Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu ametoa wito kwa vikosi vya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) vilivyopata miradi ya nishati safi ya kupikia kuwa mabalozi wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa jamii zinazowazunguka. Mwenyekiti Kingu ametoa wito huo leo Mei 5, 2026 wakati wa ziara ya Bodi hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia inaayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika Kambi ya JKT ya Maramba mkoani Tanga. Aidha, amesisitiza vijana wanaliopo kwenye kambi hizo za JKT kupatiwa mafunzo ya namna ya kutengeneza mkaa mbadala ili waweze kutumia ujuzi huo kujiajiri na kuwa mawakala wa kutengeneza mkaa mbadala pindi watakapomaliza mafunzo yao. Kwa upande wake, akimwakilisha Mkuu wa JKT, Kanali Projest Rutaihwa aliishukuru menejimenti na Bodi ya REA kwa utekelezaji wa miradi nishati safi ya kupikia huku akiahidi kusimamia mradi huo unakuwa endelevu ili kuendelea kulinda mazingi...
Marato tv - Sauti ya Jamii