Skip to main content

Posts

Showing posts from July 25, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Chuo Kikuu Cha Makerere Kugeuza Hosteli zake Kuwa Hoteli wakati wa Likizo

 Chuo Kikuu cha Makerere kimepanga Kugeuza Hosteli zake kuwa Hoteli wakati wa Likizo ya Wanafunzi ili kuongeza Mapato ya chuo hicho kikongwe zaidi Afrika Mashariki.  Mpango huo umebainishwa Julai 25,2025 na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Barnabas Nawangwe wakati wa Makabidhiano ya Moja ya Hosteli iliyofanyiwa ukarabati mkubwa na wa kisasa.  "Nadhani tunatumia vibaya Hosteli hizi,kwanini zikae bila kutumika kwa miezi yote mitatu wanafunzi wanapokuwa Likizo bila kuzalisha fedha ilhali Hosteli zetu ni Bora kuliko hata baadhi ya Hoteli" Alisema Profesa Nawangwe wakati wa Makabidhiano hayo.  Profesa Nawangwe amesema kuwa Chuo hicho kitashirikiana na wafanyabiashara pamoja na kampuni yake ya Makerere Holding Ltd kwa ajili ya kusimamia uendeshaji wa hosteli hizo Kibiashara wakati wa Likizo. "Kwanini tusizigeuze hoteli wanafunzi wetu wanapokuwa Likizo, Watu wenye Mikutano wawe wanaleta washiriki hapa kupata huduma ya Malazi,pia wanaweza kufanyia Mikutano yao hapa na kutup...

Rais Kagame Ateua Waziri Mkuu Mpya

  Rais wa Rwanda Paul Kagame amemteua Dkt Justin Nsengiyumva, kuwa Waziri Mkuu mpya. Nsengiyumva anatwaa nafasi ya Édouard Ngirente, ambaye amehudumu katika wadhifa wa Waziri Mkuu tangu mwaka 2017. Nsengiyumva ni mtaalam wa masuala ya uchumi kutoka chuo kikuu cha Leicester, na awali alihudumu kama Naibu Gavana wa benki kuu nchini Rwanda tangu Februari mwaka huu. Kando ya Nsengiyumva, Rais Kagame pia ameteua mawaziri mapya wanne akiwemo wa michezo,Vijana na Sanaa, Afya pamoja na Kilimo na Mifugo

Italia Haiwezi Kulitambua Taifa la Israeli

Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia Antonio Tajani amesema leo Ijumaa kuwa nchi hiyo haiwezi ikakubali  “umwagaji damu na njaa” katika Ukanda wa Gaza. Ameishutumu Israel lakini akaelezea kuwa Italia haiko tayari kulitambua taifa la Palestina kama inavyopanga kufanya Ufaransa. “Kamwe hatuwezi tukakubali umwagaji damu na njaa,” alisema Tajani, kwa mujibu wa shirika la habari la Italia la ANSA. Aliongeza kuwa Italia inaweza tu kuitambua Palestina “wakati sawa kama utambuzi wao wa taifa la Israeli

Mhadhiri Afukuzwa Kazi Kwa Kosa la Kufanya Mapenzi na Mwanafunzi

  MAHAKAMA ya Kazi Jijini Nairobi imeidhinisha kufutwa kazi kwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Murang’a kwa kuhusika katika uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi. Mahakama hiyo imesisitiza kuwa tabia kama hiyo ni ukiukaji mkubwa wa maadili ya kazi. Mahakama ilibaini kuwa mhadhiri huyo, Bw NKB, alikuwa na uhusiano usiofaa na mwanafunzi aliyekuwa akisomea Shahada ya Biashara huku yeye akiwa mhadhiri katika Idara ya Uhandisi wa Umeme na Elektroniki. Jaji Mathews Nduma Julai 25  Mwaka huu aliamua kuwa tabia hiyo ya Mhadhiri huyo ilikiuka kanuni za maadili za Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Murang’a, na kufutwa kazi kwa NKB mwezi Machi 2020 kulifanywa kwa misingi halali ya Kisheria.  Mahakama ilitupilia mbali madai ya mhadhiri huyo ya kutaka arejeshwe kazini na dai lake la fidia ya Shilingi Millioni 22 kwa hasara ya ajira, kuharibiwa kwa sifa yake na madai ya ukiukaji wa haki zake za ajira. “Mahakama imeridhika kuwa ushahidi uliowasilishwa na shahidi wa mshtakiwa wa kwanza kwa mizani ...

Akaunti zako za Mitandao ya Kijamii Kukaguliwa na Marekani Kabla ya Kipewa Visa

WANAOTAKA kusafiri hadi Marekani sasa watahitajika kuwasilisha akaunti zao zote za mitandao ya kijamii kwa ukaguzi kabla ya kupewa visa na ubalozi wa nchi hiyo. Wizara ya Masuala ya Kigeni ya Marekani, kwenye taarifa, inasema wale ambao hawatawasilisha akaunti zao kwa ukaguzi, watanyimwa vyeti hivyo vya usafiri. Japo Wizara hiyo mwezi jana ilikuwa imetangaza masharti makali ya ukaguzi wa wanaowasilisha maombi ya visa, jana ubalozi wa Marekani Nchini Kenya uliongeza hitaji lingine la ukaguzi wa akaunti za mitandao ya kijamii ya Wakenya wanaotaka visa. “Wale wote wanaowasilisha maombi ya visa watahitajika kuwasilisha orodha ya majina au akaunti za kila mtandao wa kijamii ambao wametumia ndani ya miaka mitano iliyopita.  Orodha hiyo itawekwa katika fomu DS-160 ya maombi ya visa.  Wanaotuma maombi wanapaswa kuhakikisha kuwa maelezo yote kwenye fomu zao za maombi ya visa ni sahihi katika ya kuzitia sahihi na kutuma,” ukaeleza ubalozi wa Marekani nchini Kenya. Hii ina maana kuwa kwa...

