa ya maendeleo huku ikizingatia ustawi wa watu wake kwa kuwezesha shughuli mbalimbali za...

Tume ya Uchunguzi, Yeriko Nyerere Wajadili ya Oktoba 29

DAR ES SAALAM:  TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, leo Machi 3, 2026 imekutana na mwanachama wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) ambaye pia ni mwandishi wa vitabu, Yeriko Nyerere. Mkutano huo wa Tume na Nyerere umefanyika katika ukumbi wa Lake Tanganyika uliopo jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mkoani hapa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Tume kukusanya taarifa, maoni na ushauri kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo wataalamu, watu wa kawaida, viongozi wa sasa na wastaafu. Katika mkutano huo hoja zilizojadiliwa zilihusu chanzo na tathmini ya athari za matukio hayo ndani ya nchi na kimataifa na ushauri wa hatua za kijamii na kisheria zinazochukuliwa ili kuimarisha amani, mshikamano wa kitaifa na matukio hayo yasijirudie tena. Tume inaendelea na mahojiano na waathirika wa Matukio hayo baada ya hivi karibuni Mamlaka ya Uteuzi kuiongezea Tume muda wa siku arobaini na mbili (42) kuanzia tarehe 20 Februa...

Makatibu Wakuu SADC Wabaini Changamoto za Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo

Kikao cha Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kupitia utekelezaji wa Mpango Mkakati Elekezi wa Maendeleo ya Kikanda (Regional Indicative Strategic Development Plan- RISDP) kimeanza leo tarehe 04 Machi 2026 jijini Pretoria, Afrika Kusini. Ujumbe wa Tanzania katika kikao hicho cha utangulizi kuelekea Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC utakaofanyika Machi 12 na 13, 2026, unaongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa.  Wakati wa hotuba za ufunguzi,  Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano ya Afrika Kusini, Balozi Tebogo Seokolo na Katibu Mtendaji wa SADC, Mhe. Elias Magosi walisisitiza umuhimu wa  mpango wa RISDP wa mwaka 2020 - 2030 kufanyiwa tathmini kwa lengo la kujiridhisha ufanisi wake na kubaini changamoto ili ziweze kupatiwa ufumbuzi kwa muktadha wa kuboresha utekel...

Waziri Mkuu aagiza muuguzi aliyefanya upasuaji nyumbani afukuzwe kazi kazi na afikishwe mahakamani

_Aelekeza TAKUKURU mahitaji ya ubadhirifu wa fedha kwenye mradi wa VETA Nyang'wale_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba ameagiza mamlaka zinazohusika kuchukua hatua kali dhidi ya muuguzi mmoja mkoani Tabora anayedaiwa kuwa mgonjwa nyumbani kwake nyumbani kinyume na maadili ya taaluma ya afya. Makumbusho leo Machi 4, 2026 alitumwa na Soko la Machinga jijini Dodoma baada ya kusimamishwa na watumishi hao, Waziri Mkuu hawezi mtu kufanya kazi nyumbani wakati Serikali imejenga hospitali, vituo vya afya na hospitali za rufaa katika maeneo mbalimbali ili wananchi wapate huduma salama. “Sasa naelekeza mamlaka zinazohusika: huyu si wa kuhamishwa, afukuzwe kazi mara moja Na akishafukuzwa apelekwe kwenye mkono wa sheria Na wale wanaotoa vibali vya zawadi wamnyang’anye hicho kibali. Aidha, Dkt. Mwigulu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Tabora msaidizi mtumishi huyo anakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria mara moja. “Mkuu wa Mkoa wa Tabora mkamateni, msimwachie. Afukuzwe kazi, aondolewe hiyo ha...