Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa kupitia utekelezaji wa Ilani ya CCM, Serikali imepiga hatua kubwa katika kufanikisha malengo ya kuhakikisha kesho bora na njema zaidi kwa vijana wa Kitanzania, wa kike na wa kiume. Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mwanamke, yaliyofanyika leo Jumamosi, tarehe 8 Machi 2025, katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha, Mhe. Rais Dkt. Samia alieleza kuwa Tanzania ina mengi ya kujivunia katika kuboresha mazingira yanayohakikisha ndoto ya usawa wa kijinsia inafikiwa nchini. “Tunapoadhimisha miaka 30 tangu Tamko la Umoja wa Mataifa la Mkutano wa Beijing, miaka 10 ya Malengo Endelevu ya Dunia na miaka 5 ya Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa, ni fursa ya kutathmini mafanikio makubwa yaliyofikiwa na kutambua hatua zaidi zinazohitajika ili kuhakikisha kila msichana na mwanamke hapa nchini anapata nafasi ya kufikia ndoto zake,...