Skip to main content

Posts

Showing posts from April 8, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mradi Wa Bwawa la Mwalimu Nyerere Wakamilika, Kutoa Uhakika wa Umeme Nchini- Majaliwa

"Serikali inaendelea kukamilisha ujenzi wa mradi wa uzalishaji umeme katika Bwawa la Julius Nyerere kwa gharama ya shilingi trilioni 6.6. Ujenzi wa mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 2,115 kwa siku umekamilika. Hadi Machi 2025. Jumla ya megawati 2,115 zimeunganishwa kwenye gridi ya taifa na hivyo kuongeza kiwango cha umeme katika gridi ya taifa kufikia megawati 4,031.7.  Kuanza kwa uzalishaji wa umeme katika mradi huo kumeongeza kiwango cha upatikanaji wa umeme wa uhakika na kuwa chachu ya kasi ya maendeleo ya nchi.   Katika kipindi cha Novemba, 2020 hadi Februari, 2025, Serikali pia imeunganisha umeme katika vijiji 4,071 kwa gharama ya shilingi bilioni 1,593 na hivyo kuwezesha vijiji vyote 12,318 vya Tanzania Bara kuunganishwa na umeme.  Hatua inayofuata baada ya kukamilisha mradi wa kupeleka umeme katika vijiji vyote, ni  kupeleka umeme kwenye vitongoji ambapo jumla ya vitongoji 33,657 kati ya 64,359, sawa na asilimia 52.3 vimeunganishwa na h...

Mbunge Mathayo Akipongeza Kituo Cha Afya Nyasho Kwa Kupata Tuzo ya Utoaji Huduma Bora 2025

Na Shomari Binda-Musoma  MBUNGE wa Jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amekipongeza kituo cha afya Nyasho kwa kupata tuzo ya utoaji huduma bora za afya kwa mwaka 2025 kwa ngazi ya kituo cha afya. Licha ya kukipongeza kituo hicho pia ameipongeza zahanati ya kwangwa kwa kupata tuzo ya utoaji wa huduma bora kwa mwaka 2025 kitaifa kwa ngazi ya zahanati. Akizungumza na GMTV leo april 9,2025 kwa njia ya simu kutoka bungeni jijini Dodoma amesema tuzo hizo zilizotolewa na Wizara ya afya zinaonyesha namna huduma nzuri zinavyotolewa ndani ya jimbo la Musoma mjini. Amesema waganga na wauguzi kwenye kituo cha afya Nyasho na zananati ya Kwangwa wanahitaji pongezi kwa kazi nzuri na kupelekea kupata tuzo hizo. Mathayo amesema hilo ni jambo kubwa kwa kuwa Wizara ya Afya kupitia ufatiliaji wake imeona huduma bora zinazotolewa maeneo hayo na kuamua kutoa tuzo hizo. Amesema afya ni suala la msingi na amefarijika kuona wananchi wanapewa huduma bora za afya kwa kuwa ni jambo jema. " Nichukue nafasi...

DC aipiga msasa Jumuiya ya Wazazi Mkinga

📍 Awataka kutumia malengo matatu ya Jumuiya hiyo, kuipa ushindi CCM 2025 📍 Awataka wawe mfano bora kwa jumuiya nyingine, kwakutokua sehemu ya makundi  📍 Aeleza mmomonyoko wa maadili, kasi ya Vijana kuuza mihadarati, usagaji na ushoga 📍 Aitaka Jumuiya kushirikiana na Wazazi kukomesha hali hiyo 📍 Mwenyekiti wa Wazazi ataka wamchague mbunge kwa faida ya wilaya badala ya Matumbo yao. 📍 Katibu Siza aahidi ushindi mkubwa kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan  Na Mwandishi Wetu, Mkinga ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM, Gilbert Kailima ambaye kwa Sasa ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga, amewapiga msasa viongozi na wajumbe wa jumuiya hiyo wilayani hapa kuelekea uchaguzi Mkuu ujao. Akizungumza katika Kongamano la Elimu na Malezi lililoandaliwa na Jumuiya hiyo wilayani hapa, April 6 2025, Mkuu huyo wa wilaya aliwataka Wazazi kuzingatia dhima na malengo ya kuanzishwa Jumuiya hiyo mwaka 1955, kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa faida ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Aliwakumbusha...

