Skip to main content

Posts

Showing posts from October 26, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Majaliwa Ashiriki Sherehe za Kuapishwa Rais Herminie wa Jamhuri ya Shelisheli

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na viongozi wa nchi za India, China, Mauritius na Comoro kwenye sherehe za kumuapisha Rais wa Jamhuri ya Shelisheli, Dkt. Patrick Herminie zilizofanyika kwenye Uwanja wa Umoja, jijini Victoria nchini humo. Waziri Mkuu ambaye amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, alikuwa miongoni mwa viongozi hao wakuu wakiwemo Makamu wa Rais, Mawaziri Wakuu na viongozi wa juu kutoka vyama rafiki vya siasa. Rais Herminie aliapishwa jana (Jumapili, Oktoba 26, 2025) kuwa Rais wa sita wa nchi hiyo. Viongozi hao ni Makamu wa Rais wa India, Bw. Chandrapuram Ponnusamy Radhakrishnan; Waziri Mkuu wa Mauritius, Dkt. Navinchandra Ramgoolam; Makamu wa Rais wa Chama cha Chinese People’s Political Consultative Conference (CPPCC) Bw. Gao Yunlong na Rais wa Baraza la Mawaziri la Kamisheni ya Bahari ya Hindi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro, Bw. Mohamed Mbae. Mheshimiwa Waziri Mkuu ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ...

Majaliwa Awasili Shelisheli Kumwakilisha Rais Dkt. Samia Uapisho wa Rais Mteule Dkt. Patrick

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 26, 2025 amewasili Seychelles kwa ajili ya kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye uapisho wa Rais mteule wa sita wa nchi hiyo Dr. Patrick Herminie  Tume ya Uchaguzi ya Taifa ilimtangaza Mheshimiwa Dkt. Patrick Herminie wa Chama cha United Seychelles (US) kuwa mshindi baada ya kumbwaga Rais aliyekuwa madarakani, Mheshimiwa Wavel Ramkalawan wa Chama cha Linyon Demokratik Seselwa (LDS).  Mheshimiwa Dkt. Patrick Herminie alipata asilimia 52.7% ya kura, huku Rais Wavel Ramkalawan akimaliza wa pili kwa kupata 47.3% ya kura.