Waluo Waanza Kuweka kando baadhi ya Mila za Kale

  JAMII ya Waluo Katika Baadhi ya Mataifa ikiwemo Kenya,Tanzania, Uganda,Ethiopia,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,Sudan na Sudan Kusini imekuwa ikishuhudia mabadiliko makubwa kuhusu utaratibu wa mazishi, huku familia nyingi zikianza kutoka kwa mila za jadi na kuanza kutenga sehemu maalum za makaburi ndani ya boma au kutumia makaburi ya umma. Mabadiliko haya yamechochewa na sababu mbalimbali, zikiwemo msongamano wa watu, upungufu wa ardhi, maisha ya mijini na mitazamo mipya ya kiimani na kijamii. Hii ni kinyume na desturi za jadi ambapo wazee wa ukoo waliamua mahali pa kumzika marehemu kulingana na jinsia, hali ya ndoa na umri. Kwa mfano, wanaume huzikwa upande wa kulia wa boma wakielekea ndani, wanawake upande wa kushoto, huku wasichana ambao hawajaolewa wakizikwa karibu na ua bomani. Hata hivyo, familia nyingi sasa zinasema mila hizo si lazima kufuatwa, hasa ikiwa marehemu hakuwa akiziamini. Bw David Omore kutoka Kakrao, Migori, alisema familia yake ilizika baba yao kwenye sehemu...

Wahuni Wanao Muhujumu Rais Dkt Samia, Bila Kujua Wao , Ndio Wanavyomsaidia

Hakuna ubishi kuwa madaraka ya urais yanabeba mvuto wa kipekee unaovuta maslahi tofauti—yakiwemo binafsi, ya makundi, na hata ya kisiasa. Katika muktadha huu, baadhi ya watu wamejitokeza kumuandama Rais Samia Suluhu Hassan kwa hoja dhaifu na tuhuma zisizo na mashiko. Makala hii inachambua kwa hoja ni kwa namna gani vitendo hivyo, visivyotegemea ushahidi, vinageuka kuwa msaada kwake bila wahusika kujua. Historia inaonesha kuwa urais umeandamwa na shutuma, fitna na hukumu zisizo na msingi, hasa nyakati za mabadiliko makubwa. - Mfano wa karibuni ni shutuma dhidi ya Rais Samia kutoka kwa baadhi ya wana CCM wenye mtazamo wa kihuni, wakiongozwa na chuki binafsi badala ya hoja za sera. > “Huwezi kumzika tembo na meno yake,” methali ya Wakikuyu inayosisitiza thamani ya uongozi wa Samia katika jicho la wapinzani wake. - Rais Samia alipokelewa kwa mashaka kutokana na jinsia yake, lakini amevuka kikwazo hiki kwa vitendo na hekima. - Amethibitisha kwa vitendo kuwa uimara wa mwanamke unaweza kuw...

Waziri Aweso Ambana Mkandarasi wa Mradi wa Maji Wilayani Karagwe

 Na Angela Sebastian; Karagwe Waziri wa maji Jumaa Aweso amewaagiza wakandarasi wa kampuni ya AFCON wanaotekeleza mradi wa kimkakati wa miji 28 wa Rwakajunju kubadili utendaji wake na kufanya kazi usiku na mchana ili kuwawezesha wananchi kupata huduma ya maji kwa wakati kuendana na malengo ya Serikali. Waziri Aweso ametoa maagizo hayo julai 25,2025 wakati alipofanya ziara maalum ya kukagua mradi wa kimkakati wa miji 28 uliopo kata Nyabiyonza Wilayani Karagwe Mkoani Kagera. Aweso Aweso amesema kuwa tayari Rais Samia katoa fedha kwa ajili ya mradi huo hivyo hakuna wakandarasi kuweka visingizio bali wachape kazi usiku na mchana ili kuwaondolea changamoto ya maji waliyokuwa nayo kwa muda mrefu wananchi wa wilaya hiyo.  "Utendaji wa kazi lazima wa ubadilike hakikisheni mnafanya kazi usiku wa mchana na mradi huu ukamilike mwezi septemba mwaka huu kama mkataba unavyowataka,fedha ipo wananchi wa Karagwe wanahitaji maji safi,salama na bora siyo maneno" amesema Aweso  Amesema ...

Waziri Mkuu Atembelea Ubalozi wa Tanzania Nchini UEA

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 25,2025 ametembelea ubalozi wa Tanzania, Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE) uliopo Abudhabi. Mheshimiwa Majaliwa alipokelewa na Balozi wa Tanzania UAE Luteni Jenerali Mstaafu,Yacub Mohamed na watumishi wa ubalozi huo.