Sagini Amekabidhi Saruji Mifuko 650 Kwa Ajili ya Ujenzi na Ukarabati wa Miradi Mbalimbali

Mbunge wa Jimbo la Butiama na Naibu Waziri Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini amekabidhi mifuko ya Saruji ya 650 kwa ajili ya Ujenzi na ukarabati wa miradi mbalimbali jimboni kwake. Akizungumza kwenye ziara ya makabidhiano Mjumbe wa Baraza Kuu UWT Taifa Ndg. Mariam Sagini aliyeambatana na Watumishi kutoka Ofisi ya Mbunge kwa niaba ya Mbunge amesema kuwa saruji hizo ni awamu ya kwanza ya utekelezaji wa ahadi zake alizoahidi katika ziara zake za kusikiliza na kutatua kero za wananchi. "Mbunge Sagini yupo kazini hachoki tayari mifuko ya Saruji inaendelea kusambazwa kwa ajili ya Ujenzi na ukarabati wa Ofisi za CCM, vyoo vya shule, Zahanati na taasisi mbalimbali zikiwemo za kidini hiki ni kiashiria tosha kuwa mbunge amekuwa wa vitendo na mtekelezaji pia anatosha kuwakilisha wananchi wa Jimbo la Butiama," amesema Mariam Sagini. Naye Afisa Mahusiano kutoka Ofisi ya Mbunge Ndg. Japhet Changarawe amewaomba wananchi kushirikiana na wana-CCM wengine kumpa ushirikiano mbunge Sagini ili...

Ndumbaro Awataka Viongozi wa Dini na Jamii Kupambana na Ukatili wa Kijinsia

 Na MASHAKA MHANDO, Tanga  WAZIRI wa Katiba na Sheria Dkt Damas Ndumbaro amezitaka familia, viongozi wa dini na uongozi wa mkoa wa Tanga kuweka mikakati ya  pamoja ya kupambana na ukatili wa kijinsia ili kukomesha tabia hiyo ambayo kwa mkoa huo ni tatizo kubwa tofauti na mikoa mingine nchini.  Akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya Msaada wa kisheria ya mama Samia (MSLAC), Waziri Dkt Ndumbaro alisema ukatili wa kijinsia ni tatizo kubwa linaloathiri jamii kwa njia nyingi, na ni muhimu kuwa na mikakati thabiti ya kutokomeza tabia hiyo ili kukomesha vikundi vinavyosababisha ukatili  hususani kwa wanawake na watoto na hatimaye  kuhakikisha kwamba wahanga wanapata msaada wa haraka.  Alisema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amemtuma alete salamu katika uzinduzi huo ili kuhakikisha kuwa masuala hayo yanashughulikiwa katika Kampeni hiyo kwa kutoa msaada wa kisheria bure kwa timu hiyo. Alisema kampeni hiyo ipo katika ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Map...

Rais Mwinyi Awakaribisha Wafanyabiashara wa Uingereza Kuwekeza Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewakaribisha Wawekezaji kutoka Uingereza kuwekeza  Zanzibar katika fursa mbalimbali ikiwemo sekta ya Uchumi wa buluu, utalii,  usafiri wa baharini,  uvuvi , nishati na miundombinu ya kidijitali. Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipojumuika kwenye chakula cha jioni na Wakurugenzi wa Taasisi mbalimbali za biashara na uchumi za Uingereza kilichoandaliwa na Taasisi ya Eastern Africa Association ya Uingereza katika Jiji la London, tarehe 7 Aprili 2025. Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amesema katika kipindi cha Miaka 4 Uchumi wa Zanzibar unaendelea kukua zaidi  ya asilimia 7 kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika katika sekta mbalimbali. Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa  wawekezaji hao  kuwekeza katika zao la Mwani, ameeleza kuwa Zanzibar ndio  mzalishaji namba moja wa zao hilo Afrika ambalo soko lake linaendelea kukua zaidi.

Happy Birthday George Marato

GMTV inakutakia George Marato, heri njema na baraka tele katika siku yako ya kuzaliwa! Hongera kwa kufikia hatua nyingine ya maisha. Uendelee kuwa na afya njema, furaha, na mafanikio katika kila unachofanya. Siku hii iwe ya kipekee kwako, ikujaze matumaini mapya na kumbukumbu nzuri zisizosahaulika.