Skip to main content

Posts

Showing posts from December 10, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Mwigulu Azungumza na Viongozi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 11, 2025 amezungumza na watendaji na viongozi wa Sektretarieti ya Maadili kwa viongozi wa Umma, katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo jijini Dodoma. Akizungumza na watendaji hao, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema kuwa yapo maeneo ambayo bado rushwa imekidhiri lakini watumishi wake hawatambuliki kama sehemu ya viongozi kwa majukumu yao. “Ni muhimu kufanya mapitio ya haraka ya tamko ili nao waweze kujumuishwa”

Uzinduzi wa Mashindano ya Mpira wa Miguu ya Jimbo la Butiama Katika Kata ya Kamuegegi

Tumezindua rasmi mchakato wa kuunda Timu ya Mpira wa Miguu ya Jimbo la Butiama, hatua ya kwanza ikiwa imefanyika leo katika Kata ya Kamugegi! Tukiwa na dhamira ya kuijenga Butiama kupitia michezo, umoja na kukuza vipaji vya vijana.  Uzinduzi huu umehudhuriwa na Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Kamugegi, Wilson Kinguye, na Diwani wa kata ya Buruma mh Mogela Mbonosi pamoja na viongozi wengine wa Kata—ikiwa ni ishara ya mshikamano na malengo ya pamoja kwa maendeleo ya vijana wetu. Mchakato huu unaanzia katika ngazi ya Vijiji, kisha Kata—zikijumuisha Kata zote 18—hadi kupatikana kwa timu moja mahiri itakayolibeba na kuliwakilisha Jimbo la Butiama kwa heshima, nidhamu na ushindani. Huu ni mwanzo wa safari endelevu ya kuimarisha, uainishaji, ukuaji wa vipaji, ushirikiano, mshikamano kwa vijana, amani, umoja na afya njema kupitia nguvu ya michezo.

Slovakia Yafungua Ubalozi Tanzania

Balozi Mteule wa kwanza wa Slovakia nchini Tanzania, Mhe. Ivan Lančarič amewasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe jijini Dodoma Desemba 10, 2025.  Mhe. Lančarič amewasilisha Nakala hizo za Hati za Utambulisho kufuatia nchi yake kufungua Ubalozi nchini Mwezi Desemba 2025.  Akipokea Nakala za Hati hizo, Mhe. Maghembe amesema ufunguzi wa Ubalozi huo ni matokeo ya utekelezaji uliotukuka wa Diplomasia ya Tanzania duniani, chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.  "Ubalozi huu utakuwa kichocheo cha kukuza ushirikiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Slovakia, hususan katika nyanja za uwekezaji, biashara na utalii", Dkt. Maghembe alisema. Kwa upande wake, Mhe. Lančarič alieleza ufunguzi wa ubalozi mpya nchini Tanzania ni utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo, ambayo inalenga kutanua wigo wa uwakilishi barani Afrika. Alisema Ubaloz...

Mwanafa Akutana na Baraza la Madiwani Muheza

📍Awataka wahamasishe mapato katika kata zao, waiongezee uwezo halmashauri *Na: Mwandishi wetu, Muheza* MBUNGE wa Jimbo la Muheza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma (MwanaFA), amefanya kikao kizito na madiwani wote wa wilaya hiyo leo, akisisitiza umuhimu wa **umoja, uwazi na utekelezaji wa haraka** wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Akizungumza na baraza hilo jipya la madiwani, Mhe. MwanaFA aliwapongeza kwa ushindi mnono wa Oktoba 29 na kuwataka sasa kusahau yaliyopita na kuungana pamoja kuleta maendeleo Muheza. > “Ushindi huu unatakiwa sasa tuongeze ushirikiano na umoja, na **tuvunje makundi** kwa sababu sasa Muheza ni Moja,” Mhe. MwanaFA alisisitiza, akiongeza kuwa yeye atashirikiana na madiwani wote bila kubagua. *KUHAMASISHA MAPATO YA HALMASHAURI** Mbunge huyo aliwakumbusha madiwani kuhusu umuhimu wa kuhimiza watendaji wakusanye mapato ili halmashauri iweze kupata uwezo wa kuwahudumia wananchi kwa miradi ya Halmashauri. Alisema halmas...

Serikali yatangaza mipango mikubwa sekta ya elimu

  Waziri wa Elimu Sayansi na teknolojia, Mh. Profesa Adolf Mkenda amesema serikali imejipanga kuanzisha mfumo wa elimu ya lazima ya miaka 10 ifikapo mwaka 2028 ili kuongeza ubora wa taaluma ya elimu nchini. Akizungumza mapema hii leo Disemba 10, 2025,  Profesa Mkenda katika Mkutano wa mawaziri na waandishi wa habari uliyoandaliwa na idara ya habari maelezo katika ofisi ya kituo cha ukombozi jijini dar es salaam ambapo pia amesema ustawi wa sekta ya elimu chini ya serikali ya Rais Samia umekua kwa zaidi ya asilimia 75 ambapo wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi wamefanikiwa kwenda sekondari. Aidha, amesema kuwa serikali imejipanga kuongeza masomo ya lazima ya biashara na kiingereza ili kuweza kusaidia wanafunzi wenye ndoto za kibiashara kuweza kufundishwa mbinu mbalimbali na hatua muhimu za kibiashara ili kuwasaidia wenye ndoto za ufanyaji biashara. Pia, Waziri Mkenda amesema katika kutambua umuhimu wa elimu ya amali nchini serikali imejipanga kutoa elimu ya ufundi katika kida...